MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 14,588
- 32,361
Nimesikitishwa sana na ninachoona mtandaoni kuhusu watu wa Karatu kukumbwa na mafuriko na nyumba zao kuzingirwa na maji. Mungu awatangulie kwenye hiki kipindi kigumu. Lakini nimeshangaa imekuwaje watu wa Karatu kuanza kujenga kwenye bwawa ambalo kila mwaka hujaa maji? Inakuwaje serikali iruhusu ujenzi bwawani? Au kuna watu wa Msimbazi Dar walihamia Karatu na kupeleka akili zao huko?
Ikumbukwe Karatu ipo kwenye muinuko mkubwa hivyo kusema kukumbwa na mafuriko ni jambo gumu mno. Ninadhani sis raia tutumie sana akili kabla ya kufanya maamuzi ya kujenga. Serikali nayo isitoe vibali vya ujenzi kiholela.