Noel france
JF-Expert Member
- Oct 8, 2012
- 1,104
- 917
Habari wanajukwaa!
Kiukweli uchaguzi wa mwaka huu ni wenye ushindani mkubwa sana, kwa pande zote.
Kwa upande wa chama tawala, turufu yao kuu ni ununuaji wa ndege, ujenzi wa miundombinu mbalimbali, pia kuleta mabadiliko ya kiuongozi ndani ya taasisi za serikali.
Kwa mfano: Katika baadhi ya taasisi za serikali hakuna ama zimepungua majigambo ambayo yalikuwa kero katika maofisi.
Lakini pia imeleta hofu kwa watumishi, kwa sababu ya kuogopana.
Vitu ambavyo vitaipelekea chama tawala kupoteza katika uchaguzi huu ni pamoja na:
1) Hofu kwa wananchi juu ya watu wasiojulikana.
2) Utawala usioheshimu utawala wa sheria.
3) Wateule kujiona miungu watu N.K
Kwa upande wa upinzani especially CHADEMA wana nafasi kubwa ya kuweza kuthubutu kuchukua nchi upande wa Tanzania bara, lakini pia kwa upande ACT wazalendo vivyohivyo wana nafasi kubwa ya kutawala katika uchaguzi wa mwaka huu haswa kwa upande wa Visiwani.
Vitu pekee vitokavyo vibeba vyama vya upinzani ni madhaifu na mapungufu yaliyojitokeza katika utawala wa sasa pia wananchi walio wengi kutaka kuona mabadiliko ya kiongozi na kimfumo.
Pia, kutakuwepo na kura ya huruma kwa mgombea aliyenusurika na kifo.
Pia viongozi wote wa upinzani wameonesha Uzalendo wao uliotukuka macho mwa wapiga kura wao na wanachama wao.
Pia kitu chaziada kitakacho wabeba wapinzani ni kule kutakwa kuonwa na kusikilizwa wao baada ya kufungiwa kwa muda mrefu kwenye majukwaa ya kisiasa.
Je, wewe mtazamo wako ni upi? Naomba kuwasilisha hoja.