Watu wa kuchora ramani za nyumba punguzeni udalali

FRANCIS DA DON umeongea mambo yaneleta maana...

Lakini kwetu sidhani kama tunazungumzia ubunifu Bali ramani tu za nyumba bila ya kuwa na ubunifu Wa mchoraji

Mtu yupo Kimara anachora ramani ya nyumba itakayojengwa Buza bila ya kufika site, ndiyo alipwe 15% ya thamani ya jengo litakalojengwa?
 
Raman mbona hata wewe mwenyewe unachora tu sikuhizi kuna progran playstore nyingi tuu sasa hiv na vipimo kabisa

Ramani ni floorplan tuu! Hayo ma elevation sijui front view sijui side view sijui 3D ni mbwe mbwe tu ukisha pandisha boma kupaua fundi wa kupaua atakuja na raman yake , wa maji atakuja na ramani yake
 
There u r.
Hapa napandisha floor nne.
Ramani nimechora mwenyewe
Structural drawing mwenyewe
Mimi ndio injinia na
Mimi ndio client. Kazi iendelee πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
Upo sahihi kabisa, sema kwa hizi nyumba zetu za vyumba vitatu, sitting, dining, jiko, choo na store ndio tunauziwa kwa 300k.

Otherwise upo sahihi.
 
Kwa hiyo mtu aliyeenda shule amekuwa sawa na layman aka download mzigo playstore aka design ghorofa, electrical drawings, plumbing, estimations nk? Acheni utani na fani za watu, sema vyumba viwili, sebule nk ndio utafanya hivyo.
 
Likianguka likaua ukiwa umelipwa kiasi kikubwa inakuwaje
Kuna professional indemnity ambayo mwana taaluma anakuwa amekata kama bina ya liabilities mbali mbali ama dharura kama hizo zikitokea, unahitaji pesa kuilipia hii bima. Pia utahitaji pesa kuweka mawakili wazuri. Pia big risks zina require mtu alipwe accordingly.., hii ndio mantiki ya kustahili malipo sawia na β€˜risk taken’
 
Sasa hiyo sio ramani, ni mchoro wa β€˜artist’ tu. Hai qualify criteria za kuitwa ramani
 
Likianguka likaua ukiwa umelipwa kiasi kikubwa inakuwaje
Kwa kuwa yeye ni injinia basi analeta ujuaji mwingi..... iko hivi athari haipangwi na mwanadamu lakini ni matokeo ya kazi ya mwanadamu..... majengo mangapi yametumia wasanifu wakubwa na yamedondoka? Hayo ni matokeo lkn kabla huwezi panga kazi yako iwe na uhakika wa kutoharibika..... aendelee kusubiri 15% ya kila kazi
 
Nimeshangaa hoja yake kwamba hawezi kulipwa kidogo kwakuwa likitokea janga atawajibika
 
Ikiwa ameongea na seems ni fani yake kwanini isiwezekane?

Labda kama ulishawahi kujenga ghorofa lakini mimi naona kama ina-make sense.
 
Ukitaka kujenga tembelea nyumba kumi, dukua ramani Kisha boredha ujenge Yako ya 11. Ujasusi wa ujenzi
 
Me nlidaka kwa 30k faster nikatembea zangu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…