Watu wanasema mimi ni nani? Swali alilouliza Yesu linalofungua ubongo wa mwanadamu kujitambua

mm sikufuatilii we ndo maana umekuja kwenye Uzi wangu


Kwani nilikufuatilia au nimechangia hoja ??

Nimekujibu kwa hoja umepata kiwewe ??? hapa hamna jukwaa la wakristo au waislamu umeweka uzi utajibiwa otherwise usiandike kitu maana hata walio na imani nyengine watakuona unadanganya au elimu yako bado changa
 
mm sikufuatilii we ndo maana umekuja kwenye Uzi wangu




KAZI NA UJUMBE WA YESU

"Maana Mwana wa Mtu alikuja kuwaokoa wale waliopotea". (Mathayo18:11)


"Sikutumwa ila kwa watu wa Israeli waliopotea kama kondoo". (Mathayo 15:24)


Yesu pia aliweka wazi ni nini Mwenyezi Mungu alimtaka afanye:


"Mimi sikunena kwa mamlaka yangu mimi mwenyewe, ila Baba aliyenituma ndiye aliyeniamuru niseme nini na niongee nini". (Yoshua12:49)

"Msidhani ya kuwa nimekuja kutengua sheria ya Musa au mafundisho ya Manabii, sikuja kutengua bali kukamilisha". (Mathayo 5:17)


Uchunguzi makini wa maneno ya Yesu unaonyesha kwamba, kinyume na Wakristo wanavyo fikiri, Yesu hakuwa na nia ya kuanzisha dini mpya; alikuja tu kuukamilisha na kuusisitizia ujumbe ambao Mwenyezi Mungu aliwapa Mitume wote waliotangulia kabla yake: kuwa Mwanadamu alitakiwa atii sheria za Mwenyezi Mungu na amuabudu Mwenyezi Mungu tu.


Hakuna wakati wowote katika kazi na maisha yake ya utume ambapo Yesu alidai kuwa zaidi ya mwanaadamu, aliyepewa ufunuo na kuongozwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu. Bila chembe ya shaka yeye mwenyewe alijiita kuwa ni mwana wa mtu, na akaweka wazi, katika aya nyingi ndani ya injili, kwamba yeye hakuwa lolote isipokuwa ni Mjumbe na Mtume aliyetumwa na Mwenyezi Mungu.


"Yesu akamjibu, Mbona unaniita mwema? Hakuna aliye mwema ila Mwenyezi Mungu peke yake". (Marko 10:18)

".. anayenipokea mimi, hanipokei mimi bali anampokea Yule aliyenituma". (Marko 9:37)

"Na uzima wa milele ndio huu, kukujua wewe uliye peke yako, Mungu wa kweli na kumjua Yesu kristo uliyemtuma". (Yohana 17:3)

"Mimi nimewaambieni ukweli niliousikia kwa Mungu, ninyi mwataka kuniua". (Yohana 8:40)

"Nakwenda juu kwa Baba yangu na Baba yenu, Mungu wangu na Mungu wenu". (Yohana20 :17)


Licha ya juhudi zake zote - maneno ya ajabu pamoja na miujiza mingi - Yesu alikataliwa, hususan na watu wake.


Miaka mitatu baada ya kuanza kazi yake ya utume, alikamatwa na kuhukumiwa kwa shutuma kwamba anasambaza maneno ya chuki miongoni mwa watu dhidi ya watawala na maneno mabaya dhidi ya vitu vyao vitukufu vya kidini. Mafanikio yalikuwa yamemkwepa - katika mwisho wa maisha yake hapa duniani, alikuwa amepata wafuasi kidogo sana wasiozidi 500.


Hali hii ilibadilika baadaye baada ya kuja nabii mpya, aliyedai kuzungumza kwa jina la Yesu, miaka michache baadaye.
 
Mathayo 16:23
Lakini Yesu akageuka, akamwambia Petro, “Ondoka mbele
yangu, Shetani! Wewe ni kikwazo kwangu. Mawazo yako si ya
kimungu ila ni ya kibinadamu!”
 



LUGHA YA YESU

Kila mti hutambulika kwa matunda yake (Luka 6:44) na vile vile mtu anatambulika kwa ulimi na lugha yake kwamba anazo nyendo za aina gani? Maana lugha ya mtu inaonesha masomo yake, tabia na nyendo yake.

Tunampima Bwana Yesu Kristo sawa na maandiko ya Biblia.

Bila ya kupoteza muda wa wasomaji wangu, ningependa kuwaletea baadhi ya maneno na lugha ya Bwana Yesu aliyotumia katika uhai wake.

1. Wasioamini (wasio Waisraeli) wameitwa mbwa na nguruwe. (Mathayo 7:6).

2. Aliwaita watu wabaya: ”Enyi wazao wa nyoka” (Mathayo 12:34).

3. Mayahudi waliitwa: “Kizazi cha zinaa.” (Mathayo 12:40,, 16:4).

4. Mayahudi waliitwa “Wazinifu na wakosefu.” (Marko 8:38).

5. “Ole wenu waandishi na wafarisayo, wanafiki,” (Mathayo 23:16).

6. “Ole wenu viongozi vipofu.” (Mathayo 23:16).

7. “Enyi nyoka, wana wa majoka” (Mathayo 23:33).

8. “Watu wengine waliitwa mbwa.” (Mathayo 15:27).

9. Aliwaita manabii wenzake: “wote walionitangulia ni wevi na wanyang'anyi.” (Yohana 10:8).

10. Aliwaita wanafunzi wake: ”Enyi kizazi kisicho amini, kilichopotoka.” (Mathayo 17:17).

11. Akamwambia Petro “Nenda nyuma yangu Shetani.” (Mathayo 16:23).

12. Akamwambia mama yake: “Ewe mwanamke nina nini nawe? (Yohana 2:4).

13. Akasema mama yangu ni nani na ndugu zangu ni akina nani? (Mathayo 12:48).

14. Siku ya Kiyama atawaita wahubiri Wakristo: “Nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi mtendao maovu.” (Mathayo 7:23).
 



WANAFUNZI WA YESU

Na majina ya hao mitume kumi na wawili ni haya;

Wa kwanza Simon aliyeitwa Petro, na Andrea nduguye; Yakobo wa Zebadayo, na Yohana nduguye; Filipo, na Bartholomayo; Tomaso, na Mathayo mtoza ushuru; Yakobo wa Alfayo; na Thadayo; Simon Mkananayo, na Yuda Iskariote, naye ndiye mwenye kumsaliti.(Marko 10:2-4).

Kila mti hutambulika kwa matunda yake (Luka 6:44).

Basi tuone mti uliopandwa na Bwana Yesu Kristo, matunda yake ni ya ladha gani? Madaraja yaliyofundishwa na Bwana Yesu tuone wanafunzi wake walikuwa wa aina gani?

Yesu alipoleta imani, basi tuone kiwango cha imani ya waaminio wake.

Sina kawaida ya kuwafundisha watu kwa maneno yangu bali nawafundisha kulingana na maandiko yao matakatifu.

Sasa tuone hali na imani ya wanafunzi wa Bwana Yesu.

1. Yesu alisema, hata sasa ninyi nanyi mngali hamna akili? (Mathayo15:16).

2. Alimwambia Petro kwamba; “Ewe mwenye imani haba, mbona uliona shaka? (Mathayo 14:31).

3. Petro alikanusha kuwa mfuasi wa Yesu mara tatu bali alimlaani. (Mathayo 26:69-75).

4. Yuda Iskariote alimuuza Yesu kwa shilingi 30 tu. (Mathayo 26:15).

5. Wakati Yesu alikuwa hatarini, wanafunzi waliendelea kulala). Mathayo 26:40-45; Marko 14:36:041).

6. Yuda alijinyonga. (Mathayo 27:5).

7. Imani ya wanafunzi: “Kwa sababu ya upungufu wa imani yenu” (Mathayo 17:20).

8. Ndipo wanafunzi wote wakamwacha wakakimbia. (Mathayo 26:50).

9. Wengi wataniambia siku ile; Bwana, Bwana hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? Ndipo nitawaambia dhahiri. Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu. (Mathayo 7:22-23).


Hapa juu mmesoma hali na imani ya wanafunzi wa Bwana Yesu sawa na Biblia. Lakini sisi Waislamu hatuamini kwamba Nabii yeyote anaweza kushindwa kiasi hiki kwamba asiweze kupata matunda ya juhudi yake na athari nzuri isitokee kwa mahubiri na mafundisho yake.

Hata katika Qur'an Tukufu wanafunzi wa Bwana Yesu wametajwa kuwa mfano mzuri juu ya ulimi wa Bwana Yesu mwenyewe. Qur'an:

“Enyi mlioamini! Muwe wasaidizi wangu kwa Mwenyezi Mungu kama alivyosema Isa bin Mariam kuwaambia wanafunzi (wake): Ni nani wasaidizi wangu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu? Wanafunzi wakasema: Sisi ni wasaidizi wa Mwenyezi Mungu.” (Qur'an 61:15).
 
Asante Sana mkuu Da'Vinci. Nimewahi kujiuliza hili swali lakini sikupata jibu kamili nikaishia kusema mimi ni mimi ninaeongea nabniliepo hapa.

Nilijiuliza je nini kinanitambulisha mimi ambacho ni cha kipekee hakifanani na mwingine kabsa? Je ni jina?

Internal Je jina linaweza kuwa utambulisho wangu katika jamii? Lakini ninkasema jina tu halitoshi kunitambulisha kwa maana wapo Internal wengi saana kwenye jamii hivyo jina haliwezi kuwa iutambulisho wangu wa peke yangu. Je! Nikibadili jina ukubwani ina maana utambulisho wangu umepotea kwa kubadili jina?

Sura. Je! Sura yangu inaweza kuwa ndo utambulisho wangu lakini nikasema hapana maana wanasema Duniani wawili wawili yani yupo mwingine mwenye Sura kama yangu hivyo sura haiwezi kunifanya wa tofauti na wa kipekee pekee.

Rangi: Rangi nyeusi haiwezi kuwa utambulisho wangu weusi tuko wengi siwezi kutafutwa kwa rangi yangu nikapatikana mimi tu mana tuko wengi. Je na hao ambao walikuwa weusi na sasa wamejicaro ina maana utambulisho wao umepotea?

Tabia: mbona tabia zinafanana sana, hivi kweli tabia yangu ikiwa mbaya au njema inaweza kuwa ndo utambulisho wangu? No. Ikiwa nilikuwa na Tabia njema na sasa niko na tabia mbaya ni kusema utambulisho wangu umepotea?

Maswali ni mengi sana ya kujiuliza kuhusu mimi ni nan.
Ila mimi ni mimi nilieandika hapa.
 
Mkuu ukishajiuliza hayo maswali hapo juu basi utagundua kua mtu ni kusudi/Purpose ili ujue kusudi lako inabidi umuulize Mungu kusudi lako ni lipi?
Mungu asiyeonakana wala kuwa na uwepo?? utarudi pale pale dunia ni game kuna vitukura wanatuchezea WORLD MATRIX.
 
Elimu ya utambuzi ndio kitu wengi wetu tunamiss, hasa the purpose of living? Tunaishi kwasababu gani hasa?
 
Elimu ya utambuzi ndio kitu wengi wetu tunamiss, hasa the purpose of living, why do i live?
 
MTAZAMO naomba link ya Uzi wako unaohusu mashahidi was Uganda. Thanks
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…