Watu wema bado wapo

Watu wema bado wapo

Dr leader

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2016
Posts
893
Reaction score
1,021
WEMA BADO WAPO

1. Nilipo pata ajali, ndipo nilipofahamu
Wachache wanaojali, tena wasonifahamu
Jaribu ni ja jabali, lahitaji utimamu
Watu wema bado wapo

2. Walojidai mapenzi, tele ningali mzima
Hakuna wakunienzi, kuutuliza mtima
Nilipouona mwezi, nilihimidi karima
watu wema bado wapo

3. Akufaaye kwa dhiki, ja wasemavyo wahenga
Huyo ni mbora rafiki, dawamu hatokutenga
Hajifichi mnafiki, huyo ni kama kinyonga
watu wema bado wapo
 
Back
Top Bottom