Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 21,470
- 40,593
Kama timu za Tanzania zitaendelea kuchukua makocha na wachezaji toka nchi zinazozungumza kifaransa, basi kuijua lugha ya kifaransa ni muhimu na lazima.
Wachezaji wetu wa ndani,wachambuzi wa Mpira, waandishi wa habari na makocha wetu, lazima wajue pamoja na kuujua Mpira, lakini mafanikio ya kweli huletwa na mawasilioano ya lugha.
Kama kocha lugha unayoijua ni Kiswahili tu na kiingereza Cha kubabia, timu unayofundisha Ina wachezaji watano wanaozungumza kifaransa pekee, hali itakuwaje?
Mchezaji kama umepata Dili la kwenda kucheza nchi inayotumia kifaransa kama lugha ya mawasiliano, ukifika huko utaingiaje kwenye mfumo haraka?
Hawa wachambuzi wetu wa Mpira (wengine ni uchwara tu) Kuna wakati hukosa taarifa za wachezaji wanaokuja kucheza huku kwa kuwa taarifa za wachezaji hao zimeandikwa kwa kifaransa.
Angalia waandishi wetu wanavyobabaika kuwahoji wachezaji wanaojua kifaransa pekee. Yaani ni vururuvururu😃😄😀
Hata mazoezini unaona kabisa wachezaji wa bongo stori wanapiga wenyewe Kwa wenyewe.
Kipaji sawa, lakini na lugha iwemo.