Watu Wa Kusini na neno "Kugoma"

Watu Wa Kusini na neno "Kugoma"

Katavi

Platinum Member
Joined
Aug 31, 2009
Posts
42,023
Reaction score
12,811
Nilipata wakati mgumu nilipokuwa Mtwara mwaka jana hasa katika matumizi, matamshi na maana ya baadhi ya maneno ya kiswahili. Ila maana ya neno "kugoma" ilinitatiza sana na ilinichukua muda kuizoea. Wao kugoma ni "KUFOKA", sina uhakika kama maana hii ni kiswahili sanifu.
 
Kugoma=kufoka=wametafsi vibaya.
 
Nilipata wakati mgumu nilipokuwa Mtwara mwaka jana hasa katika matumizi, matamshi na maana ya baadhi ya maneno ya kiswahili. Ila maana ya neno "kugoma" ilinitatiza sana na ilinichukua muda kuizoea. Wao kugoma ni "KUFOKA", sina uhakika kama maana hii ni kiswahili sanifu.
Mkuu hukuipata na KUPEGA?
 
Kugoma ni kugombeza, ila kweli kusini nako kuna mambo! Kuchovya tonge kwenye mboga wanaita 'Kupamba'.........
 
Sikuipata ndio nini?
Kutembea haraka. Mi naiona imetulia kwa sababu kwenye kiswahili
tuna Kunyata kupega hakuna lakini hiyo hiyo kunyata ukiongea kusini
inamaanisha kuwa na sura mbaya.
 
Nilipata wakati mgumu nilipokuwa Mtwara mwaka jana hasa katika matumizi, matamshi na maana ya baadhi ya maneno ya kiswahili. Ila maana ya neno "kugoma" ilinitatiza sana na ilinichukua muda kuizoea. Wao kugoma ni "KUFOKA", sina uhakika kama maana hii ni kiswahili sanifu.
Nafikiri imekaa badala ya kugomba!
 
Kutembea haraka. Mi naiona imetulia kwa sababu kwenye kiswahili
tuna Kunyata kupega hakuna lakini hiyo hiyo kunyata ukiongea kusini
inamaanisha kuwa na sura mbaya.
Ahahahahaaah!! Mkuu umeniongezea hilo neno la "kunyata", nalo nilisikia "baah ntu mwenyewe kanyata"
 
Kugoma ni kugombeza, ila kweli kusini nako kuna mambo! Kuchovya tonge kwenye mboga wanaita 'Kupamba'.........
Ahahahaaah!! Sijui ni maneno ya asili wanayatafsiri kama yalivyo.
 
Kwahiyo mfano, mbuzi kagoma.....inakuaje hapo??amefoka ama?/
 
Sasa mkuu ukitembelea kusini ya unguja si utachoka na neno "kusimika" usije ukalitamka huko.au neno tembo.
Hii ni kuonesha kwamba lugha hutofautiana katka lahaja zake na hapo ndipo tunapopata hasa maana ya lahaja
 
toa maana mkuu, utakuwa umesaidia sana
 
Maana nyingine kwamba haijaguswa ni ile ile ya "kuacha/kususia kufanya kazi mpaka masharti fulani yatimizwe".
 
Back
Top Bottom