SI KWELI Watu wasio na Bandama hawawezi Kucheka

SI KWELI Watu wasio na Bandama hawawezi Kucheka

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Kumekuwepo na nadharia inayoaminika sana Mtaani kuwa mtu asiye na Bandama hawezi kucheka.

Binafsi kwanza sielewi bandama ni nini na linahusikaje na kucheka kwa binadamu.

IMG_7635.jpeg

Naomba kufahamu undani na ukweli wa jambo hili maana nimekuwa nasikia likiongelewa sana miaka nenda rudi.
 
Tunachokijua
Bandama ni kiungo kinachopatikana ndani ya mwili wa Binadamu. Muundo wa anatomia ya binadamu unataja kiungo hiki kuwepo upande wa ubavu wa kushoto, juu kidogo ya tumbo.

Hufahamika pia kama wengu au Spleen ambapo kwa mtu mzima huwa na uzito unaokadiriwa kufikia wastani wa gramu 139.

Historia ya Kitabibu kuhusu Bandama
Binadamu ameanza kuchunguza na kujifunza kazi ya kiungo hiki zaidi ya miaka 2500 iliyopita.

Mathalani, Hippocrates (460–375 BC) alifundisha kuwa bandama ni kiungo kinacho ondoa maji yaliyopo kwenye chakula kilichopo tumboni.

Aristotle (384–322 BC) aliamini kuwa Bandama halina kazi yoyote kwenye mwili wa Binadamu.

Aidha, Pliny, kwenye karne ya kwanza baada ya Kristu (AD) aliamini kiungo hili kilikuwa mzigo kwa watu wanaokimbia riadha, hivyo alishauri kiondolewe ili kasi ya kukimbia iongezeke huku Tabibu na Mwanafalsafa Galen (130–200 AD) akiamini kuwa Bandama ni “kiungo chenye fumbo kubwa”

Dhana ya Bandama na uhusiano wake na Kucheka
Baada ya Galen, nadharia ya Mwili na Uhusiano wa Rangi 4 za majimaji unaotoa iliibuka. Nadharia hii huitwa Humorism.

Bandama lilihusishwa kuwa chanzo cha kuondoa mojawapo ya rangi hizo ambayo ni nyeusi (Nyongo nyeusi), kitabibu ikiwa na maana ya kitu chochote kinachokufanya usiwe na nia au ari ya kucheka. Hivyo, kutokana na sifa hii, iliaminika kuwa mtu asiye na bandama hawezi kucheka kwa kuwa ndio kiungo pekee kilochotumika kutoa sumu zinazoufanya mwili usicheke/ukose furaha.

Dhana hii ilidumu kwa zaidi ya miaka 1000 hadi miaka ya 1900 ambapo mapinduzi makubwa ya kitafiti yalifanyika ambayo yalibadili mwelekeo mzima wa suala hili.

Watu wasio na Bandama hawawezi Kucheka?
Mwaka 1919, Utafiti wa DH Morris et al. wenye kichwa cha habari “The Importance of the Spleen in Resistance to Infection” ulibadili mtazamo wa kazi ya kiungo hili.

Utafiti huu ulibaini na kuthibitisha kazi muhimu ya Bandama katika kuusaidia mwili kupambana na magonjwa.

Hadi sasa, tafiti za afya zimebainisha kuwa kiungo hiki hufanya kazi zifuatazo;
  1. Kuhifadhi damu
  2. Kuchuja damu kwa kuondoa uchafu na mabaki ya chembe nyekundu zilizoharibika au kufa
  3. Kuzalisha chembe nyeupe za damu kwa ajili ya kinga ya mwili
  4. Kuweka sawa uwiano wa majimaji ya mwili
  5. Kuzalisha kingamwili
Aidha, JamiiForums imezungumza na Madaktari wa Binadamu na kupitia tafiti mbalimbali na afya ambapo imebaini kuwa madai ya Bandama kuhusika na kucheka hayana ukweli.

Kama tulivyobainisha huko juu, dhana hii ilivuma sana miaka ya zamani kutokana na kutokuwepo wa ujuzi mkubwa unaohusisha afya ya binadamu.

Madhara ya kuondoa Bandama
Binadamu anaweza kuendelea kuishi hata baada ya kuondolewa kwa bandama lake.

Hata hivyo, kwa kuwa kiungo hiki huuusika kwa kiwango kikubwa katika kusaidia kinga ya mwili, mhusika anaweza kupatwa na maambukizi ya mara kwa mara yanayosababishwa na vimelea vya magonywa hasa bakteria na virusi.

Changamoto zingine zinazoweza kutokea ni kuvimba kwa kongosho, ngiri kwenye eneo la upasuaji, kuganda kwa damu kwenye mshipa unaoelekea kweye ini na maambukizi kwenye mapafu hasa ikiwa utaratibu huu haufanyika vizuri.

JamiiForums imebaini kuwa hakuna madhara ya “kushindwa kucheka” kwa watu wanaoondolewa bandama.

Mtu ili aweze kucheka hutumia pumzi, ndio maana akicheka mbavu zinabana kwa kuwa misuli lazima isapoti.

Hivyo mtu ambaye ametolewa Bandama anakuwa na upungufu wa kiungo ambacho kipo sehemu hiyo, kwa maana hiyo mtu ambaye hana Bandama anaweza kucheka lakini anapofanya hivyo lazima kuna balansi fulani ataikosa.

Akitaka kucheka lazima atafute sapoti, ndio maana unaweza kukuta kuna mtu mwingine mwenye changamoto hiyo akicheka anaweza kuinama au anajishika kifua kwa mikono yake miwili ili kupata balansi.
Huo utafiti umeufanya kwa kuwatolea watu wangap bandama ndiyo uje hapa kutuambia!? Au umesoma yalioandikwa na ww ukaandika!?

Binafsi nimeshuhudia mjomba wangu akipoteza uwezo wa kucheka baada ya kutolewa bandama.


Alikuwa mcheshi na mchekaji mzuri lakin baada ya bandama kuondoka mpaka kesho hutabasamu tu ila kucheka hola
 
Huo utafiti umeufanya kwa kuwatolea watu wangap bandama ndiyo uje hapa kutuambia!? Au umesoma yalioandikwa na ww ukaandika!?

Binafsi nimeshuhudia mjomba wangu akipoteza uwezo wa kucheka baada ya kutolewa bandama.


Alikuwa mcheshi na mchekaji mzuri lakin baada ya bandama kuondoka mpaka kesho hutabasamu tu ila kucheka hola
Usikute anajizuia kucheka ili kupunguza maumivu ya kutolewa bandama lake..
 
Back
Top Bottom