chiembe
JF-Expert Member
- May 16, 2015
- 16,859
- 28,112
Prof Kabudi pamoja na Harrison Mwakyembe waliwahi kuwa waandishi wa habari wa magazeti ya uhuru na mzalendo(if I am not mistaken). Hii ilikuwa kabla, wakati na baada ya vita vya kagera.
Kwa maneno mengine, walikuwa wanajeshi walioongoza mapambano dhidi ya nduli Idd Amin kwa silaha ya kalamu, kuufahamisha umma kuhusu vita, na kupambana na Amin wakiwa newsroom.
Wino wao ulikuwa risasi iliyopenya sawia katika mwili na falsafa za kidikteta za nduli Idd Amin na kuacha maumivu makali.
Wali-shape hoja ya watanzania kwa nini wanaingia vitani. Walikuwa mdomo wa Mwalimu Julius Nyerere katika mawasiliano yake na umma. Walijua vision na mission ya taifa.
Kwa msingi huo, uzalendo wao, na mapenzi yao kwa taifa yalianza na kupikwa na sekta ya habari.
Baada ya hapo alijiunga na chuo bora kabisa nchi ni, chenye weledi usiopimika, UDSM.
Enzi hizo ili uwe mwandishi wa habari, lazima uwe kichwa kweli kweli, tofauti na sasa ambapo hata baba Levo ametoka kuvuta makokoro ya migebuka na kubeba magunia ya mikaa Mwandiga, analisha jamii mapupu. Au Zembwela kutoka kuvaa matambara ya kuchekeshea watu mpaka kukaa radio
Ni uteuzi mzuri ambao utaenda kuimarisha sekta ya habari.
Jerry Silaa amekosa fursa, kwa kuwa habari ni nguvu, yeye akiitwa na wanahabari anagoma. Sasa amebaki kuwa nyuki wa mashineni anatuimbia tu masikioni, na sisi wala hatustuki.