Watu waliokataa Magufuli asiongezewe Miaka ndio haohao wanashadadia Mbowe aendelee kuongoza. Ndio haohao wanakapinga CCM isiendelee! Unafiki mtupu!

Watu waliokataa Magufuli asiongezewe Miaka ndio haohao wanashadadia Mbowe aendelee kuongoza. Ndio haohao wanakapinga CCM isiendelee! Unafiki mtupu!

Ndiyo hao hao wakisikia, mama tutamchukulia fomu kwa lazima aongoze awamu ya tatu, watadai demokrasia.
Sijui kwanini chawa wa chadema wanayoyadai kwa ccm na serikali yake hawayataki yatumike kwa chama.
huwa wanahoji kwanini chawa wa ccm husifia kila kitu cha serikali na chama hata kama cha kijinga. Lakini sasa wanapinga kwanini tundu lissu anapingana na mambo ya ajabu yanayoendelea kwenye chama kwamba kwa kufanya hivyo ametumwa, anatumika, hafai, mbowe aliokoa maisha yake n.k.

Kwa kweli Watanzania sio wajinga. Waache waendelee kushabikia Simba na Yanga kuliko huu upuuzi
 
Magufuli alikuwa Rais wa nchi, Mbowe ni mwenyekiti wa CHADEMA.
Nchi ni ya watu wote, wenye vyama na wasio na vyama, wenye dini, wasio na dini wapagani n.k
CHADEMA ni ya wanachadema

Kwenye suala la uongozi kwenye hii nchi yetu. Lazima uelewe CCM ndio wenye nchi.
Nchi sio ya wote. Nchi ni yaccm.
Huo ndio mtazamo wa Watawala.

Kwa hiyo unaposema CHADEMA ni yawanachadema lazima uelewe pia nchi hii ni yawanaccm ambapo ndani yake kuna wanachadema
 
Rafiki yako TL lazima akuibue Taikon wa Fasihi umeanza kumpambania tangu 2020 mpaka sasa
 
Naludia tena chama ni Mali ya umma ndo maana wanaokipigia kura chama kwenye uchaguzi wowote ni wananchi wote wewe utakuwa unachanganya kati ya kikundi Cha kufa na kuzikana na chama Cha siasa Kwa maana kwenye kikundi Cha kufa na kuzikana mnazikana wanakikundi tu

Mwambie kila mwezi wanachukua kodi za Watanzania kama ruzuku.
Yoda anajizima Data
 
Hata yanga ikicheza mechi inaangaliwa na watu wote ikiwemo wa Simba, Azam, Tabora n.k ila Yanga ni ya wanayanga.
Kama unafikiri CHADEMA ni mali ya umma nenda wewe mwanaCCM kapige kura za kumchagua mwenyekiti wa CHADEMA.

Kwa hiyo madai yanayosema CHADEMA ni Saccos ya Mbowe yapo sahihi?
 
Mpo salama!

Watu wenye ndimi mbili. Watu wenye mawe mawili ya kupimia ni watu Hatari Sana popote walipo. Ni watu wanafiki na muda wowote wanaweza kukuuza.

Alipokuwepo Magufuli, Chawa wake walitoa maoni Yao kuwa Magufuli aongezewe Muda, Magufuli atawale milele, na kama Magufuli angekataa wapo walioapa wangemshikia kiboko kumlazimisha aendelee kutawala. Yalikuwa ni maoni Yao.

Sisi wengine maoni yetu tulikataa tukasema Hapana. Miaka yake ikiisha inatosha. Wengine tukasema Katiba hairuhusu lakini Katiba ni kitabu tuu tunaweza kukibadilisha sehemu ndogo (Constitution amendment) ili kuweka kipengele cha kuongeza Muda.

Haya walewale ambao waliwaka, walimkalia kooni JPM ambaye yeye mwenyewe hata hakuwahi kusema ataongeza Miaka zaidi ya yeye kutamka hataongeza Miaka. Leo hii kile walichokuwa hawakitaki kwa JPM wanakifanya kwenye chama Chao.

Mbowe hata angekuwa kiongozi mzuri kama Malaika, kumuongezea Miaka mingine juu ya ishirini sio Sawa.

Alafu Mbowe angetakiwa aonyeshe uzuri wake katika kuandaa viongozi wengine wazuri zaidi yake wa kumrithi.

Siongei kumtetea Lisu awe kiongozi nope! Anaweza kugombea mtu mwingine Nje ya Lisu na akawa kiongozi wa CHADEMA hii itaonyesha kuwa CHADEMA inaakiba ya kutosha ya viongozi.

Kama kuna watu wanaona Mbowe aendelee Basi wasishangae wale wanaoona CCM iendelee.

Wanasema Mbowe kaitoa CHADEMA Mbali.
Watu wanasema CCM imeitoa nchi Mbali.

Uongozi mzuri ni pamoja na kuweza kuachia nafasi wengine waongoze.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Taikon
Honhera uzi una elimu kubwa huu
 
Kitu ambacho nina uhakika nacho hadi hivi sasa ni kwamba Mbowe hatagombea
 
Labda tufahamu vizuri kwanza SACCOS ni nini na huwa inafanya nini?
Pia kama kuna SACCOS ya mtu?
Tofauti na Mbowe watu gani wengine wanamiliki SACCOS binafsi?

Si umesema CHADEMA ni yawanachadema?
Na sio chama cha Watanzania.

Ndio nikakuambia kuwa madai ya wanaosema CHADEMA ni Saccos kumbe ni sahihi?

Unafikiri ni Kwa nini vyama vya upinzani vinapewa ruzuku?
 
Waporaji wa uchaguzi serikali za mitaa wanapotamani Mbowe amwachie Lissu kijiti - kaa chini tafakari kwa kina.
Kweli Mbowe amefanya kazi kubwa hadi hapa tulipo. Lakini jinsi ccm wanavyopora uchaguzi na aina ya siasa za leo, aiseee! Mbowe na siasa zake za mabembelezano miaka 20 inatosha. Abaki kama mshauri...

Pi
Kwa hiyo madai yanayosema CHADEMA ni Saccos ya Mbowe yapo sahihi?
CCM na CHADEMA ni pipa na mfuniko. Tena bora ccm wanabadili m/kiti kila baada ya miaka 5/10. CHADEMA m/kiti wa milele. Na anayejaribu.....
 
Muulize babu yako kama hajawahi kulishwa mahindi ya njano ya Wamarekani ya msaada asife njaa.

Tanzania haijawahi kupewa msaada wowote na mabeberu.

Labda hujui maana ya capitalism. Ukijua maana yake na hizo nchi zinazotoa msaada hutoweza kusema Tanzania iliwahipewa msaada.
 
Kweli Mbowe amefanya kazi kubwa hadi hapa tulipo. Lakini jinsi ccm wanavyopora uchaguzi na aina ya siasa za leo, aiseee! Mbowe na siasa zake za mabembelezano miaka 20 inatosha. Abaki kama mshauri...

Pi

CCM na CHADEMA ni pipa na mfuniko. Tena bora ccm wanabadili m/kiti kila baada ya miaka 5/10. CHADEMA m/kiti wa milele. Na anayejaribu.....

Kwa kinachotaka kutokea ni mara Mia CCM
 
Back
Top Bottom