Watu watatu wakamatwa kwa wizi wa miundombinu ya mradi wa maji Nzega

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Vyombo vya dola wilaya ya Nzega mkoa wa Tabora vinawashikilia watu watatu kwa tuhuma za kuiba miundombinu ya mradi wa maji ikiwemo mabomba ya maji, katika mradi wa maji unaotekelezwa Kata ya Sigili wilaya ya Nzega, mkoani Tabora hali inayosababisha kusuasua kwa mradi huo.

Taarifa ya wizi wa miundombinu hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Nzega, Naitapwaki Tukai katika ziara ya uzinduzi na uwekaji wa jiwe la msingi la mradi wa maji kwa vijiji vya Lyamalagwa, Bulende na Bulambuka vya kata ya Sigili, unaotekelezwa na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya maji kwa wilaya ya Nzega.

Hayo mabomba wakiiba wanapeleka wapi.
 
Back
Top Bottom