Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Jeshi la Polisi nchini linawashikilia watuhumiwa watano kwa tuhuma za kumuua Castory Casian Madembwe, Mtumishi wa TASAAF Mkazi wa Ipuli Mkoani Tabora, kisha kuufukia mwili wake nyuma ya nyumba aliyopanga mmoja wa
watuhumiwa hao na juu yake kupanda nyanya.
Watuhumiwa hao ni Nelson Samwel, Mkazi wa Ipuli Tabora (huyu ndiye mpangaji wa nyumba ambayo mwili huo ulifukiwa), Salum Heri, Mkazi wa Kadinya, Bathoromeo Maiko, Mkazi wa Isevya, Juma Ramadhani, Mkazi wa
Kidatu na Mohamed Hamad, Mkazi wa Uledi. Mtuhumiwa mmoja ambaye ni Careen Matemba mke wa Nelson Samwel anaendelea kutafutwa kwani amekimbia baada ya kugundua wenzie wamekamatwa.
Watuhumiwa hawa wanatuhumiwa kutekeleza tukio hilo la mauaji Juni 10,2025 huko Ipuli, Tabora kisha kuufukia mwili wa Castory Casian Madembwe na kupanda nyanya juu ya shimo walilochimba nyuma ya nyumba anayoishi Nelson Samwel ili isigundulike.
Soma Pia: Aliyetekwa akutwa ameuawa na kuzikwa nyumbani kwa mtu Tabora
Pamoja na watuhumiwa kumuua Castory Casian Madembwe bado walimpigia simu Mama yake na kumwambia mtoto wako ametekwa ukitaka tumwachie tuma fedha na kabla ya kukamatwa watuhumiwa hao Mama huyo alikuwa amesha watumia shilingi milioni tano.