Watu wanatumia Akili sana kupata kipato mjini mipango

Watu wanatumia Akili sana kupata kipato mjini mipango

je parle

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2018
Posts
2,022
Reaction score
3,919
Ijumaa mubaraka.....

Mjini hapa mambo ni mengi muda ni mchache sana.hili jiji lina kila aina ya mambo.

Niende kwenye ajenda.
Katika harakati zangu za kutafuta kabiashara kakukidhi mahitaji ya nyumbani .Nikawa nafuatalia biashara ya kuuza mafuta ya kula kwa kupima kwa wamama wa mtaani.basi bwana nikapita sehemu nyingi wanauza 5000 kwa litle 1 na bei kubwa ni 5200.

Nikaaanza kutafuta wanauzaje jumla kwa dumu la litle 20 nikakuta ni 81,000 na plastic ni 83,000.nikasema sawa ngoja nitafute kijiwe na kijana aweze kufanya hii biashara .ila target yangu ni kuuza dumu mbili kwa siku.itakuwa bado sio mbaya nikimtoa kijana 7000 per day ntabaki na chochote kitu kwa mahesabu yafuatayo

Dumu 2
40x81.000=162,000
Plus + 4000
Total 166,000

Nitauza ifauatavyo 40x5000=200,000

Mwisho wa siku 200,000-166,000=34,000
Nikitoa kijana 7000
Nabaki na 27.000

Haya ndio mahesabu ambayo nilikuwa napiga kichwan mwangu........

Haya twende sasa.

Katika kuingia field sasa nakutana na kituko kuna wadau wanauza mafuta hayo hayo aliyonunua kwa 83,000 kwa plastic .wao wanauza 4,000 kwa litre
Nikachoka kabisa nikajiuliza how do they benefit.?????

20x4,000=80,000
Mafuta kanunua 83.000 iweje auze bei ya elfu 4 alafu bado anaendelea na hii biashara.??? Mimi sikusita nikataka kujua nivipi hapa mbona mahesabu hayajakaa sawa? Nikamfata dogo anaeuza kumuuliza akasema subiri brother ntakuambia.nikasubiri pale mana foleni ni kubwa .akitoka huyu anaingia huyu wakina mama kibao.mwisho wa siku dogo ananiambia mafuta nanunua duka flani nenda kaulize wanauzaje.Nikaenda nikakuta bei ndio hiyo hiyo 83.000 tsh nikachoka kabisa.!

Nikamuuliza muuza duka inakuwaje jamaa wananunua kwa bei hiyo alafu wanauza elfu 4 ? Akasema hizo ndoo zinazobaki ndio faida yao yan hao wanauza tu mafuta ili wabaki na ndoo hayo mafuta hayana faida...na pia inawezekana ile little moja yao haitimiiiiiiiiii......dah nikachoka kabisa niakondoka. Ila sikukata tamaa nikarudi tena kwa dogo labda kuona mafuta wanachanganya na kitu kingine au laaa......

Akakata plastic lingine ni mafuta safi na litle anatumia hizi za maji ya uhai kupima litle moja.ni kweli wala hapunji ila bei ni hiyohiyo.ila najua pale kuna code imefungwa inatakiwa kufunguliwa kuna namna inatumika kupata faida angalau elfu kwa dumu.....kama kuna mtu anajua namna wanavyofanya ili kupata faida anijuze hapa nataka kuingia huku.nimesikia huyu mdau anauza hadi dumu 50 per day.......

Nimeamini mjini unatakiwa kuacha kupanic na kualaumu tu serikali bali unatakiwa kutumia akili nyingi uli uishi....
 
Nimecheka saana, Kwamba wanauza mafuta hawapati faida. Faida yao ni ndoo, Dadeqq [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Ndio inaonekana hivyo.
 
Biashara inahitaji Hesabu kali saaana, Kama kwa siku anauza dumu 50.
Bei ya kuuza kila dumu empty mfano ni 3,000 - 5,000 ukizidisha mara 50
Jamaa ana uhakika wa 150,000 - 250,000 kwa siku, Apo umetoa pembeni mtaji wake wa mafuta.
Unyama sana [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Bro dumu tupu bei yake ni buku mpk buku jero haizid zaid ya hapo.
 
Huu uzi umenihamasisha sana.

uwezekano wa kupata faida ya Tsh elfu 10 kwa kila ndoo upo na bado ndoo nikaiuza elfu 5 bei ya hasara

Bei ya mafuta ni elfu 90 ndoo lt 20.

lita 1 hapa wajomba wanauza 5,100.

Hapo naona ana creti 2 za soda na chupa zake anapimia mafuta.

Chupa 1 (350mils) anauza 1,800.

Faida ipo siwezi kwenda kulinda tena😂😂😂
 
Huu uzi umenihamasisha sana.

uwezekano wa kupata faida ya Tsh elfu 10 kwa kila ndoo upo na bado ndoo nikaiuza elfu 5 bei ya hasara

Bei ya mafuta ni elfu 90 ndoo lt 20.

lita 1 hapa wajomba wanauza 5,100.

Hapo naona ana creti 2 za soda na chupa zake anapimia mafuta.

Chupa 1 (350mils) anauza 1,800.

Faida ipo siwezi kwenda kulinda tena[emoji23][emoji23][emoji23]
Mzeee ndoo kubwa ni 83,000 hapo mbagala rangi tatu.

Hii ishu naifuatilia wiki sasa natembea kwa wale wanauza reja reja.nimebahatika kufungua codes zote mambo hadharani.
 
Mzeee ndoo kubwa ni 83,000 hapo mbagala rangi tatu.

Hii ishu naifuatilia wiki sasa natembea kwa wale wanauza reja reja.nimebahatika kufungua codes zote mambo hadharani.
Mkuu tatizo hujauliza napatikana wapi au bei ni ya wapi😅😅😅
 
Mkuu Kuna hii code walikufungulia!?

Ile chupa anayotumia muuza mafuta momkama kipimo nadhani ni ya maji ya hills water,? ambazo Kitako chake kina asili ya kua flat, sasa wao wanaogelea na mkondo huo.

Zile chupa hua wanazikalisha kidogo kwenye hot plate , zinapungua ukubwa maana yake kwenye Kila Lita Moja ya ukweli yeye hakosi walau 50 mils za kubana kipimo.

Kipimo cha robo si wanapimia kikombe sio!?. Kiuhalisia kama Lita Moja ni 5000 basi tunatarajia kipimo Cha robo kiuzwe Kwa 1250, ila wao wanatumia kikombe kidogo ambacho sio 250 mils bali ni 200 mils na tena kipimo chao kwa juu kinakua kimekatwa so kipimo hakitimii faida nyingine tayari hiyo.

Watumiaji wa rejareja wengi ni kinamama wa majumbani sasa akiuza hizo robo robo Kwa wingi ndipo faida yake yeye hutuna zaidi.
 
Mkuu Kuna hii code walikufungulia!?

Ile chupa anayotumia kama kipimo nadhani ni chupa ya maji ya ..... Zile ndefu mimi nimesahau jina.... Uongo?

Zile chupa nadhani hua wanazikalisha kidogo kwenye hot plate , maana yake kwenye Kila Lita Moja ya ukweli yeye hakosi walau 50 mils za kubana kipimo.

Kipimo cha robo si wanapimia kikombe sio!?. Kiuhalisia kama Lita Moja ni 5000 basi tunatarajia kipimo Cha robo kiuzwe Kwa 1250, sawa si sawa!?. Mimi hesabu za mwalimu wa kata kiasi zinanisumbua.

Lakini wao wanatumia kikombe kidogo ambacho sio 250 mils bali ni 200 mils na tena kipimo chao kwa juu kinakua kimekatwa so kipimo hakitimii.

Watumiaji wa rejareja wengi ni kinamama wa majumbani sasa akiuza hizo robo robo Kwa wingi ndipo faida yake yeye hutuna zaidi.
Dogo anaeuza nilimrubuni akanipa namba nikampigia.nikamwambia nipe password ya hayo mafuta unapataje faida ?? Kasema bwana hapa katika lita 20 mimi natoa lita 22 kuna namna ya upimaji.wale wa robo robo huwa hazitimii ila lita moja inakuwa sawa.ila ile chupa kama inaonekana kama haipo sawa.

All in all wanategemea zile ndoo tupu waliuza ndio wanabutua.......
 
Biashara inahitaji Hesabu kali saaana, Kama kwa siku anauza dumu 50.
Bei ya kuuza kila dumu empty mfano ni 3,000 - 5,000 ukizidisha mara 50
Jamaa ana uhakika wa 150,000 - 250,000 kwa siku, Apo umetoa pembeni mtaji wake wa mafuta.
Unyama sana [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Dumu ni 1500 bei ya jumla
 
Mzeee ndoo kubwa ni 83,000 hapo mbagala rangi tatu.

Hii ishu naifuatilia wiki sasa natembea kwa wale wanauza reja reja.nimebahatika kufungua codes zote mambo hadharani.
Kwenye Ile Lita Kuna namna hufanya yaan ndani ya Lita kunakuwa na kitako kingine hapo inajazwa kitu flan usawa flan na juu ndiyo kitako cha pili inawekwa ili kupunguza ujazo usifike Lita 1kamili yaani kipimo kinaenda had kupitia kipimo chao Cha Lita 1 wanaweza kupata Lita 2 had 3 za ziada (dumu la Lita 20 wao wakipima kwa kipimo chao wanatoa Lita 23) ukitaka ku prove hili nenda na Lita Yako kama Yao afu waambie wakupimie kwenye Ile Yako watagoma au nunua afu uende kwako kapime Lita Moja itakuwa haipo kamili
 
Back
Top Bottom