Watu waliokuwa kwenye pikipiki waua watu zaidi ya 50 Nigeria

Watu waliokuwa kwenye pikipiki waua watu zaidi ya 50 Nigeria

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Taarifa kutoka kaskazini magharibi mwa Nigeria zinasema kuwa majambazi waliokuwa wakiendesha pikipiki wamewauwa zaidi ya watu hamsini katika msururu wa uvamizi uliodumu kwa saa kadhaa katika vijiji vya mbali.

Wakazi wa Magami waliiambia BBC kwamba watu wenye silaha kwanza walishambulia kijiji cha ‘Yar-Doka Jumatano wakati walinzi wa kijiji kutoka vijiji jirani walipoingilia kati kusaidia, washambuliaji walizidisha mashambuliokatika maeno mengine ya vijiji.

Baadhi ya wakazi wanasema walihesabu miili ya watu walau 51 na watu wengien zaidi hawajulikani walipo.
Majeruhi wanatibiwa katika hospitali iliyopo katika Magami uliopo karibu. Msemaji wa polisi katika jimbo la Zamfara, Muhammad Shehu amethibitisha mashambulio hayo katika mazungumzo na BBC lakini hakuweza kutoa idadiyoyote ya majeruhi.

Alisema kikosi cha usalama na maafisa wa serikali walikuwa njiani kuelekea katika eneo la tukio kutathmini hali.
Baadhi ya waathiriwa wanasemekana kuwa i watu ambao walikuwa wamesambaratishwa na mashambulio ya awali ambao sasa walikuwa wanarejea nyumbani – wakitumai kuandaa mashamba yao kwa ajili ya msimu wa mvua unaoanza.

Jimbo hilo limekuwa likihangaika na harakati za magenge ambayo yamekua yakiendesha mashambulio hivi karibuni- na kufanya uvamizi mbaya na utekaji nyara kwa ajili ya kikombozi.

Mauaji katika jimbo la Zamfara yalitolewa chini ya saa 24 baada ya kikundi kingine kuvamia chuo kiku katika jimbo jirani la kaduna na kumpiga risasi hadi kumuua mfanyakazi na kuwateka nyara watu wanafunzi.

1619091269856.gif
 
Mhh huko Nigeria ni kiboko sijui hayo mambo yataisha lini wanauana sana huko aisee...
 
Ukabila na udini ni sumu mbaya sana, ikiisha kuingia mwilini haitoki.
 
Hivi hii vita dhidi ya "magaidi" duniani nini kifanyike? Maana majeshi yameshindwa
 
Back
Top Bottom