"Watu waachwe Huru kuujadili Muungano"- VP, Samia Suluhu Hassan. Huyu mama anaongea vizuri kwa Unyenyekevu mpaka raha. Huchoki kumsikiliza

Wanabodi,
Niko kwenye voluntariy lockdown, hivyo leo nimapata fursa ya kuangalia TV ya Zanzibar, ZBC, Mwandishi wa habari wa CCM Zanzibar, Daudi Ismail anamhoji Makamo wa Rais wa JMT, Mhe. Samia Suluhu Hassan anauzungumzia Muungano, kiukweli huyu Mama Samia anauzumguza vizuri muungano huku akiongea kwa heshima, taratibu, kwa utulivu na unyenyekevu, na anaongea vizuri mpaka raha, na kwa wale wenzangu na mimi wenye udhaifu na macho fulani, kiukweli Mwenyenzi Mungu amemjaalia macho mashaalah, huchoki kumsikiliza, utatamani aendelee tuu kuongea na kipindi kisiishe!.

Kwa hoja za muungano Mama Samia alizoshusha, ningekuwa ni uwezo wangu, ningeshauri October 2020, Mama Samia ndiye ampokee Dr. Shein kule Zanzibar, ili 2025, aje ampokee Magufuli, maana kwa maoni yangu, kwa uongeaji huu, huyu mama ndiye Mzanzibari pekee anayekubalika kuweza kuchagulika kuwa rais wa JMT kutokea Zanzibar, vinginevyo Wazanzibari wausahau kabisa urais wa Muungano, wao mwisho wao ni umakamo wa rais pekee.

Anasema Zanzibar inafaidika sana na muungano, kisiasa, kiuchumi na kijamii, ikiwemo kufaidika kielimu, wakati wa muungano, Zanzibar haikuwa na chuo kikuu chake hivyo Wanzanzibari wote wa enzi hizo waliofika elimu ya vyuo vikuu, wamesomea bara.

Mama Samia amesema watu waachiwe kuujadili muungano kadri watakavyo na hata kutema nyongo kuhusu muungano, na serikali inazitumia hizo hoja zinazolalamikiwa kuimarisha muungano, akasema ni heri watu wafunguke na kusema hivyo kuyatoa madukuduku yao, kuliko kunyamaza na madukuduka ndani yao, siku wakilipuka moto utawaka, hivyo watu waachwe waseme.

Amesema Zanzibar ni visiwa hivyo viko wazi pande zote, hivyo faida kubwa kabisa ya muungano ni ulinzi usalamax amani na na utulivu wa Zanzibar, bila muungano, ilikuwa ni rahisi sana kuivamia Zanzibar na Zanzibar ikivamiwa ni rahisi sana kuivamia bara, hivyo muungano umeimarisha sana ulinzi na usalama, amani na utulivu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kuna kitu Mama Samia amekisema sikuwahi kukijua!. Kumbe Wizara ya Mambo ya Nje ilipokiwa ikiitwa Wizara ya Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa ndio ilikuwa ya Muungano iki handle issues zote za Zanzibar kimataifa, lakini , ilipobadilishwa jina na kuitwa Wizara ya Mambo, ya Nje na Ushirikiano wa Africa Mashariki, sasa ina handle mambo ya Zanzibar ndani ya Africa Mashariki tuu, lakini kimataifa, kwa yale mambo ambayo sio ya muungano, SMZ ya Zanzibar imepewa uhuru wa kunegotiate ufadhili, misaada, na mikopo na mikataba ya kimataifa kwaniaba ya Zanzibar, ila kwenye kutiliana saini, anayetia saini ni serikali ya JMT, kwasababu Zanzibar haina sovereignty, sovereignty ni moja tuu ambayo iko kwenye JMT pekee!.

Hili sikuwahi kulijua, hivyo kumbe sasa Zanzibar inaweza kupata misaada na mikopo ya kimataifa, sasa kwavile uwiano wa kugawana misaada ya kutoka nchi wafadhili na wahisani, Zanzibar inastahili kupata asilimia 4.5% ya misaada yote kwa Tanzania, sasa kwa vile Zanzibar nayo inaweza kuomba ufadhili wa kimataifa, jee hii misaada ya kimataifa ya Zanzibar inayoomba, Tanzania bara pia tunapewa ule mgao wa asilimia 95.5% ya misaada ya Zanzibar, au misaada ya Tanzania tuu, ndio Zanzibar inapaswa kugaiwa asilimia 4.5%, lakini kwa misaada ya Zanzibar, then misaada hiyo ni ya Zanzibar pekee?.

Mama Samia amezungumzia kero za muungano na kusema kero nyingi zimeisha tatuliwa ila utekelezaji ndio unasua sua, na kutolea mfano deni lililokuwa la umeme la Tanesco, deni hilo lilisababishwa na double taxation, kwa Tanesco kuwachaji SMZ VAT huku shirika la umeme la Zanzibar, Zesco nalo likiwachaji kodi ya ongezeko la thamani Vat, wateja watumiaji wa umeme zao nao wakilipishwa Vat, kero hiyo imetatuliwa kwa Tenesco hawaichaji tena Vat kwa SMZ, hivyo Zanzibar haidaiwi tena deni lolote la umeme na Tanesco.

Ninachokumbuka kwenye deni la umeme la Zanzibar, lilitokana na Tenesco kuuza umeme kwa bei ya juu kwa Zesco, halafu Zesco wanauza umeme huo kwa bei ya chini Zanzibar, kumbe ilikuwa ni issue ya VAT!.

Pia amezungumzia kero za muungano kadri zinavyotatuliwa, kero nyingine zinaibuka, hivyo issue za kero za muungano ni issue endelevu.

Kuhusu usawa wa kijinsia kwenye uongozi, amesema Mungu aliumba jinsia tofauti kwa maana yake, hivyo ni vizuri wanawake wakajikubali kwa uanawake wao na kutimiza majukumu ya wanawake kama dini na Mungu alivyodhamiria, na wanaume nao watimize majukumu yao, nafasi za kazi au uongozi zisifanye wanawake kujisahau majukumu yao ya kutunza familia, na kuipongeza Tanzania, wanawake na wanaume ni sawa, akatolea mfano kuna nchi wanawake na wanaume wanafanya kazi ile ile lakini wanawake wanalipwa pungufu ya wanaume, na kuna nchi, wanawake ndio wazalishaji mali lakini hawaruhusiwi kupokea mshahara, siku ya mshahara, waume zao ndio wanakuja kuwapokelea. Tanzania mishahara inafanana na wanawake wanaruhusiwa kuingiza kipato.

Alipoulizwa kuhusu malalamiko ya watalii licha ya kuingia Tanzania na passport zao kugongwa entry, lakini wakifika Zanzibar, wanakaguliwa tena na kujaza fomu upya, Mama Samia alisema hizo ni hatua za kawaida za kiusalama, hata yeye kufuatia kuwa na jina la Hassan na kuna nchi alifika na ujumbe wa Tanzania, wengine wote waliruhusiwa yeye akazuiliwa kwa saa kadhaa hadi walioojiridhisha ndipo akaruhusiwa.

Amezungumza mengi na kumalizia kwa kusisitiza Muungano ni jambo jema, tuulinde na kuuenzi.

Kwa hoja kama hizi za huyu mama Samia, kama age sio issue sana, si huyu mama atatufaa sana 2025 au tuwashauri kwa vile Magufuli analamika sana kuhusu urais, mara ni mateso, mara ni kazi ngumu, mara ni mzigo mzito, tumshauri rais Magufuli, kwa vile Samia anatosha sana, hivyo tumpunguzie mateso, hana haja ya kuendelea na mateso, mzigo mzito na kazi ngumu ya urais, na hata kama ni wale tausi au wanyama wa Magogoni, au yale majabali ya Chamwino, tutamjengea Chato na kumuomba bora apumzike tuu mapema, na kumpisha Mama Samia ndio amalizie ngwe yake iliyobakia?.

Paskali
Rejea
Siku ya Wanawake Duniani: VP Samia Suluhu: "Womanly, Genuine, Humble, Simple na Down To Earth! - JamiiForums

Siku ya Wanawake Duniani: Je, Tuna Wanawake Wenye Sifa za Presidential Material?! - JamiiForums

Wajue The Top Five Most Prominent Members wa Bunge Maalum la Katiba!. - JamiiForums

New Cabinet: Baadhi ya Majina ni Haya Hapa!. - JamiiForums

Makamu wa Rais, Samia Suluhu aweza kuendana na kauli za Rais Magufuli - JamiiForums
Tuchague viongozi wenye sauti nzuri ili nchi iendelee kiichumi, ninampendekeza mke wangu mzaliwa wa Nzega akiongea uthadhani anaimba.
 
Mkuu elvischirwa, nimezungumzia kuongea vizuri, na sio sauti nzuri. Viongozi wetu wanapaswa kuongea vizuri, kauli huumba!. Viongozi waongee vizuri, watoe kauli njema, ili kuwaumbia mema watu wa nchi yetu.

P
 
Ukiwa na sauti nzuri lazima utaongea vizuri.
Not necesarily, wako wadada warembo, wana sauti nzuri, laini, nyororo, ambao walipaswa kuwa na sauti tamu kama asali, but its the oposite, wana sauti chungu kama shubiri, wanatema nyongo yenye sumu kali mwanzo mwisho!.
Na wako watu wana sauti mbaya, ya ukali, wanatema madini hatari!.
P
 
Mayala hujachoka kusaka uteuzi? Tatizo huna connection
Mkuu Last emperor, uteuzi unasakwa kwa VP?.
Mkuu..
mimi naona unamtamani Mama yetu...
Sio kwa sifa hizi...Secret admirer....
Duh...!, Mkuu Teknocrat, hapo nimesifu kidogo tuu, unasema eti nimetamani!, mbona hivi ni vitu vya kawaida sana kwa00 binadamu!. Mimi ni binadamu tuu, I'm a human being like all other human beings, and she is a human being too!, hakuna ubaya wowote kwa mtu yoyote, kuwa a secret admirer wa mtu yoyote, ila mimi sio a secret admirer, mimi ni open admirer!. Kama bandiko hilo wewe unaona ndio nimesifia sana mtu, jee ungeona bandiko hili, Siku ya Wanawake Duniani: VP Samia Suluhu: "Womanly, Genuine, Humble, Simple na Down To Earth!” ungesema nini?, au jee ungemjua mtu aliyesifiwa hapa ni nani, ungesemaje? Ikitokea kuna Kiongozi ana Macho mazuri, na umeyapenda, je, kuna ubaya kumsifia macho yake? Ni ukosefu wa heshima na adabu?

Tena msidhani nimeanza kum observe leo, angalia tarehe ya bandiko hili New Cabinet: Baadhi ya Majina ni Haya Hapa!. na uangalie nilisema nini juu ya mtu huyu?.

Kisha angalia hapa uone hii ni ya lini, Wajue The Top Five Most Prominent Members wa Bunge Maalum la Katiba!.

Twende hapa angalia hii ni ya lini, na anayezungumzwa ni nani, Siku ya Wanawake Duniani: Je, tuna Wanawake wenye sifa za Presidential Material?

Kama wewe una uwezo, to read in between the lines, angalia bandiko hili, nilisema nini kumhusu mtu huyu na nilimshauri nini Blaza kuhusu 2020!.
P
 
Wanabodi,
Makamo wa Rais wa JMT, Mhe. Samia Suluhu Hassan anauzungumzia Muungano, kiukweli huyu Mama Samia anauzumguza vizuri muungano huku akiongea kwa heshima, taratibu, kwa utulivu na unyenyekevu, na anaongea vizuri mpaka raha, na kwa wale wenzangu na mimi wenye udhaifu na macho fulani, kiukweli Mwenyenzi Mungu amemjaalia macho mashaalah!, huchoki kumsikiliza, utatamani aendelee tuu kuongea na kipindi kisiishe!.

Kwa hoja za muungano Mama Samia alizoshusha, ningekuwa ni uwezo wangu, ningeshauri October 2020, Mama Samia ndiye ampokee Dr. Shein kule Zanzibar, ili 2025, aje ampokee Magufuli, maana kwa maoni yangu, kwa uongeaji huu, huyu mama ndiye Mzanzibari pekee anayekubalika kuweza kuchagulika kuwa rais wa JMT kutokea Zanzibar, vinginevyo Wazanzibari wausahau kabisa urais wa Muungano, wao mwisho wao ni umakamo wa rais pekee.

Kwa hoja kama hizi za huyu mama Samia, kama age sio issue sana, si huyu mama atatufaa sana 2025 au tuwashauri kwa vile Magufuli analamika sana kuhusu urais, mara ni mateso, mara ni kazi ngumu, mara ni mzigo mzito, tumshauri rais Magufuli, kwa vile Samia anatosha sana, hivyo tumpunguzie mateso, hana haja ya kuendelea na mateso, mzigo mzito na kazi ngumu ya urais, na hata kama ni wale tausi au wanyama wa Magogoni, au yale majabali ya Chamwino, tutamjengea Chato na kumuomba bora apumzike tuu mapema, na kumpisha Mama Samia ndio amalizie ngwe yake iliyobakia?. Hili mnalionaje?.

Paskali
Kwa vile leo ni birthday ya Rais Samia, nawaomba wana jf well wishers, tuungane kumu wish a Happy Birthday this lovely lady Rais wetu mpendwa, Rais wetu mpenzi, Rais wetu kipenzi, Rais Dr. Samia Suluhu Hassan, Chifu wa kabila kubwa kuliko makabila yote Tanzania, ambayo Kanda ya kabila hilo ndio Kanda determinant ya kura za urais wa JMT, Chifu Hangaya.
IMG-20230127-WA0000.jpg

Happy Birthday.
P
 
ningekuwa ni uwezo wangu, ningeshauri October 2020, Mama Samia ndiye ampokee Dr. Shein kule Zanzibar, ili 2025, aje ampokee Magufuli, maana kwa maoni yangu, kwa uongeaji huu, huyu mama ndiye Mzanzibari pekee anayekubalika kuweza kuchagulika kuwa rais wa JMT kutokea Zanzibar, vinginevyo Wazanzibari wausahau kabisa urais wa Muungano, wao mwisho wao ni umakamo wa rais pekee.

Kwa hoja kama hizi za huyu mama Samia, kama age sio issue sana, si huyu mama atatufaa sana 2025 au tuwashauri kwa vile Magufuli analamika sana kuhusu urais, mara ni mateso, mara ni kazi ngumu, mara ni mzigo mzito, tumshauri rais Magufuli, kwa vile Samia anatosha sana, hivyo tumpunguzie mateso, hana haja ya kuendelea na mateso, mzigo mzito na kazi ngumu ya urais, na hata kama ni wale tausi au wanyama wa Magogoni, au yale majabali ya Chamwino, tutamjengea Chato na kumuomba bora apumzike tuu mapema, na kumpisha Mama Samia ndio amalizie ngwe yake iliyobakia?. Hili mnalionaje?.
Hili ni bandiko la 2020, angalia ushauri uliotolewa hapo.
Tuwatakie maandalizi mema ya siku ya wanawake duniani hapo kesho.
P
 
Wanabodi,
Niko kwenye voluntariy lockdown, hivyo leo nimapata fursa ya kuangalia TV ya Zanzibar, ZBC, Mwandishi wa habari wa CCM Zanzibar, Daudi Ismail anamhoji Makamo wa Rais wa JMT, Mhe. Samia Suluhu Hassan anauzungumzia Muungano, kiukweli huyu Mama Samia anauzumguza vizuri muungano huku akiongea kwa heshima, taratibu, kwa utulivu na unyenyekevu, na anaongea vizuri mpaka raha, na kwa wale wenzangu na mimi wenye udhaifu na macho fulani, kiukweli Mwenyenzi Mungu amemjaalia macho mashaalah, huchoki kumsikiliza, utatamani aendelee tuu kuongea na kipindi kisiishe!.

Kwa hoja za muungano Mama Samia alizoshusha, ningekuwa ni uwezo wangu, ningeshauri October 2020, Mama Samia ndiye ampokee Dr. Shein kule Zanzibar, ili 2025, aje ampokee Magufuli, maana kwa maoni yangu, kwa uongeaji huu, huyu mama ndiye Mzanzibari pekee anayekubalika kuweza kuchagulika kuwa rais wa JMT kutokea Zanzibar, vinginevyo Wazanzibari wausahau kabisa urais wa Muungano, wao mwisho wao ni umakamo wa rais pekee.

Anasema Zanzibar inafaidika sana na muungano, kisiasa, kiuchumi na kijamii, ikiwemo kufaidika kielimu, wakati wa muungano, Zanzibar haikuwa na chuo kikuu chake hivyo Wanzanzibari wote wa enzi hizo waliofika elimu ya vyuo vikuu, wamesomea bara.

Mama Samia amesema watu waachiwe kuujadili muungano kadri watakavyo na hata kutema nyongo kuhusu muungano, na serikali inazitumia hizo hoja zinazolalamikiwa kuimarisha muungano, akasema ni heri watu wafunguke na kusema hivyo kuyatoa madukuduku yao, kuliko kunyamaza na madukuduka ndani yao, siku wakilipuka moto utawaka, hivyo watu waachwe waseme.

Amesema Zanzibar ni visiwa hivyo viko wazi pande zote, hivyo faida kubwa kabisa ya muungano ni ulinzi usalamax amani na na utulivu wa Zanzibar, bila muungano, ilikuwa ni rahisi sana kuivamia Zanzibar na Zanzibar ikivamiwa ni rahisi sana kuivamia bara, hivyo muungano umeimarisha sana ulinzi na usalama, amani na utulivu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kuna kitu Mama Samia amekisema sikuwahi kukijua!. Kumbe Wizara ya Mambo ya Nje ilipokiwa ikiitwa Wizara ya Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa ndio ilikuwa ya Muungano iki handle issues zote za Zanzibar kimataifa, lakini , ilipobadilishwa jina na kuitwa Wizara ya Mambo, ya Nje na Ushirikiano wa Africa Mashariki, sasa ina handle mambo ya Zanzibar ndani ya Africa Mashariki tuu, lakini kimataifa, kwa yale mambo ambayo sio ya muungano, SMZ ya Zanzibar imepewa uhuru wa kunegotiate ufadhili, misaada, na mikopo na mikataba ya kimataifa kwaniaba ya Zanzibar, ila kwenye kutiliana saini, anayetia saini ni serikali ya JMT, kwasababu Zanzibar haina sovereignty, sovereignty ni moja tuu ambayo iko kwenye JMT pekee!.

Hili sikuwahi kulijua, hivyo kumbe sasa Zanzibar inaweza kupata misaada na mikopo ya kimataifa, sasa kwavile uwiano wa kugawana misaada ya kutoka nchi wafadhili na wahisani, Zanzibar inastahili kupata asilimia 4.5% ya misaada yote kwa Tanzania, sasa kwa vile Zanzibar nayo inaweza kuomba ufadhili wa kimataifa, jee hii misaada ya kimataifa ya Zanzibar inayoomba, Tanzania bara pia tunapewa ule mgao wa asilimia 95.5% ya misaada ya Zanzibar, au misaada ya Tanzania tuu, ndio Zanzibar inapaswa kugaiwa asilimia 4.5%, lakini kwa misaada ya Zanzibar, then misaada hiyo ni ya Zanzibar pekee?.

Mama Samia amezungumzia kero za muungano na kusema kero nyingi zimeisha tatuliwa ila utekelezaji ndio unasua sua, na kutolea mfano deni lililokuwa la umeme la Tanesco, deni hilo lilisababishwa na double taxation, kwa Tanesco kuwachaji SMZ VAT huku shirika la umeme la Zanzibar, Zesco nalo likiwachaji kodi ya ongezeko la thamani Vat, wateja watumiaji wa umeme zao nao wakilipishwa Vat, kero hiyo imetatuliwa kwa Tenesco hawaichaji tena Vat kwa SMZ, hivyo Zanzibar haidaiwi tena deni lolote la umeme na Tanesco.

Ninachokumbuka kwenye deni la umeme la Zanzibar, lilitokana na Tenesco kuuza umeme kwa bei ya juu kwa Zesco, halafu Zesco wanauza umeme huo kwa bei ya chini Zanzibar, kumbe ilikuwa ni issue ya VAT!.

Pia amezungumzia kero za muungano kadri zinavyotatuliwa, kero nyingine zinaibuka, hivyo issue za kero za muungano ni issue endelevu.

Kuhusu usawa wa kijinsia kwenye uongozi, amesema Mungu aliumba jinsia tofauti kwa maana yake, hivyo ni vizuri wanawake wakajikubali kwa uanawake wao na kutimiza majukumu ya wanawake kama dini na Mungu alivyodhamiria, na wanaume nao watimize majukumu yao, nafasi za kazi au uongozi zisifanye wanawake kujisahau majukumu yao ya kutunza familia, na kuipongeza Tanzania, wanawake na wanaume ni sawa, akatolea mfano kuna nchi wanawake na wanaume wanafanya kazi ile ile lakini wanawake wanalipwa pungufu ya wanaume, na kuna nchi, wanawake ndio wazalishaji mali lakini hawaruhusiwi kupokea mshahara, siku ya mshahara, waume zao ndio wanakuja kuwapokelea. Tanzania mishahara inafanana na wanawake wanaruhusiwa kuingiza kipato.

Alipoulizwa kuhusu malalamiko ya watalii licha ya kuingia Tanzania na passport zao kugongwa entry, lakini wakifika Zanzibar, wanakaguliwa tena na kujaza fomu upya, Mama Samia alisema hizo ni hatua za kawaida za kiusalama, hata yeye kufuatia kuwa na jina la Hassan na kuna nchi alifika na ujumbe wa Tanzania, wengine wote waliruhusiwa yeye akazuiliwa kwa saa kadhaa hadi walioojiridhisha ndipo akaruhusiwa.

Amezungumza mengi na kumalizia kwa kusisitiza Muungano ni jambo jema, tuulinde na kuuenzi.

Kwa hoja kama hizi za huyu mama Samia, kama age sio issue sana, si huyu mama atatufaa sana 2025 au tuwashauri kwa vile Magufuli analamika sana kuhusu urais, mara ni mateso, mara ni kazi ngumu, mara ni mzigo mzito, tumshauri rais Magufuli, kwa vile Samia anatosha sana, hivyo tumpunguzie mateso, hana haja ya kuendelea na mateso, mzigo mzito na kazi ngumu ya urais, na hata kama ni wale tausi au wanyama wa Magogoni, au yale majabali ya Chamwino, tutamjengea Chato na kumuomba bora apumzike tuu mapema, na kumpisha Mama Samia ndio amalizie ngwe yake iliyobakia?. Hili mnalionaje?.

Paskali
Rejea
Siku ya Wanawake Duniani: VP Samia Suluhu: "Womanly, Genuine, Humble, Simple na Down To Earth! - JamiiForums

Siku ya Wanawake Duniani: Je, Tuna Wanawake Wenye Sifa za Presidential Material?! - JamiiForums

Wajue The Top Five Most Prominent Members wa Bunge Maalum la Katiba!. - JamiiForums

New Cabinet: Baadhi ya Majina ni Haya Hapa!. - JamiiForums

Makamu wa Rais, Samia Suluhu aweza kuendana na kauli za Rais Magufuli - JamiiForums
mi naona sawa tu ila kwakuwa maisha yamekuwa ghali, kuna mfumuko wa bei , na vijana wanakimbia mashambani kuja kuendesha bodaboda mjini, MAMA samia aitishe tume huru uchaguzi ufanyike, mshindi atangazwe kihalali, lakini inshort CCM wapishe , miaka 60 ya u askini inatosha.
 
Nakuunga mkono Jaji Mfawidhi , tatizo sio CCM kupisha, tatizo ni CCM wampishe nani?.
P
 
Wanabodi,
Makamo wa Rais wa JMT, Mhe. Samia Suluhu Hassan anauzungumzia Muungano, kiukweli huyu Mama Samia anauzumguza vizuri muungano huku akiongea kwa heshima, taratibu, kwa utulivu na unyenyekevu, na anaongea vizuri mpaka raha, huchoki kumsikiliza, utatamani aendelee tuu kuongea na kipindi kisiishe!.

Kwa hoja za muungano Mama Samia alizoshusha, ningekuwa ni uwezo wangu, ningeshauri October 2020, Mama Samia ndiye ampokee Dr. Shein kule Zanzibar, ili 2025, aje ampokee Magufuli, maana kwa maoni yangu, kwa uongeaji huu, huyu mama ndiye Mzanzibari pekee anayekubalika kuweza kuchagulika kuwa rais wa JMT kutokea Zanzibar, vinginevyo Wazanzibari wausahau kabisa urais wa Muungano, wao mwisho wao ni umakamo wa rais pekee.

Anasema Zanzibar inafaidika sana na muungano, kisiasa, kiuchumi na kijamii, ikiwemo kufaidika kielimu, wakati wa muungano, Zanzibar haikuwa na chuo kikuu chake hivyo Wanzanzibari wote wa enzi hizo waliofika elimu ya vyuo vikuu, wamesomea bara.

Mama Samia amesema watu waachiwe kuujadili muungano kadri watakavyo na hata kutema nyongo kuhusu muungano, na serikali inazitumia hizo hoja zinazolalamikiwa kuimarisha muungano, akasema ni heri watu wafunguke na kusema hivyo kuyatoa madukuduku yao, kuliko kunyamaza na madukuduka ndani yao, siku wakilipuka moto utawaka, hivyo watu waachwe waseme.

Amesema Zanzibar ni visiwa hivyo viko wazi pande zote, hivyo faida kubwa kabisa ya muungano ni ulinzi, usalama, amani na na utulivu wa Zanzibar, bila muungano, ilikuwa ni rahisi sana kuivamia Zanzibar na Zanzibar ikivamiwa ni rahisi sana kuivamia bara, hivyo muungano umeimarisha sana ulinzi na usalama, amani na utulivu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Leo ni Sikukuu ya Muungano, nachukua fursa hii kuutafakari Muungano wetu adhimu, kupitia hoja mbalimbali za kimuungano.

Nawatakia maadhimisho mema ya muungano na mapumziko mema.
P
 
Hii ndio inaitwa Flight of Ideas.

Heading inazungumzia mambo ya muungano...

Paragraph ya kwanza uzuri na sauti ya mama samia....

Paragraph ya pili urais wa zanzibar.....

Paragraph ya mwisho urais wa jmt....

Which is which?
Unforgetable
Mkuu Kingsmann , hizi flights ideas zinapokuja ku materialize, zinageuka kuwa ni maneno ya unabii!, hivyo next time ukikutana na flights ideas, uzizipuuzie!. Mungu huzungumza na waja wake kwa namna nyingi!.
p
 
Kwa hiyo umeamua kujadili Mama yetu Samia Suluhu Makam wa Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania..

Nenda kituo chochote kilichojirani na wewe kwa mahojiano zaidi.
Mkuu idawa , kwenye the freedom of expression, mtu unaruhusiwa kujajidili jambo lolote as long as huvunji sheria!.
P
 
Back
Top Bottom