Mchokozi wa mambo
JF-Expert Member
- Mar 27, 2014
- 201
- 159
Ndugu zangu watu wa Stationery hali yao ni mbaya sana. Kwani bidhaa muhimu katika Stationery hasa karatasi nyeupe zimepanda sana na haijawahi kutokea.
Kabla ya kauli ya Rais kuwa bidhaa nyingi zitazidi kupanda bei ya Katoni ilikuwa inauzwa Tsh 43000 ghafla baada ya ile kauli kutoka katoni ya ream sasa ni Tsh75000.
Fikiria kabla ya kupanda bei Ream pc1 kwa bei ya rejareja ilikuwa ni Tsh 9000 au 8000 lkn inauzwa kwa Tsh 17000 na 18000.
Kwa utafiti mdogo nilioufanya nimegundua kuwa Ream nyingi zinazotumika nchini kwetu zinaagizwa kutoka Afrika ya Kusini. India, China na Indonesia. Sasa hizi bei zitapanda mpaka wapi.
Waagizaji na wasambazaji wakubwa wanakula njama na ushirikiano acha kabisa. bei tunaziona wanazipanga wao kwa makubaliano kuwa na bei moja ili kila mtu apate faida kubwa hasa kwa kuzingatia kauli ya Mheshimiwa Rais ilikuwa amewapa nguvu.
Hii ya kusema kila kitu kinapanda bei sababu ya vita vya Urusi na Ukraine ni kichaka cha kujifichia ili kutesa raia. Wakuu wa Wilaya na mikoa tokeni pamoja wa wahusika mjionee hali halisi. Huu ni uhuni mkubwa kwa nchi yetu
.