Watu wakitembelea UDSM wanashangaa jinsi mazingira yake yalivyo green, tree lined roads, lawns na gardens
Halafu wengi wanafikiri chuo cha UDSM kilijengwa na wakoloni ndio maana kipo hivyo, kumbe kilijengwa baada ya uhuru
Hii ina maana sisi Waafrika tuna uwezo wa kujenga na kuendeleza maeneo yenye mazingira mazuri.
Ila Kinachosikitisha, tumeshindwa kama jamii kujenga vitongoji vyetu kwa uzuri unaofanana na mazingira ya UDSM.
Hebu fikiria kama Goba, Madale, Kimara na maeneo mengine mengi ya Dar, yangekuwa na mandhari kama ya chuo cha UDSM, Dar ingeonekana ni mji mzuri kiasi gani
Yani wataalam wetu wa miji hawahitaji kwenda Ulaya kujifunza jinsi ya kujenga miji na makazi mazuri; UDSM peke yake inatosha kuwafundisha jinsi ya kufanya kazi yao
View attachment 3611314