Watu wa kukera zaidi duniani ambao hubidi tu kuwavumilia

Watu wa kukera zaidi duniani ambao hubidi tu kuwavumilia

Hii namba 11 🤣🤣🤣
Mtu anaweza kukuanzishia story ndefu za mpira mida ambayo uko na ishu nyingine tofauti kabisa, unamkataa kiana lakini wala hakati story yenyewe, anazidi kuja tu.
 
Wana ziita ndege za kijeshi eti ni "roketi" huwa wananiuzi kweli




Kuna wengine kila wakika wao wanawaza mambo ya mipira tu
 
Wapinga Chanjo ,hawa ni watu wenye kutaka umaarufu tu ,kimsingi huwezi kusema kwamba chanjo ni mbaya na kwamba ina madhara hivyo watu wasusie na wakati mama akiwa mjamzito ataendenda hospitali atachanjwa bila bughuza yeyote,mtoto akizaliwa ataenda clinic atapata Chanjo zote in different series bila maneno maneno yeyote ila akishakuwa mtu mzima ameshiba ugali na bamia anakuja kusema Chanjo ni mbaya Sana hazifai zina madhara makubwa sana, hivi kama kweli watoa chanjo Wana Nia mbaya mbona huku Watoto wakiwa tokea wakiwa wadogo mbona hampingi ila huku tu kwa watu wazima ndio Chanjo inamadhara ,alafu hao hao wapingaji wakitaka kusafiri kwenda nje ya nchi Ili kukidhi vigezo,wanajipeleka wenyewe kudungwa bila bughuza yeyote ila wakija mbele ya kamera makoo yanawa wakauka kulaani Chanjo . Kamwe usimuamini binadamu hata kidogo.
 
Umewasahau na wale wanaojifanya mjomba wao alipata msichana mzuriii,alivyoenda nae getho alivyotaka kuzima taa yule msichana akasema subiri akanyoosha mkono kutoka kitandani mpaka kwenye switch!wanakera sana
By the way hapo number moja sijaelewa
 
13. wale wanaobishana juu ya uwepo wa mungu
 
1. Wanaoamini dunia sio duara bali ni tambarare(Flat earthers)

2. Wapinga chanjo(anti-vaxxers)

3. Wanaomini benki au pesa zote duniani ni mali za Rothschild au sijui Wayahudi gani fulani huko duniani.

4. Wanaoamini Illuminati na Freemason ni makundi yenye nia ovu au conspiracy ya kutawala dunia.

5. Wanaoamini ushoga ni ajenda ya watu au kikundi fulani ambacho kinafanya jitihada kuueneza duniani.

6. Wanaosema hata dini inasema... hata misaafu inasema.

7. Wanaoweka msisitizo wa jambo kwa kuanza na maneno ya "kusema kweli..."

8.Wanoashika shika mtu Bega, mikono n.k wakati wanaongea.

9. Wanaorudia rudia maneno "sijui umenielewa" kila mara wakati wa mazungumzo.

10. Wale ambao kila story na wao imewahi kuwatokea pia au wanamjua mtu iliyowahi kumtokea.

11. Waanzishaji wa story za mpira kiholela wakati unahitaji utulivu.

12.Wanaomshukuru Rais na chama chake kila mahali wanapozungumza mbele ya hadhira yoyote ile, hata kama jambo halihusiani kabisa.
Bila kumtaja lukasi mwashamba uzi haujakamilika
 
Tuache na rais wetu...
Kama unataka nivuruge mada yako hapa endelea ....
 
Mwanamke anaetaka nimhudumie au nimpe hela wakati ana akili timamu, nguvu za kufanya kazi na kapewa uhuru na nyenzo zote za kutafuta hela katika hii dunia ya 50/50.
Mwanaume anayetaka kupikiwa kufuliwa na kufanyiwa kazi nyingine za nyumbani, pamoja na kupewa utii na mwanamke ilihali hawajibiki kiuchumi juu ya huyo mwanamke, na ana uwezo wa kujifanyia hayo mwenyewe
 
Back
Top Bottom