Watu wa Dar kanusheni na hili

LUBEDE

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2013
Posts
4,320
Reaction score
6,686
Watu wa Dar bwana!
Kabla hujaenda ukimpigia simu anakwambia
karibu sana kaka ukija usiache kunitafuta..
Ukifika ukampigia kwanza anakuuliza
umefikia wapi, unamwambia nipo Kawe,
utasikia nipo Kibaha kuna issue
nashughulikia nitakuchek kesho....
Kesho ndo hutaiona simu yake ng'oo... Ukimpigia simu kumwambia kesho naondoka, utasikia
mbona fasta kaka, daah sema umekuja
wakati mbaya sana, sasa hivi nipo taiti kiaina ila ukija tena tutakutana tu????...
Wote sound zao hizo hizo, utadhani
mwalimu wao mmoja????
Afu wao wakija huku mkoani,
anataka uwe nyuma yake 24/7, utadhani
mnatafuta wadhamini?
Stori zake sasa..
Hivi huku mikoani mnaishije..? Hakuna
mzunguko wa hela kabisa????..
Hiyo mizunguko ya hela huko Dar ingekuwepo
si wote mngekuwa Bakhressa????...
aseeh... acheni hizi
tabia,
mnatukera sana sisi wa mkoani..
 
Ukimwambia Wiki ijayo Mi nageuza Kijijni, vipi kuna chochote cha kuwapelekea..atakwambia ngoja niende kasi alafu ntakucheki..

Siku ikifika mkumbushie sasa kuhusu zawadi kwa Bi Mkubwa..aisee hivi kesho ndiyo Safari..

Nilitingwa kidogo lakini mwambie Bi Mkubwa Desemba ntakuwa huko ,ngoja nijipange pange kwanza .
 
Bongo bana yani siyo wanaume wa Dar na mikoani yani wote mnaishi kimajungumajungu, kimungumungu, kwa kubahatishabahatisha, kisengesenge na kijingajinga.

MNAISHI MAISHA YA AJABU SANA!

FANYENI KAZI
 
Bongo bana yani siyo wanaume wa Dar na mikoani yani wote mnaishi kimajungumajungu, kimungumungu, kwa kubahatishabahatisha, kisengesenge na kijingajinga.

MNAISHI MAISHA YA AJABU SANA!

FANYENI KAZI
aisee upo nchi za watu umevimba mapumbu halafu unatukana wabongo eti tunaishi kisengesenge!
Shika adabu yako mwana usiye na haya wewe.
 
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
 
Umenikumbusha tukio hili:
Mwaka jana nilienda kikazi mkoa wa Lindi kufanya Technical Audit kwenye miradi ya barabara. Sasa jamaa mmoja (school mate (sekondari)) katika wilaya mojawapo ni mganga mkuu wa mifugo (w), tulipoonana alinichenga hadi nikamshangaa. Sijui alidhani nitakuwa mzigo kwake? Hakujua nilifika pale kufanya kazi ambayo nilikuwa nalipwa vizuri tena vizuri sana!
Ndugu yangu EC kama unapita hapa JF elewa kwamba sikuwa na haja ya kufika kwako.
 
ha ha hahahah aahaha haahaha,pole sana mkuu kwa mkasa..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…