Watu wa content na masuala ya ujasiriamali

Watu wa content na masuala ya ujasiriamali

mshamba mchangamfu

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2015
Posts
338
Reaction score
91
Wakuu salama,

Mimi si mtaalam sana ni maswala ya habari na vyombo vingi vya habari natambua ni huru inapokuja kwenye maswala ya nini kirushe au kiandike (kama tu hakivunji sheria) kipo huru ila inapokuja maswala ya ujasiliamali kuna kuwa na upotoshaji mkubwa sana hasa wale inspirational speakers au wajasiliamali wenyewe wanapotoa ushuhuda ni ngumu ku spot kipi hasa ni uongo mtu anapoongea ila kuna vitu havihitaji rocket science au uelewa wa BS101 kuelewa kuwa hapa hakuna uhalisia au hii stori imepambwa sana

Mfano mdogo vipindi vingi vya redio mchana (saa sita mpaka saa nane hivi) vimelenga kina mama au wadada wa hali zetu za kawaida sana ( ali maarufu wa majumbani) naamini hawa ndio target audience mdada ambae mtaji wake wa maandazi unaweza ukawa ni wa kilo 4, mafuta chupa ya nusu lita na kuni mzigo mmoja (kwa vipimo vyetu vya uswazi)

Lakini unakuta anapiga simu anashauriwa akaombe tender ya kuuza maandazi kwenye shule 20 atakuwa tu milionea kesho na kwa hesabu za haraka haraka unaona inawezekana ila uelewa wa kuomba hizo tenda mtaji wa kuweza kuhimili mahitaji ya shule 20 anaupata wapi na since anaenda kuwauzia watoto wetu kuna service standard atapewa unlike akiwa tu mama Kasim anaechoma mandazi barazan kwake nitoe tu rai kwa media houses, media zinapawa kubwa sana ila ni media
 
Back
Top Bottom