Watu wa mamlaka ya sanaa pigeni marufuku Bongo Star Search

Watu wa mamlaka ya sanaa pigeni marufuku Bongo Star Search

Shindano la hovyo hadi linatis kinyaa..mtu anaimba poa tu sekunde 3 hazijaisha anakatishwa kwa kejeli na kashfa.

Unashangaa hawa watu wana utaalam gani wa kugundua vipaji vya muziki?
hao washindi wao mpaka leo wanakionyesha mafanikio gani kwenye muziki?

Sisemi kifungiwe maana hili ni soko huria, ila siwezi kumshauri mtu kushiriki shindano la kijinga vile
 
Sasa mtu badala aimbe analia milio ya ajabu kana mbuzi unataka wafanyaje sasa. Acha majaji wafanye kazi yao.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Kama unataka kudhalilishwa na kuharibia siku nenda kashiriki hayo mashindano
 
Bss Kwanzia majaji Hadi washiriki wote ni wasaka fursa tu Rita ni mpigaji amewazulumu balaa na waimbaji wenyewe wanachofata pale ni pesa tu wala hakujawai kuwa na msanii wa maana ndo maana kila anaeenda lazima aimbe..
Malaiikaaaa nakupenda malaaaikaaa[emoji445]
Malaaaikaaa nakupenda malaaiikaa[emoji445]
Nami nifanyejeee kijana mwenziooo[emoji445][emoji445]

Bss haijawahi kutoa mshindi ambae amedumu sana kweny game kwa kiwango kikubwa wengi wakishinda wakikwara pesa wanapotea wale ni wasaka fursa tu inawezekana hata washindi huwa wanapangwa tu wanashinda watu wasio stahili
 
Habari zenu wakuu,

Nimeamua Leo kuleta mada hii haswa mamlaka pigeni marufuku shindano la BSS kwa sababu hakuna anaestahili kuwa jaji pale na ndio maana pamoja na serikali yetu haina mpngo mbdala wa kuzalisha wasanii ila ndani ya nchi yetu kila mwenye pesa anaenda studio.

Hebu tuangalie nchi za wenzetu jinsi wanavyotafuta waimbaji hakuna jaji hata mmoja anaemwambia mshiriki una sauti mbaya ila hapa kwetu jaji anatamka wazi anakwambia huwezi kuimba sasa ukiangalia huyo jaji wenyewe hata chombo kimoja cha muziki hawezi piga

Tujaribu kuangalie wahindi wanapotafuta waimbaji wale majaji ni watu walioshiba.

Ni wasanii wakubwa hata ukiangalia nyimbo zao youtube utapata ushahidi kwa mfano jaji awe Himesh Reshmiya

Au Sonu Nigam
Au Udit Narayan
Au Kumar Sanu

Hapo ikitokea MTU ameshinda hawezi potea sasa hawa majaji wetu sasa Sijui wametokea kwenye kitengo gani kuhusu Sanaa au uimbji au kwakuwa maarufu hapa kwetu
Mkuu umeambiwa ukalime nini huku wewe ulishajiwekea mziki ndio utakaokutoa
 
Tatizo lililopo;
Anaejua hawezi kufanya,
Anaefanya hajui, basi shida tu.

La msingi ni kushauri watumie Lugha ya kistaarabu kusema wafutwe si sahihi.
Hivi na wao wanatumia lugha ya kistaarabu?
 
Back
Top Bottom