Watu wanaorekodi matukio ya watu wakiwa wamelewa na kuyaposti mtandaoni bila idhini yao washughulikiwe kisheria

Watu wanaorekodi matukio ya watu wakiwa wamelewa na kuyaposti mtandaoni bila idhini yao washughulikiwe kisheria

Ni adabu mbaya sana kupiga picha watu au kurekodi video watu bila idhini yao.Wewe unayechukua matukio kwa kamera,ukibabuliwa makofi au kushtakiwa kwa udhalilishaji utamlaumu nani?
Mbaya zaidi ikipostiwa tu mitandaoni inatrend vibaya sana, sasa utakuta wengine wana heshima zao ,kitendo cha kuwaposti wakiwa wamelewa kinashusha utu wao kwa kiasi kikubwa sana.
 
Kumrekodi mtu bila idhn yake sio vibaya but vibaya ni kuitumia kwa maslai yako,au kupost bila ridhaa yake, mfano kuna tukio eti usirekodi kisa ypo mtu kalewa recod ukitaka kuitumia bas simple edit uwepo wake usionekane
Hata kitendo cha kurekodi tu bila idhini ni mbaya hiyo,
Una rekodi ili iweje kwa mfano?
 
Unakuta umeenda na mchezo uji mara mshapigwa picha jamani
Unakuja kushtuka umeshafika TikTok na insta 🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣kama hiyo haitoshi unaletwa JF watu wanakujadili bila watu kujua muhusika nawe pia upo humu na huo uzi umechangia.
 
watu wa hii nchi wengi wao ni washamba na wanakosa ustaarabu kabisa
 
Back
Top Bottom