Etugrul Bey
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 6,514
- 15,247
Huyu ni mtu ambaye anakusaidia wakati yeye mwenyewe anataka msaada,yani kuna watu ambao wao wenyewe hali zao ni za mashaka lakini bado wana moyo wa kutoa,kama wewe ni mmoja wapo ubarikiwe sana
Mtu ambaye anawapuuza watu wengine kwa ajili yako,yani watu wengine wanampa maneno ya uchochezi au fitina juu yako lakini bado anaziba masikio na bado yupo na wewe,big up sana kwa boss wangu mpya licha ya kwamba boss wangu wa zamani alitia fitina juu yangu,lkn my new boss kwakuwa ananijua vyema ameniamini na tunapambana pamoja
Mtu ambaye anakupa mda kusikiliza shida zako,yupo tayar mda wowote kukusikiliza bila kuchoka,na anatunza siri zako
Mtu ambaye haonyeshi kuchoka kwa tabia zako mbaya,pamoja na tabia zako mbovu lkn yupo pamoja na wewe
Na mtu ambaye anaonyesha dhahiri furaha yake kwako
Namalizia kwa kusema maisha hayakupi mtu mmoja mara mbili
Kwa nyuzi za motivation basi usikose kunisoma,nipo kwa ajili yako
Ni hayo tu!