Watu wa MicroFinance wanaopiga simu kutafuta wateja, wanatoa wapi namba?

Mowwo

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2015
Posts
1,083
Reaction score
1,628
Bila shaka mko vyema,

Nimezoea kuona matangazo ya Microfinance mbalimbali online lakini sijawahi kuwa na app yoyote ya hayo mambo.

Cha kushangaza leo nimepigiwa simu na namba(partially nitaattach screenshot) akajitambulisha anatokea kwenye Microfinance(akataja jina) na kunijulisha wanakopesha mpaka bei gani.
Nimemjibu simple tu, sitaki mikopo.

Baada ya kukata simu nimesearch jina la hiyo microfinance lipo. Najiuliza, wametoa wapi namba?

Kwanini wapige direct kwangu?

Tuwe makini wakuu

 
Mitandaoni faragha zetu sio binafsi kwa asilimia 100
Kuna kubahatisha number
Kuna kuchukua mitandaoni Mfano FB, group za WhatsApp nk
 
Kuna huyu muhindi na kiingereza chake cha kihindi kanitaja kwa majina matatu na video call juu

Mpaka sasa sijaelewa bado detail zangu kazipataje bahati yake nilikua naendesha muda alio piga
 
Umechelewa kupigiwa na wanakopesha popote ulipo bila hata ya wewe kuwafata kwa mikopo midogo 500k kushuka chini na wanataja hadi location yako sio kwa kuku trace bali kupitia watu waliokusajili
Mkopo wa laki 5 bila dhamana si wanapigwa sana za uso. Mimi sikumskiliza kabisa, nimeachana nae mapema sana
 
Umewahi kuwauliza waliokupa namba ya simu unayotumia kuna vigezo na masharti gani ya kuitimia? Hiyo biashara kubwa ndugu yangu 🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…