Watu wa ajabu ajabu waliopo na wanaozidi kushika kasi

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
48,475
Reaction score
70,102
1. Watetezi wa Udikteta

Kumeibuka kundi kubwa la watu katika huu mtandao wakihusudu na kutamani kutawaliwa kidekteta kwa imani kwamba madikteta ndio huleta maendeleo kwa kasi. Naamini ni ujinga wa historia umewajaa vichwani mwao, hakuna mtu mwenye akili atakayefuatilia Historia ya madikteta akatamani aina ya utawala wao.

2. Watetezi wa Russia

Hawa wako kama madebe matupu, hoja zao ni dhaifu sana, conspiracy na uongo mwingi.
Sehemu kubwa wanakimbilia kujenga hoja zao kupitia Marekani au West. Kwa sasa wamejaa jukwaa la Kimataifa na wanaanzisha nyuzi kila dakika.

3. Wanaharakati dhidi ya ushoga

Sijawahi kuelewa hata hoja ya moja ya watu walio obsessed/au wanashughulishwa sana na ushoga. Sasa wamefikia mahali wanasema mashoga wauwawe tu. Siamini kama ushoga unapaswa kupewa mjadala wowote na kufanyika sehemu ya ajenda muhimu za nchi.

4. Watetezi wa ndoa za utotoni

Sijwahi kukutana na hoja ya maana hasa ya kumfanya mtu ashadadie au akubali binti yake wa miaka 14 aolewe, jambo la ajabu watetezi wakubwa wa hili ni wanaume!

5. Wenye chuki na upinzani

Nchi hii upinzani haujawahi kushika madaraka makubwa ila kuna watu wanauchukia upinzani na wanasiasa wake kana kwamba shida zote au shida yoyote ya nchi hii imetokana na uwepo.

6. Wanaopinga Katiba Mpya
Ni vigumu kuelewa kinachomfanya mtu kutokwa na povu akipinga katiba mpya kwenye hii nchi. Watakuambia ni gharama sana lakini kila mwaka wanakimbiza mwanga, watakuambia katiba mpya haileti ugali mezani lakini hata hiyo kuukuu nayo haiwaletei ugali mezani kwa sasa, ni
 
punguza hasira na makasiriko yoda why tupangiane haya ni maisha kila mmoja anafanya vile anavoona inafaa why uponde kisa mitizamo yao hvo ivo kuna watu wanakuona kilaza kama unavowaona
 
1. Watetezi wa Udikteta

Kumeibuka kundi kubwa la watu katika huu mtandao wakihusudu na kutamani kutawaliwa kidekteta kwa imani kwamba madikteta ndio huleta maendeleo kwa kasi. Naamini ni ujinga wa historia umewajaa vichwani mwao, hakuna mtu mwenye akili atakayefuatilia Historia ya madikteta akatamani aina ya utawala wao.

2. Watetezi wa Russia

Hawa wako kama madebe matupu, hoja zao ni dhaifu sana, conspiracy na uongo mwingi.
Sehemu kubwa wanakimbilia kujenga hoja zao kupitia Marekani au West. Kwa sasa wamejaa jukwaa la Kimataifa na wanaanzisha nyuzi kila dakika.

3. Wanaharakati dhidi ya ushoga

Sijawahi kuelewa hata hoja ya moja ya watu walio obsessed/au wanashughulishwa sana na ushoga. Sasa wamefikia mahali wanasema mashoga wauwawe tu. Siamini kama ushoga unapaswa kupewa mjadala wowote na kufanyika sehemu ya ajenda muhimu za nchi.

4. Watetezi wa ndoa za utotoni

Sijwahi kukutana na hoja ya maana hasa ya kumfanya mtu ashadadie au akubali binti yake wa miaka 14 aolewe, jambo la ajabu watetezi wakubwa wa hili ni wanaume!

5. Wenye chuki na upinzani

Nchi hii upinzani haujawahi kushika madaraka makubwa ila kuna watu wanauchukia upinzani na wanasiasa wake kana kwamba shida zote au shida yoyote ya nchi hii imetokana na uwepo.

6. Wanaopinga Katiba Mpya
Ni vigumu kuelewa kinachomfanya mtu kutokwa na povu akipinga katiba mpya kwenye hii nchi. Watakuambia ni gharama sana lakini kila mwaka wanakimbiza mwanga, watakuambia katiba mpya haileti ugali mezani lakini hata hiyo kuukuu nayo haiwaletei ugali mezani kwa sasa, ni
Huko kwingine tutavumiliana ila hapo kwenye ushoga kwa kweli naomba ubaki mwenyewe, sikuungi mkono.
 
7. Watetezi wa mabeberu na USA
Kila kukicha machafuko Africa sio congo, sio somalia, sio Ethiopia Wala Nigeria.

Africa magharibi na Kati kote kumetapakaa vikundi vya uasi serikali zinapinduliwa

Mabeberu wanazisaidia serikali mikopo ya kijeshi ili viwanda vyao vya silaha vipate masoko.

At the same time,

Mabeberu hao hao wanadhamini vikundi vya uasi ili waibe rasilimali kwa mgongo wa kuja kulinda amani sehemu zenye machafuko.

Hili Hapa Gari la kulinda UN CONGO DRC, limepata ajali limekutwa na viroba vya madini[emoji116]
JamiiForums-1570400833.jpg
 
Kuna makundi mawili hujayataja...kuna Wale waumini WA mfumo dume ...wao Kiongozi mwanamke sio kiongozi...

Na kuna Wale WA makabila na dini..
Kiongozi mradi sio WA dini yake basi hafai ..wengine mradi sio kabila lake hafai
 
Back
Top Bottom