DOKEZO Watu wawe makini na Mtandao wa 'Simu za Mtumba' Kariakoo

DOKEZO Watu wawe makini na Mtandao wa 'Simu za Mtumba' Kariakoo

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Ni kweli kabisa, hizo simu nyingi huvuki 2 month. Ni biashara inaonrkana halali sababu ya mafrem na wanavyo zibrand ila wezi wakubwa.

Msinunue hizo simu za mtumba mtalia.
 
Kariakoo (Dar) kwa siku za hivi karibuni kumeibuka wimbi la kubwa la biashara ya simu zilizopachikwa jina kama 'Simu za Mtumba' ambazo uuzwa kwa bei nafuu, simu hizo ni za 'brand' mbalimbali nisingependa kuyataja hapa.

Udadisi nilioufanya kwa miezi kadhaa ambayo nimekuwepo Kariakoo nimegundua kuna kilio kikubwa na maumivu kwa baadhi ya Watu ambao uuziwa simu hizo.

Ukikatiza Kariakoo hususani Mtaa wa Msimbazi au eneo la China Plaza utakutana na Vijana wakiuza simu hizo kwenye maeneo ya fremu kama ilivyo kawaida kwa simu nyingine.

Ikitokea amejitokeza mnunuzi anaambiwa kwamba simu hizo ni za mtumba, hivyo inauzwa mikononi bila kuwa viambatanishi vyovyote, ikiwemo kufungwa kwenye box na vifaa vyake kama ilivyozoeleka kwenye utaratibu wa kuuziana simu nyingine mpya.

Pia soma: Hivi TBS inafanya kazi gani kama Wafanyabiashara wanaingiza 'Bidhaa Fake' na kutangaza waziwazi, iPhone 15 Tsh. 380,000?

Hata hivyo, pia uuzwaji wa simu hizo unafanyika kwa wingi bila kutoa risiti kwa wanunuzi huku wauzaji wengi wakitumia kauli kuwa zinauzwa bei pungufu ndio maana hawatoi risiti, wamekuwa wakidai mbele ya wanunuzi kuwa ni simu ni 'original za mtumba' hivyo hakuna ulazima wa risiti.

Hali ya kusikitisha baadhi ya watu ambao ununua simu za aina hiyo, wengi wamebakia kujifuta machozi hasa zinapopatwa na matatizo siku chache baada ya kununua, ikiwemo simu kuzimika au kupata changamoto nyingine za kimfumo (setting)

Ambapo imekuwa vigumu kwa wengi wao kuzirejesha madukani, baadhi ya waliodhubutu kufanya hivyo wanaambiwa hizo ni simu za mtumba ukinunua umenunua, ikipata changamoto hawawajibiki. Ni kwamba hazina hata waranti, mnunuzi anashindwa kudai kwa sababu anakuwa hana risiti.

Inaelezwa kwamba kuna Mtandao wa Watu wakubwa ambao uingiza simu hizo sokoni na kuzisambaza kwa baadhi ya Wafanyabiashara Kariakoo ambao nao uwapatia vijana maarufu kwa jina 'mawinga' au ‘vijana wa madili' ili kufanya mauzo na kupata asilimia kadhaa sawa na makubaliano.

Watu wameumizwa na simu hizo bila kupata msaada, nitoe wito kwa mamlaka zifuatilie hili suala maana watu wengi wamepigwa kwa kuuziwa simu mbovu kwa kigezo kuwa ni simu za mtumba.

Ni vyema Mamlaka zifuatilie uungizwaji wa simu hizo ambazo kwa asilimia kubwa baada ya kuwa mkombozi kwa wananchi zinaongeza maumivu kutokana na utapeli wa kuziuza kwa bei rahisi mfano Sh 70,000 hadi Sh 200,000

Licha ya bei kuwa zaidi ya hapo lakini wastani mkubwa wa wanaokumbana na changamoto hiyo ni wanaouziwa simu kwa bei hizo.

Ni vyema ikajulikana nani yupo nyuma ya mtandao huo na kama anavyo vibali vya kuingiza na kuuza simu hizo pamoja na namna anavyowajibika sokoni.
Dah mm mpaka sasa nazungushwa niliuziwa simu kioo kibovu mwenye duka anadai niongeze ela nipewe simu nyingne
 
Wapumbavu wacha wabamizwe tu wabongo wengi wanapenda kitonga sana ndio mana wanaliwa vichwa sana
 
Bora ununue simu mtumba uishie kupata hasara ya simu kuharibika kuliko kununua simu mtumba kisha uje kukamatwa uambiwe hiyo simu iliibiwa kwa marahemu Arusha siku alipouliwa na majambazi. Utajua kama hujui
Kesi yake ndogo hyo.

Utaambiwa kuna mwanajeshi kauwawa huko hii sim ndyo aliyo kuwa akitumia marehemu.
 
Boxer mtumba, Shati mtumba, jinzi mtumba sasa mpaka simu tena Mtumba khaa...
 
Kuna Watanzania wana nyodo sana hadi wanakera. Hela hawana ila demands za kikuda kabisa. Mfano kuna wabongo njaa wanataka nao kumiliki Samsung Note 10+ hii ipo ya kioo kidogo isiyo full display na ya ile yenyewe original screen panel na tofauti ya bei wastani ni 180,000.

Sasa mtu anakuja na laki nne na nusu anataka Note 10+ hiyo unauziwa na babako???

Kwa taarifa yako watu hawataacha kununua simu used. Samsung S series mpya ni S24 pekee, Pixel series mpya ni 8 na 9, iPhones mpya ni 15 na 14 chache mno. Sasa ni kila mtu ana hela ya kuzinunua?

Na kila bidhaa used inakuwa na some risks za kuwa na shida, kwanini Apple watoe limited warranty? Kwanini Samsung watoe 2 years warranty. So baada ya miaka miwili, hiyo S22 Plus au Ultra unayonunua bongo ikiwa used nani anacover warranty yake. Na je umelipia premium price?
Ununue gari used Japan lifike ulalamike fuel consumption ni kubwa kuliko as advertised sasa si ni used hiyo chances za kuwa na kasoro ndogondogo zipo.

Na kama mnataka warranty lipa bei ya warranty. Unataka friji upewe warranty ya mwaka na unatoa laki nne.
Mnawajua licenced dealers wa hizo brands walipo nenda pale ukauziwe simu ya 400,000 kwa bei yao ya 600,000 na utakuwa na uhakika na warranty. Umetoka na makanyagio yako umeenda Kariakoo na laki tatu zimechakaa unataka upate after sales service sawa na aliyenunua bidhaa ileile kwa 550k kwa official dealer?

Mfanyabiashara yeyote anaangalia mteja anataka nini, wateja wengi bongo wanataka bei ndogo (wanaita kitonga, neno linakera hata kutamka). Sasa wapi uliona bidhaa ya bei ndogo ikawa na ubora mkubwa? Kelele zote hizi hutoona official dealers wamejaza wateja madukani, watu wataishia Kariakoo kufuata bei wanazomudu. Mfanyabiashara akileta bidhaa bora ambayo ananunua bei kubwa na kuuza bei kubwa raia hawaelewi.
Umenena Kwa hasira sana, atakaye elewa na aelewe
 
Wewe umeongelea mambo ya kawaida ya kibiashara, lakini mleta mada kazungumzia utapeli zaidi.
 
Sim sio kitu cha kununua mtumbani believe me. Kama kuna mtu mwenye mentality hii hapa jf aiondoe. Sasahiv watu wnaoongoza kwenda gereji ni wamiliki s10 au s10+ used. Na mpaka spea zake kariakoo zimekuwa scarce kwelikweli mana demand yake sio poa
Kwa namna wabongo wanapenda cheap, sidhan kama watakuelewa
 
Kuna mwaka kuna vijana kama wanne walikuwaga wanashinda sana hapo China Plaza walipotea kipindi kama hichi cha kufunga mwaka… nakumbuka ilikuwa 2020 au 2021 kama sikosei. Inasemekana walikuwa kwenye huu mtandao wa utapeli wa simu za wizi na biashara zinginezo za haramu wanajihusisha nazo.

Naona wameanza tena… Waache!
 
Kaa kimya
 
Back
Top Bottom