Nyakijooga
JF-Expert Member
- Dec 9, 2018
- 276
- 473
Kariakoo (Dar) kwa siku za hivi karibuni kumeibuka wimbi la kubwa la biashara ya simu zilizopachikwa jina kama 'Simu za Mtumba' ambazo uuzwa kwa bei nafuu, simu hizo ni za 'brand' mbalimbali nisingependa kuyataja hapa.
Udadisi nilioufanya kwa miezi kadhaa ambayo nimekuwepo Kariakoo nimegundua kuna kilio kikubwa na maumivu kwa baadhi ya Watu ambao uuziwa simu hizo.
Ukikatiza Kariakoo hususani Mtaa wa Msimbazi au eneo la China Plaza utakutana na Vijana wakiuza simu hizo kwenye maeneo ya fremu kama ilivyo kawaida kwa simu nyingine.
Ikitokea amejitokeza mnunuzi anaambiwa kwamba simu hizo ni za mtumba, hivyo inauzwa mikononi bila kuwa viambatanishi vyovyote, ikiwemo kufungwa kwenye box na vifaa vyake kama ilivyozoeleka kwenye utaratibu wa kuuziana simu nyingine mpya.
Pia soma: Hivi TBS inafanya kazi gani kama Wafanyabiashara wanaingiza 'Bidhaa Fake' na kutangaza waziwazi, iPhone 15 Tsh. 380,000?
Hata hivyo, pia uuzwaji wa simu hizo unafanyika kwa wingi bila kutoa risiti kwa wanunuzi huku wauzaji wengi wakitumia kauli kuwa zinauzwa bei pungufu ndio maana hawatoi risiti, wamekuwa wakidai mbele ya wanunuzi kuwa ni simu ni 'original za mtumba' hivyo hakuna ulazima wa risiti.
Hali ya kusikitisha baadhi ya watu ambao ununua simu za aina hiyo, wengi wamebakia kujifuta machozi hasa zinapopatwa na matatizo siku chache baada ya kununua, ikiwemo simu kuzimika au kupata changamoto nyingine za kimfumo (setting)
Ambapo imekuwa vigumu kwa wengi wao kuzirejesha madukani, baadhi ya waliodhubutu kufanya hivyo wanaambiwa hizo ni simu za mtumba ukinunua umenunua, ikipata changamoto hawawajibiki. Ni kwamba hazina hata waranti, mnunuzi anashindwa kudai kwa sababu anakuwa hana risiti.
Inaelezwa kwamba kuna Mtandao wa Watu wakubwa ambao uingiza simu hizo sokoni na kuzisambaza kwa baadhi ya Wafanyabiashara Kariakoo ambao nao uwapatia vijana maarufu kwa jina 'mawinga' au ‘vijana wa madili' ili kufanya mauzo na kupata asilimia kadhaa sawa na makubaliano.
Watu wameumizwa na simu hizo bila kupata msaada, nitoe wito kwa mamlaka zifuatilie hili suala maana watu wengi wamepigwa kwa kuuziwa simu mbovu kwa kigezo kuwa ni simu za mtumba.
Ni vyema Mamlaka zifuatilie uungizwaji wa simu hizo ambazo kwa asilimia kubwa baada ya kuwa mkombozi kwa wananchi zinaongeza maumivu kutokana na utapeli wa kuziuza kwa bei rahisi mfano Sh 70,000 hadi Sh 200,000
Licha ya bei kuwa zaidi ya hapo lakini wastani mkubwa wa wanaokumbana na changamoto hiyo ni wanaouziwa simu kwa bei hizo.
Ni vyema ikajulikana nani yupo nyuma ya mtandao huo na kama anavyo vibali vya kuingiza na kuuza simu hizo pamoja na namna anavyowajibika sokoni.