Watu wa kukera zaidi duniani ambao hubidi tu kuwavumilia

Watu wa kukera zaidi duniani ambao hubidi tu kuwavumilia

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
48,475
Reaction score
70,102
1. Wanaoamini dunia sio duara bali ni tambarare(Flat earthers)

2. Wapinga chanjo(anti-vaxxers)

3. Wanaomini benki au pesa zote duniani ni mali za Rothschild au sijui Wayahudi gani fulani huko duniani.

4. Wanaoamini Illuminati na Freemason ni makundi yenye nia ovu au conspiracy ya kutawala dunia.

5. Wanaoamini ushoga ni ajenda ya watu au kikundi fulani ambacho kinafanya jitihada kuueneza duniani.

6. Wanaosema hata dini inasema... hata misaafu inasema.

7. Wanaoweka msisitizo wa jambo kwa kuanza na maneno ya "kusema kweli..."

8.Wanoashika shika mtu Bega, mikono n.k wakati wanaongea.

9. Wanaorudia rudia maneno "sijui umenielewa" kila mara wakati wa mazungumzo.

10. Wale ambao kila story na wao imewahi kuwatokea pia au wanamjua mtu iliyowahi kumtokea.

11. Waanzishaji wa story za mpira kiholela wakati unahitaji utulivu.

12.Wanaomshukuru Rais na chama chake kila mahali wanapozungumza mbele ya hadhira yoyote ile, hata kama jambo halihusiani kabisa.

13.Wale ambao kila tukio linalotokea na kuvuma/kutrendi limepangwa na "system"/ utawala ili kupooza jambo fulani.
 
Wazee wapumbavu waliotelekeza watoto wao kwa visingizio uchwara kuwa "akikua atanitafuta". Mtoto asipofanikiwa akawa chokoraa mzee anamkana, akifanikiwa mzee analeta mikwara mbuzi ya kumlaani asipomsaidia.
 
Vp kuhusu hawa jamaa wanaoamini Dunia ni flat yaani Flat-Earthers??
20240831_171624.jpg


20240831_171655.jpg
 
12. Wale wanaokerwa na hayo mambo yote 11 yaliyoorodheshwa hapo juu.

Ova
 
Wanaosema hata dini inasema... hata misaafu inasema..
Hawa wanakera zaidi maana wanadhani miungu yao tu ndiyo ya kweli. Utadhani wanaumiliki ukweli humo kwenye vitabu vyao. Ndiyo wanaongoza kwa unafiki
 
1. Wanaoamini dunia ni duara(Flat earthers)
2. Wapinga chanjo(anti-vaxxers)
3. Wanaomini benki au pesa zote duniani ni mali za Rothschild au sijui Wayahudi gani fulani huko duniani...
Hii namba 11 🤣🤣🤣
 
1. Wanaoamini dunia ni duara(Flat earthers)
2. Wapinga chanjo(anti-vaxxers)
3. Wanaomini benki au pesa zote duniani ni mali za Rothschild au sijui Wayahudi gani fulani huko duniani..
Mwanamke anaetaka nimhudumie au nimpe hela wakati ana akili timamu, nguvu za kufanya kazi na kapewa uhuru na nyenzo zote za kutafuta hela katika hii dunia ya 50/50.
 
Hawa wanakera zaidi maana wanadhani miungu yao tu ndiyo ya kweli. Utadhani wanaumiliki ukweli humo kwenye vitabu vyao. Ndiyo wanaongoza kwa unafiki
Huwa inaboa sana kila mara mtu anajenga hoja zake kwenye mjadala secular kabisa kwa kutoa rejea ya maandiko ya kitabu chake cha dini ambacho wengine wala hawana habari nacho, au wengine wanajidai wako smart zaidi wana quote vyote viwili ku balance, ujinga mtupu.
 
Back
Top Bottom