Watu wanatumia Akili sana kupata kipato mjini mipango

Watu wanatumia Akili sana kupata kipato mjini mipango

Ijumaa mubaraka.....

Mjini hapa mambo ni mengi muda ni mchache sana.hili jiji lina kila aina ya mambo.

Niende kwenye ajenda.
Katika harakati zangu za kutafuta kabiashara kakukidhi mahitaji ya nyumbani .Nikawa nafuatalia biashara ya kuuza mafuta ya kula kwa kupima kwa wamama wa mtaani.basi bwana nikapita sehemu nyingi wanauza 5000 kwa litle 1 na bei kubwa ni 5200.
Nikaaanza kutafuta wanauzaje jumla kwa dumu la litle 20 nikakuta ni 81,000 na plastic ni 83,000.nikasema sawa ngoja nitafute kijiwe na kijana aweze kufanya hii biashara .ila target yangu ni kuuza dumu mbili kwa siku.itakuwa bado sio mbaya nikimtoa kijana 7000 per day ntabaki na chochote kitu kwa mahesabu yafuatayo

Dumu 2
40x81.000=162,000
Plus + 4000
Total 166,000

Nitauza ifauatavyo 40x5000=200,000

Mwisho wa siku 200,000-166,000=34,000
Nikitoa kijana 7000
Nabaki na 27.000

Haya ndio mahesabu ambayo nilikuwa napiga kichwan mwangu........


Haya twende sasa.

Katika kuingia field sasa nakutana na kituko kuna wadau wanauza mafuta hayo hayo aliyonunua kwa 83,000 kwa plastic .wao wanauza 4,000 kwa litre
Nikachoka kabisa nikajiuliza how do they benefit.?????

20x4,000=80,000
Mafuta kanunua 83.000 iweje auze bei ya elfu 4 alafu bado anaendelea na hii biashara.??? Mimi sikusita nikataka kujua nivipi hapa mbona mahesabu hayajakaa sawa? Nikamfata dogo anaeuza kumuuliza akasema subiri brother ntakuambia.nikasubiri pale mana foleni ni kubwa .akitoka huyu anaingia huyu wakina mama kibao.mwisho wa siku dogo ananiambia mafuta nanunua duka flani nenda kaulize wanauzaje.Nikaenda nikakuta bei ndio hiyo hiyo 83.000 tsh nikachoka kabisa.! Nikamuuliza muuza duka inakuwaje jamaa wananunua kwa bei hiyo alafu wanauza elfu 4 ? Akasema hizo ndoo zinazobaki ndio faida yao yan hao wanauza tu mafuta ili wabaki na ndoo hayo mafuta hayana faida...na pia inawezekana ile little moja yao haitimiiiiiiiiii......dah nikachoka kabisa niakondoka. Ila sikukata tamaa nikarudi tena kwa dogo labda kuona mafuta wanachanganya na kitu kingine au laaa......akakata plastic lingine ni mafuta safi na litle anatumia hizi za maji ya uhai kupima litle moja.ni kweli wala hapunji ila bei ni hiyohiyo.ila najua pale kuna code imefungwa inatakiwa kufunguliwa kuna namna inatumika kupata faida angalau elfu kwa dumu.....kama kuna mtu anajua namna wanavyofanya ili kupata faida anijuze hapa nataka kuingia huku.nimesikia huyu mdau anauza hadi dumu 50 per day.......

Nimeamini mjini unatakiwa kuacha kupanic na kualaumu tu serikali bali unatakiwa kutumia akili nyingi uli uishi....
mbona umeshaambiwa faida yake ni ndoo zitakazoisha mafuta, kwamaana hiyo kama anauwezo wa kumaliza ndoo 50 kwa siku, hata akiuza ndoo moja tupu kwa 1000 atapata faida ya elfu 50. Ni parefu sana asee, nimejifunza kitu hapa.
 
Dogo anaeuza nilimrubuni akanipa namba nikampigia.nikamwambia nipe password ya hayo mafuta unapataje faida ?? Kasema bwana hapa katika lita 20 mimi natoa lita 22 kuna namna ya upimaji.wale wa robo robo huwa hazitimii ila lita moja inakuwa sawa.ila ile chupa kama inaonekana kama haipo sawa.

All in all wanategemea zile ndoo tupu waliuza ndio wanabutua.......
Hatimaye umesoma ule ukurasa ambao wengi wanauruka katika kitabu Cha mafanikio


Sahau pepo

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
mbona umeshaambiwa faida yake ni ndoo zitakazoisha mafuta, kwamaana hiyo kama anauwezo wa kumaliza ndoo 50 kwa siku, hata akiuza ndoo moja tupu kwa 1000 atapata faida ya elfu 50. Ni parefu sana asee, nimejifunza kitu hapa.
Kuuza ndoo za lita 20 ,50 si kaz ndogo. Hebu achen hesab za fesibuku jaman.. hamkui tu mpaka leo..
 
Unta
Biashara inahitaji Hesabu kali saaana, Kama kwa siku anauza dumu 50.
Bei ya kuuza kila dumu empty mfano ni 3,000 - 5,000 ukizidisha mara 50
Jamaa ana uhakika wa 150,000 - 250,000 kwa siku, Apo umetoa pembeni mtaji wake wa mafuta.
Unyama sana [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23
😆😆😆😆😆😆🙌
 
Kuuza ndoo za lita 20 ,50 si kaz ndogo. Hebu achen hesab za fesibuku jaman.. hamkui tu mpaka leo..
Ni kweli ila mpaka mtu kufanya hivyo inamaana ana uhakika wa sehemu pa kuzipeleka
 
Pamoja na njia zote hizo.kuna mtindo hiyo chupa wanayotumia kupimia wameieka kwenye moto kwa mbali..inabadili umbo maeneo ya chini na katikati ..ukitaka kuamini nenda na chupa yako waitumie hiyo kupimia lazma wakatae.siku chupa hizi za maji zinawekwa kwenye moto ili kuzibadili maumbo zinakuwa ndogo sio rahisi kujua mteja wa kawaida..
 
Kwamba wanauza dumu 50 za lita 20 kwa siku.?

Yaani wanauza lita 1000 kwa siku.?

Unamaanisha kila mtu akija kununua lita 1 tu. Wanauwezo wa kuhudumia watu 1000 kwa siku.?

Dah.! Wapewe hongera.
 
Kuuza ndoo za lita 20 ,50 si kaz ndogo. Hebu achen hesab za fesibuku jaman.. hamkui tu mpaka leo..
Tembea ujionee mzee baba.alafu kijiwe sio kimoja kuna vijiwe kama vitano hivi
 
Biashara ni akili tu..ni kama wale wauza mchele unaweza kuuzia mchele aina moja kwa bei tatu tofauti..wanaweka na bei kabisa pale juu...unaanza kudanganya macho yako.
Duh, kwa kweli Hamna mfanyabiashara wa kuiona pepo kwa mtindo huu
 
Back
Top Bottom