Watu walionufaishwa na Usomaji wa Vitabu

🙏🙏🙏
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji120]

Usomaji utakusaidia kuepukana na umbra.

Wasomaji wa vitabu wanapokutana, ni kawaida kwao kujadili "ideas", lakini wale wengine sasa! Wakikosa cha kuongea huishia kuwajadili watu.
Yaani mkuu ukisoma vitabu ni rahisi kuwadanganya watanzania namuheshimu ruge lakini alikuwa anawakamata kupitia vitabu wananifurahisha wakisema ogopa mungu na teknolojia halafu wanasema ni msemo wa ruge watanzania wenzangu tusome vitabu tuache ujinga na kudanganywa.
 
Kati ya jambo ambalo ninamshukuru sana Mungu, ni kuwa na tabia ya usomaji wa vitabu.

Sijui ningekuwaje bila vitabu! Vitabu vimenisaidia sana, vimenitoa pabaya mno.

Mtu anayekejeli usomaji wa vitabu ni wa kuonewa huruma sana. Najua, anayekejeli hajui kuwa hajui, hasa ikizingatiwa kuwa katika ulimwengu huu, karibia kila mtu utakayekutana naye, hata yule aliyeonekana wazi kuwa ni "mjinga", bado atajiona ana akili kukuzidi.

Ndiyo maana asiyejua manufaa ya vitabu haoni mapungufu yake. Atakapofanikiwa kujenga urafiki na vitabu ndiyo atajigundua kuwa alikuwa anaishi ndani ya boksi lenye giza katika ulimwengu mpana wenye nuru.
 
You are right mkuu!

Hata Nyerere alikuwa msomaji sana wa Vitabu.

Umenikumbusha na Mwalimu mmoja, miaka ile nikiwa kidato cha Sita, alishawahi kuniambia kuwa "HATA MUNGU ANASEMA JISAIDIE KWANZA NDIPO NAMI NIKUSAIDIE", nilipomwuliza ilikoandikwa, aliishia kuniambia tu kuwa ni kwenye Biblia!

Maskini Mwalimu wa watu! Kumbe hiyo kauli ilikuwa ni ya Benjamin Franklin, mwanafalsafa wa Marekani aliyependa vitabu kuzidi hata chakula. Si bure mpaka sasa Wamarekani wangali wakimkumbuka! Alilisadia sana taifa lake. Na siri ya mafanikio yake ni ulafi wa vitabu. Alivifakamia mno.

Kama huyo Mwalimu angelikuwa msomaji wa vitabu, angefahamu kuwa huo usemi ulikuwa ni wa Benjamin Franklin na siyo Biblia.

Kusoma vitabu vizuri kunalipa sana.

Shukran mkuu🙏! Umenikumbusha mbali!!!
 
🤣🤣🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…