Tambua tu kwamba wewe kama husomi vitabu umekwisha, uko gizani na umepitwa sana na unaendelea kupitwa.
Mtu asiye msomaji wa vitabu ni sawa na mtu mfu anayetembea. Asiye msomaji wa vitabu hawezi kujua faida na manufaa ya usomaji wa vitabu. Usomaji wa vitabu ni chakula cha akili, huimarisha uwezo wa kufikiri na uwezo wa kujenga hoja. Usomaji wa vitabu huchangamsha akili, huongeza maarifa, huimarisha msamiati na hukuza uwezo wa lugha. Huboresha kumbukumbu, hujenga uwezo wa uchambuzi wa masuala mbalimbali, hujenga uwezo wa kuandika na umakini na pia njia bora ya kupunguza sononi.
Msomaji wa vitabu ana maudhui ya kutosha (Content) kuliko asiyesoma vitabu. Hata inapotokea ubishani au uchangiaji mada utaiona waziwazi tofauti ya wasomaji na wasio wasomaji wa vitabu. Wasio wasomaji badala ya kujadili hoja watapayuka, wataonesha ghadhabu, watashambulia mtu binafsi badala ya kutetea hoja yake. Mara nyingi wasomaji wa vitabu watachangia hoja kwa utulivu, kwa kujenga hoja na mifano na rejea mbalimbali kutoka kwenye vitabu alivyosoma, bila ghadhabu wala kupayuka.
Is reading the key to success?
It has been proven that children who read better, preform better in school and have a more active imagination, leading to a larger world and more possibilities for success.