Watu wanaorekodi matukio ya watu wakiwa wamelewa na kuyaposti mtandaoni bila idhini yao washughulikiwe kisheria

Watu wanaorekodi matukio ya watu wakiwa wamelewa na kuyaposti mtandaoni bila idhini yao washughulikiwe kisheria

Hance Mtanashati

JF-Expert Member
Joined
Sep 7, 2016
Posts
20,137
Reaction score
26,189
Ipo wazi inajulikana pombe sio chai na mtu akinywa pombe uwezo wake wa kufanya maamuzi kwa asilimia kubwa hupungua.

Sasa utakuta kuna huu mchezo wa kuposti watu wakiwa wamelewa kwenye sherehe au sehemu nyingine yoyote ile na wakawa wamechangamka kwa namna moja au nyingine then utakuta mtu hana mazoea na huyo mtu anaanza kumrekodi video kisha anaposti mitandaoni mwisho wa siku muhusika pombe zikimuisha kutokana na kusherehekea ipasavyo kwenye shughuli ya mtu wake wa karibu anajikuta yupo mitandaoni watu wanamdhihaki .

Wengine wanafanya kazi za kuheshimika na utakuta ni mabalozi wa makampuni mbalimbali ,kitendo cha kuposti hizo vitapelekea makampuni kusitisha kazi na muhusika tena hata heshima yake kushuka hali ya kuwa haikuwa akili yake ya kawaida bali ni furaha tu ya kilaji.

Hii inaleta athari kubwa sana, maana si kila mtu anaweza kustahimili hilo jambo mwisho wa siku itapelekea mwingine kupata sonona na kujidhuru kabisa ikiwezekana hata kujitoa uhai.

Kama kuna sheria inayowaadhibu watu wanaofanya mapenzi na watu waliolewa hata kama walikubaliana ,lakini kitendo cha kufanya mapenzi hali ya kuwa mmoja amelewa anaweza kwenda kushtaki na ukafungwa kabisa hata kama ni mtu wako wa ndoa.

Nadhani hili pia linaweza kuwezekana kudhibiti hawa wachukua matukio ya watu wakiwa kwenye kilaji na kuwaposti mitandaoni bila ridhaa ya muhusika.
 
Kumrekodi mtu bila idhn yake sio vibaya but vibaya ni kuitumia kwa maslai yako,au kupost bila ridhaa yake, mfano kuna tukio eti usirekodi kisa ypo mtu kalewa recod ukitaka kuitumia bas simple edit uwepo wake usionekane
 
Na nyinyi walevi mkilewa mbona mnatukana matusi hovyo....mnavunja viti hovyo,...mnawashika wahuduma makalio bila ruhusa yao.

Mwisho mkitembea barabara yote yenu....

Je, huu ni uungwana....Rahasha huu si ungwani basi tukisema tuwastaki mnasingizia pombe...!
 
Hii inahusu maana si mlevi wala mpiga picha walevi.
 
Back
Top Bottom