Watu wa Kusini pelekeni watoto shule, kuzamia South Africa itazidi kuwaangamiza

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2012
Posts
21,387
Reaction score
44,030
Inasikitisha sana kwa kinachoendelea dhidi ya vijana wanaozamia South Africa kutafuta maisha huku wakiwa hawana elimu wala ujuzi wowote. Wengi wao ni kutoka wilaya ya Temeke hasa kata ya Mbagala. Ambapo pia wengi wao ni watu wa mikoa ya kusini kwa maana ya Lindi na Mtwara. Maisha wanayoishi huko SA yanasikitisha sana.

Mimi siandiki kiushabiki wala kwa kusikia stori za vijiweni. Mwaka 2016 mtaani kwetu kulikuwa na dogo kibaka msumbufu sana. Kilichokuwa kimebakia ilikuwa ni watu kumuua tu. Nikamwonea huruma na kukaa nae chini na kumuuliza ni kitu gani anaweza fanya ili aachane na uhalifu. Akajibu anataka awe la Library ya muziki. Nikampa laki 3 aanzishe biashara. Baada ya kumpa ghafla dogo akapotea. Ilipopita miezi kadhaa nikapokea ujumbe Facebook toka kwa dogo kumbe laki 3 alitumia kama nauli kutimkia South Africa.

Kupitia posts zake za FB niligundua dogo yuko na urafiki na watu wanye viashiria vyote vya uhalifu. Tokea wakati huo ndo nikaanza kujua mambo mbalimbali kuhusu watu wanaozamia South. Vijana wengi kule wanaishi maisha mabovu mno ya kudhalilika. Ukiwa kwenye magroup ya FB kila mara huwa wanapost matatizo tu. Watu kuchanganyikiwa, kukosa pa kuishi, kukamatwa na polisi na mara kadhaa vifo.

Wenyewe wanajiita mabaharia na hujiona wapambanaji kwelikweli huku kiuhalisia wanapoteza muda. Mbagala wanaiita BACK CITY.

Sipendi ukabila wala ukanda ila katika hili watu wa Dar hasa Temeke, Pwani, Lindi na Mtwara hamuwezi kwepa lawama. Kwenye wanaodhalilika South Africa sijawahi ona jina la watu wa mikoa kama Njombe, Mbeya au Kilimanjaro.

Kupitia hii post niwapongeze wakinga na wanyakyusa kwa kupenyeza biashara zao Zambia na Malawi. Nimeona wazambia wakiwatupia lawama wanyakyusa na wakinga kwa kuwavuruga kibiashara.
 
Sipendi ukabila wala ukanda ila katika hili watu wa Dar hasa Temeke, Pwani, Lindi na Mtwara hamuwezi kwepa lawama. Kwenye wanaodhalilika South Africa sijawahi ona jina la watu wa mikoa kama Njombe, Mbeya au Kilimanjaro. Kupitia hii post niwapongeze wakinga na wanyakyusa kwa kupenyeza biashara zao Zambia na Malawi. Nimeona wazambia wakiwatupia lawama wanyakyusa na wakinga kwa kuwavuruga kibiashara.
Pambana na maisha yako achana na maisha ya watu
 
Kwahiyo kupeleka watoto shule ndo kumaanisha kwamba hawatozamia SA au ughaibuni.!
 
Ni kweli usemayo, dogo wangu alikua huko km miaka 15-20 hivi sasa,
Alidungwa visu mara 4.
Na shida alipata mshangazi wamezaa huko.
Dah kila siku ikawa kilio tu analia,
Ukimtoa leo kesho kakabwa tena.
Ikabidi maamuzi magumu arudi tu maskani no way atakufa.
Yah,yupo mpk sasa ana mishe zake katulia tu.
 
Maisha mazuri hayapatikani sauzi.
Hata huko kumebadilika njaa kali.utafanya kazi gani ya kukupa pesa nyingi wakati haujasoma?
 
Kwahiyo kupeleka watoto shule ndo kumaanisha kwamba hawatozamia SA au ughaibuni.!
Inapunguza ukubwa wa tatizo. Wachache watakaozamia wanaweza pata kazi kupitia elimu na kuepuka maisha ya kudhalilika kabisa mitaani. Hawa wasiojua hata kuandika vizuri kiswahili huishia kuwa wahalifu au kufanya kazi ngumu zisizokidhi hata mahitaji muhimu ya binadamu.
 
Inasikitisha sana kwa kinachoendelea dhidi ya vijana wanaozamia South Africa kutafuta maisha huku wakiwa hawana elimu wala ujuzi wowote. Wengi wao ni kutoka wilaya ya Temeke hasa kata ya Mbagala. Ambapo pia wengi wao ni watu wa mikoa ya kusini kwa maana ya Lindi na Mtwara. Maisha wanayoishi huko SA yanasikitisha sana.

Mimi siandiki kiushabiki wala kwa kusikia stori za vijiweni. Mwaka 2016 mtaani kwetu kulikuwa na dogo kibaka msumbufu sana. Kilichokuwa kimebakia ilikuwa ni watu kumuua tu. Nikamwonea huruma na kukaa nae chini na kumuuliza ni kitu gani anaweza fanya ili aachane na uhalifu. Akajibu anataka awe la Library ya muziki. Nikampa laki 3 aanzishe biashara. Baada ya kumpa ghafla dogo akapotea. Ilipopita miezi kadhaa nikapokea ujumbe Facebook toka kwa dogo kumbe laki 3 alitumia kama nauli kutimkia South Africa.

Kupitia posts zake za FB niligundua dogo yuko na urafiki na watu wanye viashiria vyote vya uhalifu. Tokea wakati huo ndo nikaanza kujua mambo mbalimbali kuhusu watu wanaozamia South. Vijana wengi kule wanaishi maisha mabovu mno ya kudhalilika. Ukiwa kwenye magroup ya FB kila mara huwa wanapost matatizo tu. Watu kuchanganyikiwa, kukosa pa kuishi, kukamatwa na polisi na mara kadhaa vifo.

Wenyewe wanajiita mabaharia na hujiona wapambanaji kwelikweli huku kiuhalisia wanapoteza muda. Mbagala wanaiita BACK CITY.

Sipendi ukabila wala ukanda ila katika hili watu wa Dar hasa Temeke, Pwani, Lindi na Mtwara hamuwezi kwepa lawama. Kwenye wanaodhalilika South Africa sijawahi ona jina la watu wa mikoa kama Njombe, Mbeya au Kilimanjaro.

Kupitia hii post niwapongeze wakinga na wanyakyusa kwa kupenyeza biashara zao Zambia na Malawi. Nimeona wazambia wakiwatupia lawama wanyakyusa na wakinga kwa kuwavuruga kibiashara.
Ahsante tumepokea pongezi, kweli huko kwa madiba wanadhalilika sana!
 
Back
Top Bottom