Kama ni kweli Serikali imetumia usalama kugushi makaratasi ya uchaguzi, kupanga matokeo ya uchaguzi Tanzania nzima na kufilisi wapinzani wafanyabiashara na hata kuwajeruhi au kushiriki kwa namna yeyote kwenye mauaji ya wapinzani ni tishio kubwa sio tu kwasasa lakini kwa miaka mingi sana ijayo.
Tatizo kubwa kuna watu wanafikiri hili ni jambo la mpito tu lakini ukweli ni kwamba usalama wa taifa umejipa kazi isiyo ya kwao. Hiki kitengo hakitakuwa cha awamu moja maana ukisha onjesha madaraka makubwa hivi kwa idara moja haina tofauti sana na nchi kutawaliwa kijeshi.
Je, hii ina maana gani? Hii ina maana kwamba usalama unakuwa na nguvu kuliko Wananchi hivyo hakutakuwa na sababu ya Wagombea wa nafasi tofauti kuwafuata wananchi badala yake wanaweza kuwafuata viongozi wa chama na usalama pekee kwani ndiyo wachaguaji wa ukweli sio wananchi. Lakini la pili kwenye hili ni kwamba usalama utakuwa na nguvu ya kutishia bunge zima hadi Mawaziri.
Kwa wale washabiki hasa wenye elimu inaelekea wanashabikia kitu ambacho hawajui au wamejidanganya kwasababu tu wanampenda Magufuli na mambo anayofanya. Hili sio sawa maana bila mfumo mzuri wa kidemokrasia tunaweza kuwa na Raisi mbaya na hatutaweza kumtoa kwa namna yeyote. Lakini vilevile unaweza ukawa na viongozi wabaya usalama wenye malengo binafsi na wakamtisha mpaka raisi wa nchi maana serikali imewapa vitu na uwezo ambao hawatakiwi kuwa nao. Hatuwezi kukaa na kusali tu nkwamba kila siku tutapata watu bora kwenye hizi idara au hata Uraisi hivyo mnaoshangilia sana mjue mabadiliko haya makubwa inawezekana kabisa akapewa kiongozi ambaye si mzalendo na nchi yetu inaweza kurudi nyuma kwa miaka mingi bila na kuwa na sheria yeyote ya kumtoa.
Umri wa kati wa Watanzania ni miaka 17-18 tu hivyo Tanzania ina watoto wengi ambao hawawezi kugoma, kuandamana wala kuelewa mambo mengi kwa upana na wale wachache wanaoelewa wamekuwa vipofu kwa manufaa binafsi au kwa mapenzi yao. Binadamu ni kama maua yenye harufu nzuri mwisho wake yanaharibika hata yawe mazuri vipi. Hii ndiyo sababu pekee pamoja na mapenzi yangu binafsi kwa Magufuli jinsi alivyobadilisha siasa hasa kwa upinzani na CCM ilivyoshinda kwa kutumia usalama imeweka pengo kubwa ambalo itakuwa ngumu kuziba.