Watu wawili wafariki kwa mlipuko katika Godauni la Kiwanda cha Sukari cha Mtibwa, Morogoro

Watu wawili wafariki kwa mlipuko katika Godauni la Kiwanda cha Sukari cha Mtibwa, Morogoro

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
525
Reaction score
1,257
Watu wawili wamefariki Dunia baada ya kutokea mlipuko katika godaoni la Kiwanda cha Sukari Mtibwa.
Lakini hadi sasa viongozi wa serikali na kiwanda wamegoma kuzungumzia chochote kuhusiana na tukio hilo lakini Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro imekiri kupokea maiti mbili za watu waliofariki Dunia katika tukio hilo.

Waandishi wa habari wa wamefika katika eneo la tukio ili kufuatilia tukio hilo lakini wamekutana na ulinzi mkali.

===========
Updates

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Alex Mukama amesema:

"Chanzo cha vifo hivyo ni mlipuko ambao bado hatujajua umesababishwa na nini, wataalam wanaendelea na uchunguzi, sehemu ya tukio kulikuwa na moto lakini umedhibitiwa, majeruhi pia wamepelekwa hospitali, bado sijajua idadi kamili kwa kuwa nipo sehemu ya tukio."
 
Sio hydrogen peroxide maana ina tabia ya kulipuka
 
Back
Top Bottom