Watu wasiojulikana wanafanya kile kile walichokuwa wanafanya Interahamwe wa Rwanda

Watu wasiojulikana wanafanya kile kile walichokuwa wanafanya Interahamwe wa Rwanda

Mpigania uhuru wa pili

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2023
Posts
3,380
Reaction score
6,376
Baada ya Juvénal Habyarimana aliyekua Rais wa rwanda kuingia madarakani kupitia mapinduzi mwaka 1973 kwa kumpindua Grégoire Kayibanda kutokana na hofu aliyokua nayo dhidi ya madui zake ilibidi aanzishe kikundi kinachoitwa interahamwe hiki kikundi cha kihutu kilikua na lengo la kufanya kazi chafu ni tofauti na jeshi la rwanda na hii ilitokana na uhasama wa wahutu wa kaskazini na kusini mwa rwanda walikuwa hawapatani

Interahamwe Walikua na kazi zifuatazo;-
  • Kuteka watusi na wahutu wenye msimamo wa kawaida wengine walirudishwa ila wengine waliuwawa
  • Kuwasighulikia wale wanaoikosoa serekali
  • Kuiba kura Juvénal Habyarimana alikua anashinda kwa asilimia 95 na kuendelea kwenye kila chaguzi
  • Kufanya kazi chafu za serekali ambazo kikawaida hawawezi kuzifanya kupitia taasisi zake
  • Kuhakikisha watu wanakuwa wazalendo kwa nchi ya rwanda na kuwashughulikia wale wasaliti
Mwishoni mwa miaka ya 1980's Interahamwe walipishana na Rais Juvénal Habyarimana juu ya mambo tofauti tofauti ikiwemo mazungumzo ya aman kati serekali ya rwanda na RPF ya kina kagame waliko uganda na inaaminika interahamwe ndo waliolipua ndege ya Juvénal Habyarimana baada ya kumuona kama msaliti japokua hili swala ni debate

Kwa Tanzania Watu wasiojulikana a.k.a Interahamwe walipata nguvu sana kipindi cha utawala wa magufuli walikuwepo huko nyuma ila hawakua na nguvu sana katika legacy mojawapo za hovyo za utawala wa magufuli ni kuacha kikundi cha watu wasiojulikana

Utawala wa samia mwanzon alitaka kuwapotezea ila baadae akagundua bado anawahitaji sana ila wamsaidie yeye kusalia madarakani

Watu wasiojulikana wana-nguvu zaidi ya mahakama na taasis za serekali kwa lugha nyingine wako juu ya sheria madhara ya hiki kikundi yanaweza yasionekane leo ila hawa ndo watakao iondoa ccm madarakani kama ilivyotokea kwa Interahamwe na serekali ya Juvénal Habyarimana kupishana na matokeo yake nchi kuangukia mikononi mwa RPF

Kwa Tanzanaia kuanzia kipindi cha magufuli mpaka sahivi ni ngumu sana kwa Rais yeyote wa ccm kuongoza nchi bila kuwatumia hawa watu wasiojulikana a.k.a Interahamwe sababu kwa miaka 60+ya utawala wa ccm nchi iko kwenye umaskini sasa hakuna cha kuonyesha kwa wananchi kilichobaki ni kutumia nguvu na mabavu kuongoza nchi-

Kazi za watu wasiojulikana a.k.a Interahamwe wa tanzania ambao ni wanajeshi, usalama wa taifa na mapolisi
  • Kuteka, kutesa na hata kuua watu ambao wanaonekana kuwa tushio kwa serekali
  • Kuteka, kutesa hata kuua watu ambao wanaikosoa serekali
  • Kuiba kura kwenye chaguzi
  • Wanafanya kazi kama task force kwa ajili ya kukusanya kodi kwa lazima
  • Wanawatishia wafanya biashara na watu wenye ukwasi kuchangia ccm kwa lazima
  • Wanafanya biashra za magendo kama nchi mojawapo ya njia ya serekali kupata mapato ni kupitia biashara za magendo mfano kusafirisha watu, kutumia passport za kibalozi kusafirisha madawa ya kulevya
  • Waekezaji wakubwa lazima wapitie kwao ndo maana watu wasiojulikana ni matajiri sana
  • Kununua wale wanasiasa waupinzani maarufu kama njia ya kuwanyamazisha
Kwa sasa hivi nchi inaongozwa na matakwa ya watu wasiojulikana na sio katiba na taasisi zilizopo

Kiongozi wa watu wasiojulikana kwa sahivi ni ABDUL mtoto wa rais aliyeko madarakani
 
Tuliambiwa na machadema na wahuni toka ccm kwamba jiwe ndio alikuwa mtekaji!
Miaka 3 sasa imepita toka jpm afariki ila bado watu wantekwa mbele ya chura kiziwi anaeupiga mwingi na kufungua nchi
Yeye ndo aliyewapa nguvu watu wasiojulikana kwa lugha nyingine ni moja ya legacy ya magufuli
 
Japokuwa bandiko lako umeliandika Kama kwa hasira lakini Kuna ukweli mchungu usiopingika. Aidha, hata Precedent Case uliyotumia iko relevant haswaa na Visa vya matukio vinavyoendelea hapa Tanzania.
 
Uelewa huru:-

Wanamchafua mtia Nia wa urais mapema kabisa Ili wapate uhalali na sababu za kumuondoa na kumkosanisha na wananchi!

Rais anaewania awamu ya pili anafanya Ili apendwe na raia wake achaguliwe tena,ukiona TU Rais anaewania upili utawala wake unahusishwa na kupotea watu na teka teka ujue system haimtaki apate muhula wa pili!

Fikra huru tu za mlipa kodi!
 
Uelewa huru:-

Wanamchafua mtia Nia wa urais mapema kabisa Ili wapate uhalali na sababu za kumuondoa na kumkosanisha na wananchi!

Rais anaewania awamu ya pili anafanya Ili apendwe na raia wake achaguliwe tena,ukiona TU Rais anaewania upili utawala wake unagusishwa na kupotea watu na teka teka ujue system haimtaki apate muhula wa pili!

Fikra huru tu za mlipa kodi!
Kama kweli hawamtaki ni vyema wakam-face mhusika face to face na wamweleze ukweli ili asiendelee na Nia yake hiyo aliyonayo kuliko kufanya vitendo viovu vya 'kuhubiria chuki' dhidi ya Raia wa kawaida.

Wamfuate na wamweleze ukweli kinagaubaga bila kumuogopa, hata Mamlaka za Ujasusi za nchini Ufaransa waliwahi kufanya hivyo kwa aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Bw. Francois Hollander, Rais huyo wa wakati huo aliwaelewa na alikubaliana nao japo kwa shingo upande. Rais huyo Hakugombea mhula wa Pili kama alivyotaka na badala yake akatangaza kutengua/kufuta azma yake hiyo ya kugombea Urais kwa Mara ya Pili.
 
Kama kweli hawamtaki ni vyema wakam-face mhusika face to face na wamweleze ukweli ili asiendelee na Nia yake hiyo aliyonayo kuliko kufanya vitendo viovu vya 'kuhubiria chuki' dhidi ya Raia wa kawaida.
Wamfuate na wamweleze ukweli kinagaubaga bila kumuogopa, hata Mamlaka za Ujasusi za nchini Ufaransa waliwahi kufanya hivyo kwa aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Bw. Francois Hollander, Rais huyo wa wakati huo aliwaelewa na alikubaliana nao japo kwa shingo upande. Rais huyo Hakugombea mhula wa Pili kama alivyotaka na badala yake akatangaza kutengua/kufuta azma yake hiyo ya kugombea Urais kwa Mara ya Pili
Afrika haijafilia hiyo level au hiko kiwango cha ustaarabu madaraka yalivyokua matamu unategemea Rais ayaachie kirahis rahisi
 
Tuliambiwa na machadema na wahuni toka ccm kwamba jiwe ndio alikuwa mtekaji!
Miaka 3 sasa imepita toka jpm afariki ila bado watu wantekwa mbele ya chura kiziwi anaeupiga mwingi na kufungua nchi
Umeambiwa hao watekaji walipata nguvu sana wakati wa Magufuli, na Samia alitaka kuwapotezea, ila ameona anawahitaji bado.
 
Kama kweli hawamtaki ni vyema wakam-face mhusika face to face na wamweleze ukweli ili asiendelee na Nia yake hiyo aliyonayo kuliko kufanya vitendo viovu vya 'kuhubiria chuki' dhidi ya Raia wa kawaida.
Wamfuate na wamweleze ukweli kinagaubaga bila kumuogopa, hata Mamlaka za Ujasusi za nchini Ufaransa waliwahi kufanya hivyo kwa aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Bw. Francois Hollander, Rais huyo wa wakati huo aliwaelewa na alikubaliana nao japo kwa shingo upande. Rais huyo Hakugombea mhula wa Pili kama alivyotaka na badala yake akatangaza kutengua/kufuta azma yake hiyo ya kugombea Urais kwa Mara ya Pili
Mtego wa katiba mbovu unamfanya mtia Nia kuwa Mungu kwao na kuogopa kumwambia ukweli!

Binafsi nilikua na matumaini Dana na mama kuhusu katiba mpya na nilidhani atatupa katiba halafu yeye atajiondoa kutia Nia,Cha ajabu akaambukizwa ule ugonjwa wa kiafrika ule!

Katiba mbovu hii namna ya ku I handle imeumiza watu sana Kwa miaka mingi!
 
Back
Top Bottom