Watu wanakwenda University/Chuo ili iwe nini?

Watu wanakwenda University/Chuo ili iwe nini?

nzalendo

JF-Expert Member
Joined
May 26, 2009
Posts
12,106
Reaction score
12,916
Wasalaam si kama nina pinga elimu la hasha!

Lakini kwa upande wangu sioni sababu ya kwenda Chuo Kikuu ''haraka'' mara tu umalizapo kidato cha sita.
Watu wengi huenda kwa kuiga bila kuwa na mpango mahsusi au kujiuliza baada ya chuo/au nina kwenda ''chuo'' then what next?(KUJITAMBUA)

Ieleweke wazi dunia hii tunayoishi ni tofauti na ile ya zama za mwanzo za Uhuru.

Mfumo wetu wa Elimu hasa ya Chuo na Sekondari si rafiki tena kukuwezesha wewe uweze kujitegemea.
Hivyo usitafute/hangaikie kitu ambacho ni kama mchezo wa kubahatisha.

Mfano unasoma

1. Sheria halafu eti unarudi mtaani unaanza ujasiriamali wa kutengeza sabuni na blah blah.

2. Unasoma Sijui nini B nini komu..halafu unakuja mtaani eti wewe unaanza ukulima ...hivi maana ya elimu ni nini hasa?

Mbona hao wasioenda CHUO wanafanya mambo ya maana kuliko mtu unaejiita eti msomi halafu mambo unafanya kinyume kabisa na usomi?

(ZAMANI NYUMBA YENYE MTU WA FORM FOUR,UKIPITA HATA KWA NJE,UTAJUA HII NYUMBA ANAKAA MSOMI)

Mfano.

1.Mwanamuziki Diamond yeye alisema hana mpango wa kwenda shule kusoma watu walimshangaa sana ...lakini mimi nilimuunga mkono...manake alisema kama akienda shule atasoma lugha na muziki lakini si kwenda kusoma Jiografia kitu ambacho anaona hakitamsaidia. ''bora aachie wengine wahangaike navyo.''

2. Hivi hamuoni wahindi?.....mbona hawahangaiki na mambo yenu ya chuochuo na wana fanikiwa sana? wanaangalia upepo Je?ana nia ya ''Transport'' yeye ataenda kujifunza usafirishaji na mara nyingi si shule.

( WENGI HUJIFUNZIA MITAANI TU)

''Umefika wakati mfumo wa Elimu ubadilike''
 
Kwa kweli wazungu walete turn dawa ya kuwazindua waafrika kutoka usingizini...

Ushahidi mwingine wa underdevelopment no huu
 
Una elimu gani wewe? Okay hao wanaomaliza form six wamefundishwa na watu gani? Unavyougua unaenda hospitali au unatumia miti shamba? Barabara unazopita zimejengwa na akina nani?
Shehe nielewe vizuri.
Nimeanza kwa kusema si kama napinga Elimu,La! Hasha.
Watu mnatakiwa muwe na maono.kesho yako haijengwi na wewe kwenda Chuo.
Au kwa kutokwenda University si mwisho wa maisha.
Mfano.
Aliye sababisha Hospitali ya KCMC iwepo,marehemu Mch.Stephano Mosha Elimu yake ilikuwa ni ya Form four tu.
Leo hii kuna mijitu ina ma Phd,blah blah,Je? Wamefanya kitu gani?
 
Nimekusoma mtoa mada lkn lazima baadhi ya watu waende vyuo vikuu otherwise System zitasimama
Bila chuo kikuu nani atatengeneza bia,saa,simu,Atm,Mpesa,Ndege,magari,madawa,usindikaji nani atabuni formula.Shule ni muhimu mno.Sema sio kila mtu ni wa kwenda chuo kikuu
 
Vizuri mkuu ila hao madokta, manesi wanaotibu watu huko wangetoka wapi kama wasingefika huko vyuo vikuu, Kuna professional mbalimbali bila vyuo vikuu watapatikana kweli

labda useme tusilazimishe kila mtu asome anaependa kusoma asome anaetaka kupita njia nyingine aende tu maana ndo maisha kila mtu atakayoyachagua
 
Unaweza kusoma mpaka ukamaliza vyuo vyote ukarudi na kujifanya unabuni miradi,miradi yenyewe eti small scale agriculture.. Ha ha ha ha ha hii ndo bongo dsm
 
Nimekusoma mtoa mada lkn lazima baadhi ya watu waende vyuo vikuu otherwise System zitasimama
Bila chuo kikuu nani atatengeneza bia,saa,simu,Atm,Mpesa,Ndege,magari,madawa,usindikaji nani atabuni formula.Shule ni muhimu mno.Sema sio kila mtu ni wa kwenda chuo kikuu
I Like you point.
Thank you
Merci.
Asante
Bene gratsie
Haika
Wabheja
Ndaga
Asante karesaa
Asante Mkwaiii
 
Unaweza kusoma mpaka ukamaliza vyuo vyote ukarudi na kujifanya unabuni miradi,miradi yenyewe eti small scale agriculture.. Ha ha ha ha ha hii ndo bongo dsm

Small scale agriculture ndio inaendesha Tanzania mkuu. Unafikiri kila mtu angekua mchuuzi tungekula nini?
 
Ulichoongea ni kweli kabisa.. Sema hapa tutapinga kutokana na madhara ya hiyo elimu tuliyopata.. Hasa wale ambao wamekalia madawati ya vyuo vikuu miaka 3/4 na hawajapata ajira..

Nina mdogo wangu,, kamaliza kidato cha sita mwaka 2014 akapata div3 ya point 11.. Hakupata Chuo kwa kozi aliyokua anataka (udaktari).. Nikamshauli aje jeshini then atasoma baadae.. Akapinga sasa hivi anaangaika mtaani wakati wale wenzake wapo TMA.. kiukweli haina haja ya kuunga Chuo direct wakati hakuna mustakabali mbeleni.. Sikwenda Chuo ila nimeajiriwa.. Plan.. Plan
 
Hujanielewa!!!
Nimeanza kwa kuandika...''si kwamba napinga Elimu,La! hasha''....

bonge la ujumbe sema tu hujasomeka kwa watu wengi! ni vyema na haki mtu aka focus kwenye fun yake na sio kufuata mkumbo. kama unakwenda chuo kwa lengo la kuendeleza fun yako its okay lakini kama unakwenda chuo kwa fun isiyo yako umepotea kabisaaa... kwani utajutia mda na pesa ulizo poteza. "Do the right thing in the right place at the right time"
 
Ulichoongea ni kweli kabisa.. Sema hapa tutapinga kutokana na madhara ya hiyo elimu tuliyopata.. Hasa wale ambao wamekalia madawati ya vyuo vikuu miaka 3/4 na hawajapata ajira..

Nina mdogo wangu,, kamaliza kidato cha sita mwaka 2014 akapata div3 ya point 11.. Hakupata Chuo kwa kozi aliyokua anataka (udaktari).. Nikamshauli aje jeshini then atasoma baadae.. Akapinga sasa hivi anaangaika mtaani wakati wale wenzake wapo TMA.. kiukweli haina haja ya kuunga Chuo direct wakati hakuna mustakabali mbeleni.. Sikwenda Chuo ila nimeajiriwa.. Plan.. Plan

Point 11 hadi 12 ilikua Div 2 at that time kabla huyu jamaa wa Bagamoyo hajachakachua Elimu, div 3 ilikua inaanzia point 13
 
bonge la ujumbe sema tu hujasomeka kwa watu wengi! ni vyema na haki mtu aka focus kwenye fun yake na sio kufuata mkumbo. kama unakwenda chuo kwa lengo la kuendeleza fun yako its okay lakini kama unakwenda chuo kwa fun isiyo yako umepotea kabisaaa... kwani utajutia mda na pesa ulizo poteza. "Do the right thing in the right place at the right time"

mi FUN yangu haipo chuo
 
for those who are born in poorest families, they do not have even a productive land, capital to invest, no ideas to implement! they need school to be taken out from the cave on how world goes, interaction btn pe'pl n' things are put in accordance.

the next generation will only need directives n' little education to fullfil their desires as long as they have capital.
 
Back
Top Bottom