Watu wapigwa na kuvuliwa nguo nyumbani kwa Wema Sepetu

TANMO

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2008
Posts
11,763
Reaction score
11,873
Nyumbani kwa muigizaji wa filamu, Wema Sepetu, kumetokea tukio la kushangaza la watu wawili wanaodaiwa kuwa mafundi, kupigwa na kudhalilishwa kwa kuachwa uchi wakidaiwa kuhusika na wizi.

Kwa mujibu wa Bongo5 ambao walizungumza jana na jirani wa Wema aliyetambulika kwa jina la Mama Steve, alisema tukio hilo lilitokea Ijumaa majira ya saa 5 asubuhi mpaka saa 9 jioni.

"Waliopigwa na kulazwa chini uchi wa mnyama ni mafundi ambao wanakujaga kila siku kumtengenezea Wema nyumba yake," amesema mama huyo. "Sasa baada ya kumaliza kazi yao wakaondoka, baada ya kuondoka wakaitwa tena na kuambiwa kuna simu imeibiwa ndani, ndo mtiti ukaanza."

"Petit akatumwa akachukue mabaunsa 7 na baada ya kufika wakapandisha muziki mpaka mwisho ili sisi tusisikie nini kinaendelea huko ndani. Sasa kuna mtu alikuwa anapita hapa kwenye geti lao akasikia mtu analia sana ikambidi akachungulie ndo akamkuta fundi watu wawili wamelazwa chini uchi wa mnyama wanapigwa na hawana nguvu kabisa!

Ndo yule jamaa kwakuwa alikuwa anamjua yule fundi akaita watu wakaanza kugonga geti ili wafungue lakini hawajafungua geti. Tukawa tunasikia sauti ya Wema ikisema ‘jamani waacheni hao mtawaua' lakini anasema hivyo wakati yeye inaonyesha ndo alikuwa kinara wa matukio hayo. Wema na ana roho ya kikatili sana. Amefanya matukio mengi lakini hivyo hapana! Yaani kama anataka usalama wake anatakiwa ahame vinginevyo vijana watamfanyika tukio la kinyama sana," ameongeza mama huyo.

"Baada ya watu kuwa wengi sana pale nje ndo geti likafunguliwa watu wakaingia na kuwachukua wale vijana wakiwa hawajitambui na wapo uchi ndo wakapelekwa hospitali. Sasa baada ya kupelekwa hospitali polisi wa kituo cha Mabatini na wao wakagonga geti wakawa hawataki kulifungua polisi wakapindukia na kuingia ndo wakawakamata baadhi ya watu na kuondoka nao. Hilo ndo tukio alilolifanya mwanadada wenu ambaye anadai alikuwa Miss Tanzania," alisema Mama Steve.

Pia shuhuda mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Mama Samira, alisema amesikitishwa na tukio hilo la kinyama. "Hii ni tabia yake, hata wafanyakazi wake wa ndani anao kaa nao saa zingine anawapiga makofi! Kwakuwa ni ndani kwa ndani sisi majirani hatufuatilii, lakini kwa hilo na sauti yake tumeisikia japo watu wake wanadai hakuwepo," alisema.

Kwa mujibu wa Bongo5, mjumbe wa nyumba kumi, Mwarami alithibitisha kutokea kwa tukio hilo huku akidai hataki kuliongelea sana kwakuwa limeshafika katika kituo cha polisi Mabatini.

Mkuu wa kituo cha polisi cha Mabatini hakupatikana ili kuthibitisha na kutujuza kile kinachoendelea katika sakata hili.
Mtu wa karibu wa Wema, Petit Man aliyetajwa kuhusika kwenye tukio hilo, aliiambia Bongo5 kuwa watu hao walipigwa lakini hawakuvuliwa nguo. "Yeah kuna tukio limetokea, lakini hakuna mtu aliyevuliwa nguo," alisema Petit na baada ya hapo alikata simu.

Habari kwa hisani ya Bongo 5
 
wema hana ustaarabu kabisaa.
Majirani washamchoka na tabia zake za kinyama.
Kuna siku nilisema hapa wema alisimama katikati ya mtaa akaanza kutukana majirani.
Watamfanya kitu kibaya asipobadilika.
Kama amedhurika hivi, halafu anajifanya ana roho nzuri mfyuuuuuuuu
 
mie nashangaa watu wanavyomuona innocent sana wkt c kweli
 
Mmmh huyo mama steve nae mpana...

Halafu unaweza kukuta mafundi wamelipwa kudundwa ili kurushwa kwenye in my shoes

Lakini kama ana kamkono kepesi ka kupika utamponza

Ila kama hao mafundi wanaume...halafu wamepigwa mpaka kuvuliwa nguo...... uanaume wao inabidi uchunguzwe zaidi
 
Nakwambia huyu dada nishamshuhudia akimfokea Mtu mzima Kama Mtoto kisa huo ucelebrity wake yaani akiwa nyuma ya camera ni Mtu mbaya sana.. Nashangaa hao wanaokaa kumsifia mkarimu na mpole.

Kwa kweli mimi nimemjua zaidi kwenye kile kipindi chake cha in my shoes,ni mbishi na mkorofi hapendi kukosolewa kabisa!
Mimi siwezi kuishi naye tungepigana hadharani!
 

Weka picha.
 
Huyo binti atakuja kufa kifo kibaya sana.

Na kama mmoja wao hao watu wanaodaiwa kupigwa ningekuwa mimi, basi ningemuwinda huyo Wema nimuue kikatili sana.

Yeye ni nani hadi awe anaamrisha watu wake wawapige watu wengine?

Kama hao jamaa hawatalipiza kisasi nitawaona wajinga kabisa.

Na ingekuwa ni mimi ningepigana mpaka mwisho. Siwezi kuruhusu kunyanyaswa na mtu mwingine.

Heri nife nikipigana kutetea utu wangu kuliko kukubali kupokea kichapo nikiwa nimejikunyata kwa woga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…