Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
Jiulize, kwani Tanzania ilikuwa imefikia wapi na Mchakato wa Katiba Mpya, na ni nini kilichokuwa kimebaki ili kuikamilisha?
Na pia jiulize, ni mambo gani yanatakiwa ili kuwa na Tume Huru ya Uchaguzi?
Sasa unapokuwa na majibu yanayojitosheleza ya maswali haya, ndio utoe kauli kuhusu haya mambo mawili. Lakini pia, nani amesema haiwezekani suala la Tume Huu ya Uchaguzi kufanyika sambaba na harakati za kuwa na Katiba Mpya? Kumbuka kwamba, Tume Huru ya Uchaguzi ni jambo ambalo tayari lipo kwenye Katiba Mpya iliyopendekezwa, na kukiri kwamba inahitajika haraka ni kukiri kwamba Katiba mpya inahitajika haraka..
Suala la kuwa na Tume Huru ya Uchaguz ni dogo sana, na halipaswi kuonwa kwamba liwe utangulizi wa Katiba Mpya. Na watu wakumbuke kwamba Tume Huru ya Uchaguzi ni lazima ipewe nguvu na Katiba, ambapo Katiba iliyopo haiwezi kuipa nguvu Tume Huru ya Uchaguzi. Ukilazimisha kuwa na Tume Huru ya Uchaguzi kwa Katiba iliyopo sasa basi utakuwa na Tume Huru ya Uchaguzi ambayo si tu haiko huru bali pia haina meno, kibogoyo.
Lakini jambo ambalo kila Mtanzania anapaswa kujua ni kwamba, ikiwa watu watakubali Tume Huru ya Uchaguzi liwe jambo la kutekelezwa kabla ya Katiba Mpya, basi wanabariki mbinu za kufanya Katiba Mpya isiwepo hadi baada ya 2025.
Labda kama watu wana utambuzi, basi wambane Samia na serikali ili watoke kauli ya lni basi suaa la Katiba Mpya litamalizwa. Tunatakiwa kusubiri hasi lini, mwezi gani, mwaka gani? La sivyo ni kudanganyana tu.