"Watu waachwe Huru kuujadili Muungano"- VP, Samia Suluhu Hassan. Huyu mama anaongea vizuri kwa Unyenyekevu mpaka raha. Huchoki kumsikiliza

Ni wapuuzi wachache tu watakao puuzia thamani yako humu JF.
Pasco ni zaidi ya tunavyomfikiria.

Pia wanaompuuzaga ni wajinga wachache wa pale bavicha wanaotakaga mtu akitoa maoni yawe yale yanayowaoendeza tu e.g mtu akisema ccm itaanguka mwakani hapo utaona yanashangilia bila hata ku reason.
 
Nami nijiunge na Watanzania wenzangu kumtakia Happy Birthday President Mama Samia Suluhu Hassan.
P
 
Hizo ni tabia za KICHACHAWA na tabia za nyinyi CHAWA ni kuwahadaa maboss wenu kuwa mnawapenda kwa kuwaandalia sherehe kama hizi!!!
Mkuu Bulesi, nimesema wazi kabisa kuwa sherehe za birthday ni sherehe za kizungu sisi watu wa bushi tulikuwa hatuzifanyi, lakini sasa kutokana na maendeleo nasi sasa tunazifanya. Kumfanyia bosi, wife, wazazi, watoto a surprise party, ni ishara ya upendo na sio uchawa, ila pia naomba kukiri, the dividing line between upendo wa dhati na uchawa is very thin, kama ilivyo mwanaume kumtokea demu bomba mwenye sura nzuri na bonge la shape na kumwambia "I love You," kuwa unampenda na umemzimikia kwake umekufa umeoza, the dividing line between hiyo I love you yako yako kama ni love kweli na umempenda kwa dhati au ni lust tuu unamtamani umduu tuu, is very thin, with naked eyes you just can't tell, ila sisi wa jicho la tatu can!. Najitolea mfano mimi mwenyewe, ikitokea nikamsifia Samia kwa lolote very genuine, halafu ukaniita chawa utakuwa ni unanionea kwasababu kumsifu sikuanza leo!.
Angalia tarehe za mabandiko haya...
Hivyo kwa mtu kama mimi kumtakia Rais Samia Happy Birthday, ni bonafide Happy Birthday na sio uchawa!.
Happy Birthday Rais Mama Samia!.
Paskali.
 
Nawatakia Wanawake Wote, maadhimisho mema ya Siku ya Wanawake Duniani.
P
 
Wanabodi,
Leo sikukuu ya Muungano, nafanya mapitio ya baadhi ya mabandiko ya muungano.

Japo waasisi wa muungano wetu huu adhimu ni Nyerere na Karume, muungano ni kama ndoa, kuna mtu ana proposes, mwingine anakubali, ndoa inafungwa. Kwenye muungano wetu huu adhimu, aliye proposes ni Nyerere, Karume akakubali. Nia ya Nyerere ni kwenda kwenye serikali moja. Wito kwa viongozi wetu, kama nia ya kweli ni kudumisha muungano, twende kwenye serikali moja. Tumuenzi Mwalimu Nyerere kwa kuyaishi maono yake!. Nawatakia Muungano Mwema.

Paskali
 
Zile sababu alizoziona Nyerere akapendekeza muundo wa serikali mbili bado zipo. Itakuwa vyema tukaenda na serikali tatu. Mambo yanabadilika kwa kasi. Hivi sasa hatuna tena watu wa calibre ya Nyerere. Twende na TATU
 
Mkuu Suzy Elias, ungekuwa umetutendea haki kama ungesema hilo tishio la usalama wa JMT ni tushio gani endapo Zanzibar itepewa hadhi sawa na haki sawa ndani ya JMT kama ilivyo Tanzania Bara, mfano muungano wa federation au muungano wa mkataba?.

Kuna wengi wamemjua Samia baada ya kuwa Rais wa JMT, ndio mnaweza kuwa na mashaka na Samia kwenye kuulinda huu muungano wetu adhimu. Angalia bandiko hili ni la lini na Rais Samia alisema nini kuhusu muungano
Karibu pande hii
P
 
Nadhani Zanzibar ilikuwa na watu wenye akili Sana, ingawa hujiweka kama wajinga (vile mnasema wanacheka nawe huku moyoni wana Lao) hata ukiangalia ni wazi kuwa mahari ya ndoa hii ya Muungano, anayeilipa ni Tanganyika, mashart mengi anapewa yeye Tanganyika, like if you want you must do and don't.


In other ways angalia kifikra za kiutu uzima wa wazee wa Chama cha TANU wa wakati ule, sio kihistoria iliyoandikwa, utagundua Nyerere alipewa zawadi ya kuwa mwenyekiti wa TANU, ili akabidhiwe kirahisi Uhuru wa Tanganyika and then eventually awakabidhi Watu wa Pwani, (ndugu wa Kizanzibari, Oman and Seychelles).

Katika Kujua haya usicheze kama kuonyesha Unajua, Chezesha ujue na wengine wajue how they are!

Sio kuwa tu mjuaji!
Make sure you know your Purpose and the Impacts!
Sio kujipendekeza![emoji109][emoji109]~[emoji1666][emoji1666]
 
Jitu Zima takataka
 
Kama alichokisema Mama Samia watu wawe huru kuujadili muungano na kutema nyongo, nyongo inapotemwa na kiongozi wa serikali iliyopo madarakani, inageuka sumu!.
Wanabodi,

Politics is a game like any other games, that people plays, it has its rules and regulations, ukikiuka unaweka pembeni. Yaani mchezo wa siasa pia ni mchezo kama mchezo mwingine wowote, una sheria zake, taratibu na kanuni, ukikiuka, unapewa kadi nyekundu unawekwa pembeni.

Serikali ya Zanzibar, ni serikali ya mseto, inaendeshwa na vyama viwili, CCM na ACT, ila watu wa ACT ndani ya GNU wanapaswa kutekeleza sera za CCM.

Serikali ya GNU japo ni serikali ya mseto, lakini inaongozwa na Ilani ya uchaguzi ya CCM, hivyo ACT ndani ya GNU ama wanatakiwa kuhubiri ilani ya uchaguzi ya CCM, na sera za CCM ama wanyamaze kimya, halafu wale ACT wengine nje ya GNU ndio wanaweza kuendelea kupiga siasa za ilani ya ACT!.

Ndani ya Serikali, kuna kitu kinaitwa a collective responsibilities, ukiishakuwa ndani ya serikali, huwezi kusema jambo lolote ambalo ni kinyume cha sera na ilani inayotawala ukabaki salama.

Maalim Seif alipokuwa ndani ya GNU, alinyamaza, hivyo Masoud Othman Masoud ama naye anyamaze, ama atoke nje ndio akaendelee kuhubiri kuuvunja huu muungano wetu adhimu!

Mtu aliyemo ndani ya serikali, hawezi kuyasema maneno kama haya
Othman Masoud anamuona Hussein Mwinyi kama mateka asiyeweza kuitetea Zanzibar, hadhi, maslahi, na haki zake.
Msikilize Othman Masoud hapa chini.
Kwa maoni yangu, huyu mtu anatakiwa awekwe pembeni, apate muda wa kutosha ajishughulishe na siasa, kwasababu ACT ndani ya GNU wanatakiwa kutekeleza Ilani na sera za CCM!

Ushauri kama huu kumhusu mtu huyu huyu niliwahi kuutoa kule nyuma na ukatekelezwa, Dr. Shein Mfute Kazi Haraka, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Kabla Hajamwaga Sumu Hii

Hili la kila uchao mtu huyu kuuchokoa muungano hakuanza leo, na hakuna ubaya wowote kuuzungumzia muungano kwa jambo lolote alimradi hilo linalozungumzwa ni liwe la ukweli kuna siku aliongopa kuhusu sovereignity Kuhusu Muungano, Makamo wa Kwanza wa Zanzibar, Adai ni Zanzibar Pekee iliyopoteza Sovereignty, Je Yuko Sahihi?

Hata Mama Samia akiwa VP aliwahi kushauri watu waachwe wa vent kuhusu muungano,

P
 

Huyu Jamaa ana uchu wa Madaraka
Nimehudumu kwenye media kwa miaka 30, niliwahi gombea nafasi yoyote ya uongozi hadi useme nina uchu?
kajipendekeza kwa Magufuli mpaka Kafa
Kwenye kipindi cha JPM, niliwahi gombea chochote?.
Kaanza kwa Mama bado hali ni tete
Wengi wenu mmemfahamu Mama Samia, baada ya kuwa Rais wa JMT, angalia tarehe ya bandiko hili ni la lini na nilizungumza nini kumhusu Samia!, Jee nilikuwa najipendekeza kwa Samia tangu 2020?
P
 
Mkuu..
mimi naona unamtamani Mama yetu...
Sio kwa sifa hizi...Secret admirer....
Duh...!, Mkuu Teknocrat, hapo nimesifu kidogo tuu, unasema eti nimetamani!, mbona hivi ni vitu vya kawaida sana kwa binadamu!. Mimi ni binadamu tuu, I'm a human being like all other human beings, and she is a human being too!, hakuna ubaya wowote kwa mtu yoyote, kuwa a secret admirer wa mtu yoyote, ila mimi sio a secret admirer, mimi ni open admirer!. Kama bandiko hilo wewe unaona ndio nimesifia sana mtu, jee ungeona bandiko hili, Siku ya Wanawake Duniani: VP Samia Suluhu: "Womanly, Genuine, Humble, Simple na Down To Earth!” ungesema nini?, au jee ungemjua mtu aliyesifiwa hapa ni nani, ungesemaje? Ikitokea kuna Kiongozi ana Macho mazuri, na umeyapenda, je, kuna ubaya kumsifia macho yake? Ni ukosefu wa heshima na adabu?

Tena msidhani nimeanza kum observe leo, angalia tarehe ya bandiko hili New Cabinet: Baadhi ya Majina ni Haya Hapa!. na uangalie nilisema nini juu ya mtu huyu?.

Kisha angalia hapa uone hii ni ya lini, Wajue The Top Five Most Prominent Members wa Bunge Maalum la Katiba!.

Twende hapa angalia hii ni ya lini, na anayezungumzwa ni nani, Siku ya Wanawake Duniani: Je, tuna Wanawake wenye sifa za Presidential Material?

Kama wewe una uwezo, to read in between the lines, angalia bandiko hili, nilisema nini kumhusu mtu huyu na nilimshauri nini Blaza kuhusu 2020!.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…