Watu wanasema mimi ni nani? Swali alilouliza Yesu linalofungua ubongo wa mwanadamu kujitambua

Na petro aliposema hiyo kufuru Yesu akamwambia wewe "shetani". Usisahau hilo.
 
Una maana gani?

Mathayo16:23 Akageuka, akamwambia Petro, Nenda nyuma yangu, Shetani; u kikwazo kwangu; maana huyawazi yaliyo ya Mungu, bali ya wanadamu.

 
Mathayo16:23 Akageuka, akamwambia Petro, Nenda nyuma yangu, Shetani; u kikwazo kwangu; maana huyawazi yaliyo ya Mungu, bali ya wanadamu.
Je waweza fungua uzi katika andiko hili ili tuje kujadili huko?
 
Wapi Yesu amesema "Mimi Mungu"?
 
Je waweza fungua uzi katika andiko hili ili tuje kujadili huko?
Hilo andiko linajibu andiko lako na nimelinukuu juu hapo. Kwanini nifungue uzi wakati najibu andiko lako?

Au imekuwa mwiba kwako?
 
Mathayo16:23 Akageuka, akamwambia Petro, Nenda nyuma yangu, Shetani; u kikwazo kwangu; maana huyawazi yaliyo ya Mungu, bali ya wanadamu.

Hahahaaa, hivi wewe unajua biblia au kanjanja tu kama shetani aliyemjaribu Yesu kubadili jiwe liwe mkate.. Unatumia vifungu vya biblia kwa tafsiri isiyo sahihi.... Hilo ni andiko lenye uhai muhimili katika Imani ya kikristo..

Fungua uzi tukusaidie kwa mapana yake.
 
Nikuweke sawa nini wakati mimi nimeuliza swali?

Wapi Yesu amesema "Mimi Mungu"?
Hapa

Ufunuo wa Yohana 21:5
Na yeye aketiye juu ya kile kiti cha enzi akasema, Tazama, nayafanya yote kuwa mapya. Akaniambia, Andika ya kwamba maneno hayo ni amini na kweli.
6 Akaniambia, Imekwisha kuwa. Mimi ni Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho. Mimi nitampa yeye mwenye kiu, ya chemchemi ya maji ya uzima, bure.
7 Yeye ashindaye atayarithi haya, nami nitakuwa Mungu wake, naye atakuwa mwanangu.
7
 

Wewe mtaalamu si ungalimjibu tu hapa au hata kufungua wewe huo uzi ??
 

Katika Kitabu cha Ufunuo 1, ayah ya 8, inaonyeshwa kuwa Yesu alisema yafuatayo kuhusu yeye mwenyewe:

“Mimi ni Alfa na Omega”, asema Bwana, aliyeko, aliyekuwako na anayekuja, Mwenye Nguvu”.

Hizi ni sifa za Mwenyezi Mungu. Hivyo, Yesu, kulingana na Wakristo , hapa anadai uungu.

Hata hivyo, maneno yaliyotajwa hapo juu, ni kulingana KJV.

Katika RSV, wanazuoni wa Biblia walisahihisha tafsiri na kuandika:

“Mimi ni Alfa na Omega”, asema Bwana Mungu, aliyeko, aliyekuwako na anayekuja, Mwenye Nguvu”.

Masahihisho pia yalifanywa kwa New American Bible (Biblia Mpya ya Marekani) iliyochapishwa na Katoliki.

Tafsiri ya Ayah hiyo imerekebishwa ili kuiweka katika muktadha wa sawa kama ifuatavyo:

“Bwana Mungu anasema: ‘Mimi ni Alfa na Omega, yule aliyeko na aliyekuwako na anayekuja, Mwenye Nguvu’”.

Kwa masahihisho haya, ni dhahiri kuwa hii ni kauli ya Mwenyezi Mungu wala sio kauli ya Yesu
 
Wapi Yesu amesema "Mimi Mungu"?
Ni wapi Yesu Kristo amesema ''Mimi Si Mungu"?

Mmoja wao alipoona kwamba ameponywa alirudi akimtukuza Mungu kwa sauti kubwa. 16Akajitupa chini mbele ya miguu ya Yesu huku akimshukuru. Huyo alikuwa Msamaria. 17Hapo Yesu akasema, "Je, si watu kumi walitakaswa? Wale tisa wako wapi? 18Hakupatikana mwingine aliyerudi kumtukuza Mungu ila tu huyu mgeni?" 19Halafu akamwambia huyo mtu, "Simama, uende zako; imani yako imekuponya."

Kwanini Yesu hakumkemea huyu Msamaria kuwa asimsujudie kwa kuwa Yeye si Mungu?
Luka 17:15-19

Na tena Mungu ana pomleta mwanae, mzaliwa wa kwanza ulimwenguni, anasema: “Malaika wote wa Mungu wamwabudu yeye.”
Waebrania 1:6

Faizafoxy, ebu tuambie, ni nani anayepashwa kuabudiwa?
Hapo juu ktk Luka 17:15-19 huyu Msamaria aliyeponywa ukoma alirudi kumshukuru nani?
 
Unapoteza muda kumuelewesha huyo..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…