Watu waliomkufuru Mungu wakafariki dunia

Usiogope ni uzushi tu.. hakuna aliewai kufa kwa sababu ya kuhoji mambo haya ya kufikirika..na kudanganya watu..

Suala sio kuhoji, kuna tofauti kati ya kuhoji na KUKUFURU. Jaribu kukufuru uone. Bahati mbaya hautaona kwasababu utakuwa umekufa.
 
Na hao miungu bandia waliwezaje kuhudhuru mkutano na huyo mungu kwa mjibu wa zaburi 82,kama kweli walikua bandia?


Mkuu ukisoma Hiyo Zaburi 82:1-8 bila Shaka utaelewa Mungu anazungumza juu ya miungu gani! Hasa ule mstari Wa 5,6,7 utaelewa vzr Kua Miungu gani Hiyo itakayo kufa ambayo Mungu anazungumzia! Na hapo Mungu hakukutana na Hiyo miungu Bali amekua akisima kujidhirisha kati ya Hiyo miungu na kuwatoa masikini ktk Yule Muovu! 82:3,4
 
Usiogope ni uzushi tu.. hakuna aliewai kufa kwa sababu ya kuhoji mambo haya ya kufikirika..na kudanganya watu..
Ushahidi ulioubeba mgongoni mwako ni huu,unaposema nilizaliwa mwaka 19...,chanzo cha huko kuhesabu ni kuzaliwa kwa masihi wengine wanamuita mesaya na huyu alitumwa na Mungu. kizazi hiki hatuwezi epuka ua kukana uwepo wa Mungu maana hata tukikana nafsi zetu zinatusuta maana hata vyeti vyetu vya shule,kuzaliwa,passport na vingine vinavyotuhusu vinabeba ujumbe wa kuzaliwa kwa masihi.
 

Ni makubaliano yalifanywa ili kuanzisha mfumo wa kuesabu miaka/muda kuanzia kwa yesu..wengine wanatumia mfumo wa hijira wa kiislamu wa kuhesabu kuanzia 622 a.d. wala si mfumo wa mungu..
tena kuonesha mfumo una tatizo huyo yesu alizaliwa 4 b.c.e sio zero..
na kuanzishwa kwa mfumo huu haukutumia miujiza ya yesu bali makubaliano tu..
 
Kukufuru ni msamiati wa kuogopesha watu wasihoji tu.. yaani dini zina mbinu mbalimbali kuanzisha dogma watu wasihoji

Nimeshasema, fanya kufuru, tutashuhudia. bahati mbaya wewe hautaelewa kwani utakuwa Marehemu. Kama nilivyosema kuna tofauti kati ya kufuru na kuhoji.

Mfano kuna mabinti watatu USA walikuwa wamelewa, wakaenda kwa mama ya mmoja wao kumsalimia. Walikuwa na gari. Wakiwa njiani kwenda kwa mama ya rafiki walipita Supermarket wakanunua mayai.

Wakati wa kuondoka, mama aliwaambia "Mungu awatangulie". Mmoja akajibu na wenzake wakamsapoti kwa kiherehere cha pombe. Hawezi kututangulia sisi labda akakae nyuma kwenye buti la gari. Basi wakaondoka, si muda mrefu taarifa zikaja, wamepata ajali na kufariki hapo hapo. Ajabu hakuna hata yai moja lilivunjika.

Hiyo ndio kufuru tunayoongelea hapa. Ni tofauti kabisa na kuhoji. Kuhoji ni kitu kingine na kufuru na kitu kingine.

Fanya jaribio la kukufuru, tutakusikia.
 
Asante kwa mfano wako mzuri!

 

Hapo penye red,hiyo A.D inawakilisha neno ano domino ikiwa na maana ya baada ya kristo kiswahili wanatumia B.K baada ya kristo.Na hata walioishi kabla ya kristo linatumika neno la kiingereza B.C before christ.Yote katika yote hakuna njia rahisi ya kukwepa ukweli huu,uwe na dini usiwe na dini.
 
Sorry bro! je hata wewe ukifa itakuwa ni kwa sababu ya kukufuru? kama sivyo je kutkuwa na tofauti gani kti yako na hao uliowataja hapo juu
 

Hutulazimiki kutumia B.C wala A.D tunaweza kutumia B.C.E before common era au B.P before present.. kwahiyo mambo ya yesu si muhimu kabisa hapo
 
Mkuu mleta mada hizi habari ulizoleta ni za uongo at best na unproven kwa kuanzia huyo Azuza alikufa kwa Ukimwi na sio cancer ili kupanda na upande wa pili wa habari taomba uweke hii link Untimely Deaths of Famous People Who Mocked God - Fiction! and Unproven! kwenye post yako ili usipotoshe UMMA. Kutangaza na kushare imani its all well and good ila kusambaza imani yako kwa njia ya uongo ni Utapeli na ulaghai..., (Ukizingatia Imani yako inakutuma kusema kweli daima)
 
Hutulazimiki kutumia B.C wala A.D tunaweza kutumia B.C.E before common era au B.P before present.. kwahiyo mambo ya yesu si muhimu kabisa hapo
Samahani, ngoja niwahi nyama yangu ya kiti moto inapoa.
 


Mkuu kwani wewe hujui kuna Mungu na miungu? Miungu ya hapa duniani ipo mingi tuu google utapata kila aina ya miungu iliyopata kuishi hata katika kipindi cha kina socrates 400 B.C...lakini Mungu wetu ndiye creator wa hawa walioitwa miungu baada ya kumuasi akawatupa kutoka mbinguni

Hio hapa chini ni moja kati ya miungu iliyokuwa inaabudiwa na kuishi na watu enzi hizo...aliwekwa kwenye cover ya album ya mwanamuziki satanist Ozzy Osbourne
 

Attachments

  • 1394218063552.jpg
    30.5 KB · Views: 94
Mp.umb.avu husema moyoni mwake kuwa hakuna Mungu

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums

Isaya 45:7
Mimi naiumba nuru, na kulihuluku giza; mimi nafanya
Suluhu, na kuhuluku ubaya; Mimi ni BWANA , niyatendaye hayo yote.
(NIV)
Isaya 45:7
Mimi hufanya mwanga na kuumba giza ;
Huleta fanaka na kusababisha balaa.
Mimi , Mwenyezi-Mungu hutenda vitu hivi vyote.
(GNV)
 

I like the confidence..
 

Kuna watu ambao hawa amin kabisa kuwa mungu yupo, wanasema fiction kama wewe, bimafsi sijaona kitu ambacho kimeweza kukubalika na kuaminika ulimwengu mzima pasipokukoselewa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…