Watu wengi hawajui kikosi cha mizinga na nako 2 nako waliwahi kuwa na bifu kali kupelekea hadi kuumizana vibaya

Stability

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2020
Posts
822
Reaction score
2,966
Bou Nako, mmoja wa waanzilishi wa Nako 2 Nako, alikuwa moja ya walengwa wakuu katika beef hiyo kubwa.

Kuna hadithi kwamba aliumizwa vibaya sana wakati wa shambulio lililohusishwa na upande wa Kikosi cha Mizinga, na ilisemekana kuwa karibu na kifo. Haruna Moshi “Boban” aliripotiwa kumsaidia kuokoa maisha yake wakati huo.

Pia kuna wakati Nako 2 Nako walikodi kosta na washkaji zao kutoka Arusha hadi Dar kwenda kuwashambulia kikosi, na walikuta mbwa wa ulinzi wa mmoja wa vijana wa kikosi cha mizinga na wakaamchoma visu na kumuua.
 
Hao Kikosi cha Mizinga baadhi yao walikuwa wanasoma Pale Tumaini University Iringa, kuna mida walikuwa wanaimba maeneo ya hostel, sasa wakiwa wanaimba wanatukana matusi makubwa makubwa huku wanavuta mabangi, moyoni nikawa najisemea ukiwa chuo kikuu ndio unakuwa ms***e kama hawa wahuni
 
Dudubaya anadai Kalapina na wahuni wenzake walitaka kumsulubu Chid Benz Bilcanas yeye na Nako to Nako soldiers wakamuokoa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…