Watu wanne ambao unatakiwa kuwasamehe kwenye maisha yako

Watu wanne ambao unatakiwa kuwasamehe kwenye maisha yako

Silent King

Senior Member
Joined
Jul 17, 2026
Posts
163
Reaction score
366
Wa kwanza ni wazazi wako,
Yes wazazi wako,wazazi wetu kwa namna moja au nyingine kwenye makuzi yetu kuna mambo ambayo huenda sio kwa ubaya au bila wao wenyewe kujua,tunajikuta wametukwaza sana na kutuachia majeraha makubwa sana.

Tumekuwa tukiwalaumu,tukiwa chukia na saa nyingine kutopenda kuwa karibu nao. Lakini ifike kipindi tuwasamehe,haina faida yoyote kwa mustabali wa maisha yetu na afya zetu pia,tujue kwamba wewe unayeendelea kuwa na chuki ndio muathirika mkubwa sana au mhanga wa jambo hili,kwasababu huenda hao wazazi wako hata wahajui kama wamefanya jambo ambalo linawaumiza watoto wao,tafadhali tuwasamehe now baada ya kusoma chapisho hili,for your own good.

Wa pili,watu wote walio kukosea,nao pia wasamehe in the name of peace and love,unajua nini? Maisha ni mafupi kuweka kinyongo moyoni, maisha ni mafupi kujipa stress na jakamoyo.

Kumbuka kusamehe ni kwa faida yako mwenyewe,watu huwa hatujui,tunafikiri tusipo samehe basi tuna mpa adhabu yule ambaye hatumsamehe,in actual sense tunajipa adhabu wenyewe,tupindue meza sasa na kujipa amani na utulivu,na haya hutayapata kama unaruhusu negative energy kwenye nafsi yako

Wa tatu, kujisamehe mwenyewe,sometimes tunafanya upuuzi na ujinga,na kupelekea kujilaumu sana "kwanini nimetamka yale niliyotamka?" Au "lau ningenyamaza kimya wakati huenda yasingetokea haya"

Okay yametokea yaliyo tokea but you can not change that now,huwezi rudisha maneno mdomoni,but you can do one thing which brave people do,just forgive yourself, yes jisamehe mwenyewe,utapata amani moyoni.

Nne, kaombe msamaha kwa watu uliowakosea au mtu uliye mkosea,hii itakupa amani ya moyoni kwako,even a text message will do better

Wakati mwengine tunakatisha mahusiano na watu kwasababu tu ya mambo ambayo huenda tungeomba msamaha yangekuwa yamekwisha,na tukafanya mambo makubwa pamoja,tupekeana ramani na mambo yakaenda sawa

Maisha ni neema kubwa sana,hivyo tusiyachukulie poa

Silent king
 
Maisha ni mafupi sana kuyapoteza kwa kisasi. Samehe, acha yaliyopita yabaki nyuma, na endelea kuifuata ile ndoto nzuri uliyonayo moyoni.

Kisasi huendeleza ubaya, lakini msamaha huleta amani.

Usifanye kisasi kuwa sehemu ya kusudi lako maishani lenga kujijenga, kukua, na kuwa mtu bora kuliko yule aliyekuumiza.

Stay humble 😌
 
Maisha ni mafupi sana kuyapoteza kwa kisasi. Samehe, acha yaliyopita yabaki nyuma, na endelea kuifuata ile ndoto nzuri uliyonayo moyoni.

Kisasi huendeleza ubaya, lakini msamaha huleta amani.

Usifanye kisasi kuwa sehemu ya kusudi lako maishani lenga kujijenga, kukua, na kuwa mtu bora kuliko yule aliyekuumiza.

Stay humble 😌
Nimeipenda hii
 
Back
Top Bottom