"Watu waachwe Huru kuujadili Muungano"- VP, Samia Suluhu Hassan. Huyu mama anaongea vizuri kwa Unyenyekevu mpaka raha. Huchoki kumsikiliza

"Watu waachwe Huru kuujadili Muungano"- VP, Samia Suluhu Hassan. Huyu mama anaongea vizuri kwa Unyenyekevu mpaka raha. Huchoki kumsikiliza

Mama Samia yuko vizuri sana. Tafuta clip alipomtembelea Tundu Lissu pale Hospitalini Nairobi. Utamfaidi Samia orijino yaani bila zile mbwembwe za kisiasa. Mama mmoja mtamu saaana.
Naunga mkono hoja
P
 
Kwa hali ya covid 19 ilivyo katika taifa letu ni vigumu kutabiri nani atakuwa rais wa nchi mwishoni mwa mwaka huu wakuu wanamchezea mgeni sebuleni na hajali idadi ya walinzi wanaomzunguka mzee you never know Pasco imagine wale wazee wa kucheza na kura wakati wako busy kuiba mara paap anaanguka mmojawapo kwa kushindwa kupumua
Mkuu Hassan J. Mosoka , duh...!. hizi kauli nyingine hizi!.
P
 
Ni kweli mkuu, lakini inaonekana Samia orijino ni mwanaharakati, kama alivyoeleza. Pia ni maverick. Hii ina maana ni kweli mara kadhaa atakuwa alitofautiana saaana na Magufuli. Hebu imagine, Magufuli na ubabe wake kuwaita "Pumbavu" waziri Daktari Mpango na Prof. Kabudi, wanaume, hivi atakuwa kamuitaje Samia, mwanamke? Na Samia naye atachukuliaje?

Pia inaonekana ni mpenda haki. Aliwahi kuwasifia hadharani wabunge wa upinzani bara, kuwa wanajenga hoja vizuri na hata akathubutu kudai wabunge wa ccm wapewe semina! Nadhani system haikufurahia hali hiyo. Na hapa tumemsikia akiwasifia wapinzani katika baraza la wawakilishi kwamba wanajenga hoja vizuri kuliko wa ccm! Na pia kwamba mawaziri wa serikali ya ccm ni waongo. Mtu wa aina hii si anapata taabu sana katika serikali iliyojaa unafiki, ya awamu ya 5?
Mkuu Mindi , naunga mkono hoja
P
 
Umeanza Tena kujipendekeza kwa uyu RAISI mpya[emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
Humu jf tuna vilaza wengi kuliko tunavyo jidhania!. Ukikutana na thread yoyote, kabla hujachangia, kwanza angalia ni thread ya lini, unaweza kuchangia hoja zako ukijijua unachangia kitu cha maana, kumbe ni utumbo mtupu!.
Pole!.
P
 
Wanabodi,
Niko kwenye voluntariy lockdown, hivyo leo nimapata fursa ya kuangalia TV ya Zanzibar, ZBC, Mwandishi wa habari wa CCM Zanzibar, Daudi Ismail anamhoji Makamo wa Rais wa JMT, Mhe. Samia Suluhu Hassan anauzungumzia Muungano, kiukweli huyu Mama Samia anauzumguza vizuri muungano huku akiongea kwa heshima, taratibu, kwa utulivu na unyenyekevu, na anaongea vizuri mpaka raha, na kwa wale wenzangu na mimi wenye udhaifu na macho fulani, kiukweli Mwenyenzi Mungu amemjaalia macho mashaalah, huchoki kumsikiliza, utatamani aendelee tuu kuongea na kipindi kisiishe!.

Kwa hoja za muungano Mama Samia alizoshusha, ningekuwa ni uwezo wangu, ningeshauri October 2020, Mama Samia ndiye ampokee Dr. Shein kule Zanzibar, ili 2025, aje ampokee Magufuli, maana kwa maoni yangu, kwa uongeaji huu, huyu mama ndiye Mzanzibari pekee anayekubalika kuweza kuchagulika kuwa rais wa JMT kutokea Zanzibar, vinginevyo Wazanzibari wausahau kabisa urais wa Muungano, wao mwisho wao ni umakamo wa rais pekee.

Anasema Zanzibar inafaidika sana na muungano, kisiasa, kiuchumi na kijamii, ikiwemo kufaidika kielimu, wakati wa muungano, Zanzibar haikuwa na chuo kikuu chake hivyo Wanzanzibari wote wa enzi hizo waliofika elimu ya vyuo vikuu, wamesomea bara.

Mama Samia amesema watu waachiwe kuujadili muungano kadri watakavyo na hata kutema nyongo kuhusu muungano, na serikali inazitumia hizo hoja zinazolalamikiwa kuimarisha muungano, akasema ni heri watu wafunguke na kusema hivyo kuyatoa madukuduku yao, kuliko kunyamaza na madukuduka ndani yao, siku wakilipuka moto utawaka, hivyo watu waachwe waseme.

Amesema Zanzibar ni visiwa hivyo viko wazi pande zote, hivyo faida kubwa kabisa ya muungano ni ulinzi usalamax amani na na utulivu wa Zanzibar, bila muungano, ilikuwa ni rahisi sana kuivamia Zanzibar na Zanzibar ikivamiwa ni rahisi sana kuivamia bara, hivyo muungano umeimarisha sana ulinzi na usalama, amani na utulivu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kuna kitu Mama Samia amekisema sikuwahi kukijua!. Kumbe Wizara ya Mambo ya Nje ilipokiwa ikiitwa Wizara ya Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa ndio ilikuwa ya Muungano iki handle issues zote za Zanzibar kimataifa, lakini , ilipobadilishwa jina na kuitwa Wizara ya Mambo, ya Nje na Ushirikiano wa Africa Mashariki, sasa ina handle mambo ya Zanzibar ndani ya Africa Mashariki tuu, lakini kimataifa, kwa yale mambo ambayo sio ya muungano, SMZ ya Zanzibar imepewa uhuru wa kunegotiate ufadhili, misaada, na mikopo na mikataba ya kimataifa kwaniaba ya Zanzibar, ila kwenye kutiliana saini, anayetia saini ni serikali ya JMT, kwasababu Zanzibar haina sovereignty, sovereignty ni moja tuu ambayo iko kwenye JMT pekee!.

Hili sikuwahi kulijua, hivyo kumbe sasa Zanzibar inaweza kupata misaada na mikopo ya kimataifa, sasa kwavile uwiano wa kugawana misaada ya kutoka nchi wafadhili na wahisani, Zanzibar inastahili kupata asilimia 4.5% ya misaada yote kwa Tanzania, sasa kwa vile Zanzibar nayo inaweza kuomba ufadhili wa kimataifa, jee hii misaada ya kimataifa ya Zanzibar inayoomba, Tanzania bara pia tunapewa ule mgao wa asilimia 95.5% ya misaada ya Zanzibar, au misaada ya Tanzania tuu, ndio Zanzibar inapaswa kugaiwa asilimia 4.5%, lakini kwa misaada ya Zanzibar, then misaada hiyo ni ya Zanzibar pekee?.

Mama Samia amezungumzia kero za muungano na kusema kero nyingi zimeisha tatuliwa ila utekelezaji ndio unasua sua, na kutolea mfano deni lililokuwa la umeme la Tanesco, deni hilo lilisababishwa na double taxation, kwa Tanesco kuwachaji SMZ VAT huku shirika la umeme la Zanzibar, Zesco nalo likiwachaji kodi ya ongezeko la thamani Vat, wateja watumiaji wa umeme zao nao wakilipishwa Vat, kero hiyo imetatuliwa kwa Tenesco hawaichaji tena Vat kwa SMZ, hivyo Zanzibar haidaiwi tena deni lolote la umeme na Tanesco.

Ninachokumbuka kwenye deni la umeme la Zanzibar, lilitokana na Tenesco kuuza umeme kwa bei ya juu kwa Zesco, halafu Zesco wanauza umeme huo kwa bei ya chini Zanzibar, kumbe ilikuwa ni issue ya VAT!.

Pia amezungumzia kero za muungano kadri zinavyotatuliwa, kero nyingine zinaibuka, hivyo issue za kero za muungano ni issue endelevu.

Kuhusu usawa wa kijinsia kwenye uongozi, amesema Mungu aliumba jinsia tofauti kwa maana yake, hivyo ni vizuri wanawake wakajikubali kwa uanawake wao na kutimiza majukumu ya wanawake kama dini na Mungu alivyodhamiria, na wanaume nao watimize majukumu yao, nafasi za kazi au uongozi zisifanye wanawake kujisahau majukumu yao ya kutunza familia, na kuipongeza Tanzania, wanawake na wanaume ni sawa, akatolea mfano kuna nchi wanawake na wanaume wanafanya kazi ile ile lakini wanawake wanalipwa pungufu ya wanaume, na kuna nchi, wanawake ndio wazalishaji mali lakini hawaruhusiwi kupokea mshahara, siku ya mshahara, waume zao ndio wanakuja kuwapokelea. Tanzania mishahara inafanana na wanawake wanaruhusiwa kuingiza kipato.

Alipoulizwa kuhusu malalamiko ya watalii licha ya kuingia Tanzania na passport zao kugongwa entry, lakini wakifika Zanzibar, wanakaguliwa tena na kujaza fomu upya, Mama Samia alisema hizo ni hatua za kawaida za kiusalama, hata yeye kufuatia kuwa na jina la Hassan na kuna nchi alifika na ujumbe wa Tanzania, wengine wote waliruhusiwa yeye akazuiliwa kwa saa kadhaa hadi walioojiridhisha ndipo akaruhusiwa.

Amezungumza mengi na kumalizia kwa kusisitiza Muungano ni jambo jema, tuulinde na kuuenzi.

Kwa hoja kama hizi za huyu mama Samia, kama age sio issue sana, si huyu mama atatufaa sana 2025 au tuwashauri kwa vile Magufuli analamika sana kuhusu urais, mara ni mateso, mara ni kazi ngumu, mara ni mzigo mzito, tumshauri rais Magufuli, kwa vile Samia anatosha sana, hivyo tumpunguzie mateso, hana haja ya kuendelea na mateso, mzigo mzito na kazi ngumu ya urais, na hata kama ni wale tausi au wanyama wa Magogoni, au yale majabali ya Chamwino, tutamjengea Chato na kumuomba bora apumzike tuu mapema, na kumpisha Mama Samia ndio amalizie ngwe yake iliyobakia?.

Paskali
Rejea
Siku ya Wanawake Duniani: VP Samia Suluhu: "Womanly, Genuine, Humble, Simple na Down To Earth! - JamiiForums

Siku ya Wanawake Duniani: Je, Tuna Wanawake Wenye Sifa za Presidential Material?! - JamiiForums

Wajue The Top Five Most Prominent Members wa Bunge Maalum la Katiba!. - JamiiForums

New Cabinet: Baadhi ya Majina ni Haya Hapa!. - JamiiForums

Makamu wa Rais, Samia Suluhu aweza kuendana na kauli za Rais Magufuli - JamiiForums
Nawatakia maadhimisho mema ya Sikukuu ya Muungano .

Paskali
 
Mama Samia amesema watu waachiwe kuujadili muungano kadri watakavyo na hata kutema nyongo kuhusu muungano, na serikali inazitumia hizo hoja zinazolalamikiwa kuimarisha muungano, akasema ni heri watu wafunguke na kusema hivyo kuyatoa madukuduku yao, kuliko kunyamaza na madukuduka ndani yao, siku wakilipuka moto utawaka, hivyo watu waachwe waseme.
Nashauri hata katiba, watu waruhusiwe kuijadili katiba.
P
 
Back
Top Bottom