Watu wa maji na beacon zao na mabango ya ilani kuwekwa kwenye makazi

Watu wa maji na beacon zao na mabango ya ilani kuwekwa kwenye makazi

Alkelokas

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2012
Posts
203
Reaction score
103
Hivi karibuni katika mtaa ninaoishi ambapo pia nimejenga nyumba ninayoishi,kumejitokeza watu wanaojiita Bodi ya maji ya Bonde la Ziwa Nyasa wakidai kuwa hili ni eneo la chanzo cha maji hivyo hapapaswi kufanya shughuli zozote za kibinadamu.

Kilichonishangaza ni kuwa watu walipokuwa wanajenga hawakusema chochote lakini sasa wameleta hizo beacon na mabango yakiwasihi watu wasiendeleze maeneo hayo yaliyo ndani ya beacon hizo.

Wanaofahamu sheria kuhusu umbali toka chanzo cha maji au kingo za maji naombeni mnijuze maana hizo beacon sijaelewa walitumia utaratibu upi kuweka mana hawakutumia umbali wa mita kwa maana beacon moja na nyingne haziko usawa mmoja.

Kingine naombeni uzooefu kwa watu waliokwisha wekewa hizi beacon katika maeneo yao mstakabali wao uliishiaje kwa maana walibomolewa au kukatazwa kulima au la?

Wakati huo tuna kikao kesho kwa watu waliowekewa beacon tujue pakuanzia kwa maana Mkuu wa wilaya na Mbunge wetu alipopigiwa simu alidai hana taarifa na zoezi linaloendelea.
 
Ndani ya mita 60 kutoka kwenye chanzo cha maji hatutakiwi kufanya shughuli za kibinadamu, bila shaka ni Sheria ya mambo ya ardhi, mazingira something else

Lakini beach zinauzwa na serikali inapokea kodi inaruhusu watu binafsi kujenga maeneo hayo.

Nadhani tukomae kutafuta ela maana bila ela tuna nyanyasika sana
 
Walivyoulizwa mbona hamfati mita 60 wanakwambia eti walitumia Gps siyo mfumo wa mita.
 
Back
Top Bottom