Madaktari wa kwanza kabisa walienda shule gani kusomea udakrari?
Hayo maswali ya debate za ktoto.. Kuku na yai klianza kipi
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Madaktari wa kwanza kabisa walienda shule gani kusomea udakrari?
Madaktari wa kwanza kabisa walienda shule gani kusomea udakrari?
hili swali kwelikweli
yeye ameandika amejifikiria yeye kama yeye nafaida anayopata na sio jamii iliyomzunguka, kusema kweli baadhi ya kazi unasidia jamii zaidi kuliko ww unavyonufaika , mfano walimu .Una elimu gani wewe? Okay hao wanaomaliza form six wamefundishwa na watu gani? Unavyougua unaenda hospitali au unatumia miti shamba? Barabara unazopita zimejengwa na akina nani?
Ulichoongea ni kweli kabisa.. Sema hapa tutapinga kutokana na madhara ya hiyo elimu tuliyopata.. Hasa wale ambao wamekalia madawati ya vyuo vikuu miaka 3/4 na hawajapata ajira..
Nina mdogo wangu,, kamaliza kidato cha sita mwaka 2014 akapata div3 ya point 11.. Hakupata Chuo kwa kozi aliyokua anataka (udaktari).. Nikamshauli aje jeshini then atasoma baadae.. Akapinga sasa hivi anaangaika mtaani wakati wale wenzake wapo TMA.. kiukweli haina haja ya kuunga Chuo direct wakati hakuna mustakabali mbeleni.. Sikwenda Chuo ila nimeajiriwa.. Plan.. Plan
Angalau umeelewa nina maanisha nii uzini (ndani ya uzi huu).dugu, tatizo lililopo ni hili tunaishi kwenye jamii isiyokua na malengo ambayo haijitahmini kwamba baada ya kipindi fulani mtu awepo sehemu fulani nikiwemo mimi hapa, kipindi ninasoma chuo sikua na malengo yoyote yale nilichagua kozi ya sheria ambayo nilichagua tu sababu rafiki yangu fulabi alikua anaipenda hivyo akani convince kitu ambacho ninainterest nacho ni kutengeneza vikatuni na music videos sijutii kusoma hiyo kozi maana mpaka sasa hivi ninaweza kulinda mawazo yangu kisheria(intellectual property), ninaweza kunegotiate mkataba na pia kusajili kampuni kitu ambacho mbeleni nitakuja kukifanya, hivyo ningekua na malengo mazuri kipindi nipo chuoni ningeanzaga kujishughulisha mapema by the time ninamaliza ningekua mbali sana.
2.Suala la watu kusomea vitu vingine na kufanya vitu vingine hili ni suala binafsi na uelewa wa mtu unachangia watu kutokana na wewe mtu kuweza kujiuza kitu ambacho wahitimu wengi hawawezi either kuandika barua za kazi, pili hata kujua uombe vipi hiyo kazi technique namba moja ninayoikubali ni kutumia masomo uliyosoma na kufanya uwiano na kazi iliyotangazwa na pia watu waliosoma wengi wanakuaga na ujinga fulani mfano amesomea kiswahili na anaona kuna tangazo la kazi ya translator anashindwa kujiuza kuonesha ile kazi anaiweza ingawa anaehitajika ni mtu aliesomea kiingereza hivyo wengi hua hawaelewi mtu anaweza fanya kazi yoyote ile kutokana na kuicategorize degree uliyoisomea i.e social sciences,business studiea etc nikiri kwa degree yangu ya sheria sasa hivi ninafanya kazi ya social science sababu niliweza kujiuza vizuri hivyo wasomi wabadilike kwenye suala hilo
3.kuhusu suala la wahindi na kutokusoma hilo ninalipinga maana asilimia kubwa ya wahindi wamesoma hatakama ni kuunga unga lakini vyuoni watakwenda either mumbai,canada, au uingereza na fani zao hua ni udaktari, engineering na accountancy kama unabisha angalia mtandao wa linkedin uone cv zao, ambae atakua ameunga unga utamkuta amesoma learn IT, diploma ya IT na kuendelea na wengi utakuta wanakampuni za IT au wameajiriwa kama IT personnel, kuhusu kufanya biashara wengi wao wanaelewa nini maana ya umaskini hivyo wamejiwekeza kwenye biashara kwa kupata mitaji either kihalali au isivyo halali na pia hawana ubinafsi bali husaidiana wao kwa wao bila matatizo tatizo letu waswahili hata tukitaka kuinuana kifamilia lazima atatokea mpigaji moja atataka kudhulumu watu wote either hela au chochote pia sisi waswahili hatuna uaminifu unakuta mtu anakukopa elfu 50 anasema wiki ijayo nitakurudishia lakini anaaanza kua chenga etc etc oh mambo yameingiliana sijui nini na nini
Kwaio suluhisho ni hili mtu inabidi uwe na maleng na hiyo shule au chuo unachoenda kusomea pia watu wasikariri unachosomea ndo utakacho kuja fanyia kazi sababu soko la ajira haliwezi accomodate watu wote hence only the best are selected(sio interms of GPA bali jinsi unavyojiuza)na pia unachotakiwa kujua ni kwamba mchakato wa kusoma ni mrefu sana maana stnd 1-form 6 ni miaka 13 ya kusoma hiyo kama umeanza shule na miaka 7 na kama haujafeli unamaliza form 6 na miaka 20 jumlisha miaka mitatu au minne ya chuo hapo ni balaa unakuja mtaani hujui kujiuza huna mawazo alternative zaidi ya kuajiriwa unakua frustrated maana expectations na reality hazija kutana.....nashauri watu wagoogle kitabu cha poor dad rich dad ni alternate ya kuondoa frutration za maisha na pia watu wamshirikishe Mungu katika kupata mawazo bora ya biashara maana binafsi nimeona umuhimu wake bado kutekeleza tu....nimetumia simu niwie radhi kama maandishi hayajakaa vizuri na pia ni ndefu sana