Watu watano wafariki dunia baada ya Lori kufeli breki kwenye mlima Mbalizi, Mbeya

Juzi pale mikumi, Morogoro, Lori limefeli brake na kuingia ndani ya nyumba iliyoko pembeni mwa barabara na kuuwa mtu mmoja..
Haya maisha ya duniani tunaishi lakini hatujui ni lini tutaondoka ,na kifo kinakuja kwa njia mbalimbali cha msingi ni kuomba mungu atujalie afya njema,unaweza ukajiwekea ulinzi na usalama wa kila namna kwa gharama zozote na za juu mwisho wa siku, ukaondoka
 
Hi
Hiv Huyu Kamanda kashasttafu mana ç'i msikii tena
 
Serikali inashauriwa KILA siku ule mpando wa mbalizi utamaliza watu pale iwe one way pekee na sio two way. Malori kufeli brake ni wimbo wa taifa pale
 
Wataalamu wa mechanics hivi Hakuna namna ya kulock tairi za tela zisizunguke pindi brake inapofeli. Au tairi za nyuma za kichwa zisizunguke Ili gari isiende mbele?
 
Serikali inashauriwa KILA siku ule mpando wa mbalizi utamaliza watu pale iwe one way pekee na sio two way. Malori kufeli brake ni wimbo wa taifa pale

Nadhani pale serikali imeamua wananchi wake wafage tuuu!
 
Wataalamu wa mechanics hivi Hakuna namna ya kulock tairi za tela zisizunguke pindi brake inapofeli. Au tairi za nyuma za kichwa zisizunguke Ili gari isiende mbele?

Ishuke pekee au ipande pekee
 
Imezoeleka kila mwisho wa mwaka ndipo jeshi la polisi linakuja na hamsha hamsha kusimamia usalama barabarani, ikiwa ni pamoja na kufuatilia mabasi ambayo imeonekana ndiyo chanzo kikubwa cha ajali.

Miezi kadhaa sasa ajali zimeongozana na baadhi ya hizo zimeshuhudiwa zikitokana na maroli au waendesha pikipiki a.k.a bodaboda.

Kwa wiki hii iliyoisha mpaka leo jumatatu ni ajali kama nne zimetokea na kuleta madhira kwa jamii.

Najiuliza, kwa nini hali hii, nikikumbuka kipindi fulani huko nyuma wakati kama huu iliwahi kutokea ajali mbaya na watu kufa.
 
R.I.P Mwl John,alikuwapo ajali Hio.

Mke wake alikufa mwaka Jana akijifungua,akamwachia kichanga...dah nae ametembea.

Huruma sana kwa watoto.
 
Mungu asante kwa kumlinda Mchungaji Mwamluku na wengine waliopona katika ajali hii. Mtumishi huyu anachunga kanisa la TAG Isamilo Jijini Mwanza.
 
Ule utaratibu wao wa malori na gari ndogo kupita kwa zamu uliishia wapi??
Lile zoezi wangelisimamia vizuri lingesaidia sana kupunguza ajali mlima mbalizi.

Tatizo ni pale gari kubwa bado hazijamaliza kushuka kutoka iwambi na kule mbalizi washaruhusu gari ndogo zianze kupanda.
Workdone inakuwa sawa na sifuri.


Timing inakosekana.
Wangepiga hesabu za muda vizuri kwamba tukiruhusu hizi gari kushuka basi zitachukua muda fulani kumalizika..
Lakini utashangaa wanaangalia tu baada ya nusu saa wanaruhusu gari ndogo zianze kushuka na kupanda.
Matokeo yake zile gari ndogo zinatokea kule chini Mbalizi kwa pupa zinakutana na Malori yaliyotoka Iwambi bado hayajamalizika na baadhi ya Lori pia zinakuwa hazimaliza kupanda .. matokeo yake ni ajali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…