Watu wengi huongelea mabadiliko katika klabu ya yanga

Watu wengi huongelea mabadiliko katika klabu ya yanga

moodykabwe

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2015
Posts
625
Reaction score
602
WATU WENGI HUONGELEA MABADILIKO KATIKA KLABU YA YANGA


Lakini hawajui yanga ilishafanya Mabadiliko toka Mwaka 2007...Kwa mujibu ya Katiba ya yanga Ya mwaka 2010


mabadiliko haya ni kama ifwatavyo

*Ibara ya 56 Kampuni ya Umma ya Yanga*

1. Kutakuwa na Kampuni itakayojulikana kama *Young Africans Sports Corpration Limited* ambayo itasajiliwa chini ya sheria ya Makampuni kama kampuni ya Umma yenye hisa ("kampuni")



2. Wanachama wote wa klabu ambao katika tarehe ya marekebisho ya katiba ya mwaka 2007 wako hai watakuwa kwa nguvu ya uwanachama wao, wanahisa katika kampuni kwa kiwango cha idadi ya hisa watakazo pata kwa mujibu wa muafaka wa yanga uliofikiwa na wana_yanga tarehe 22.06.2006.



3. Klabu itamiliki hisa zilizo Sawa na asilimia Hamsini na moja (51℅) ya hisa zote zilizomo katika kampuni.


4. Mkutano Mkuu wa Uchaguzi utachagua wanachama wawili ambao sio miongoni mwa viongozi wa klabu kuwa wajumbe wa bodi ya wakurugenzi wa kampuni kwa ajili ya kuwakilisha maslahi ya klabu kwenye kampuni.



5. Kampuni itakuwa chombo Maalumu cha klabu kitakachokuwa na dhamana ya kufanya biashara ambazo klabu ya *Young Africans Sports club* itaona kuwa inafaa kwa ajili ya kujiimarisha kiuchumi.


6. Inawezekana yakawepo Makubaliano kati ya Kampuni na Klabu ili kampuni iweze kuendesha timu ya mchezo ikiwemo timu ya mpira Wa miguu ya klabu.



7. Kwa ajili ya kuweka utaratibu Mzuri wa kuendesha timu, klabu na Kampuni wataingia katika makubaliano ya kimaandishi kuhusiana na uendeshaji wa timu, makubaliano ambayo kwa niaba ya klabu yatasainiwa na Katibu Mkuu wa klabu.

*Mwisho wa kunukuu*


Ndugu zangu wana_yanga Hatupaswi kuhubiri mabadiliko ila tunapaswa kuwashindikiza viongozi wetu kwenda kusajili kampuni ya klabu yetu na mambo mengine yafwatie Tunahubiri mabadiliko tunacheleweshe wenyewe tu na wanasheria wetu wa klabu waongo kupita maelezo wanashindwa kuwaambia watu ukweli.......


Kama ni mabadiliko watu wa yanga tushafanya mabadiliko pekee ambayo mm ningeyaona ni sahihi ni kupunguza idadi ya wajumbe wa mkutano wa mku wa klabu

Kutoka wanachama Matawi na sasa tuingie kwenye mfumo wa viongozi wa matawi kuwa ndio wajumbe wa mkutano mkuu....



Kwa sababu sasa duniani tuko wengi sana na wanachama wa yanga tuko wengi sana kwa sasa hivi kwa mfano huu mfumo wa benk uliokuwa unaendelea kama watu wote wa yanga tungechukua kadi tungekaa wapi???



Kinachotakiwa klabu iwe na viongozi wenye maono nilazima tubadilike kwenye mfumo wa mikutano yetu kwanzia chini mpaka juu
Tufanye yanga INA matawi mia mbili tu kila tawi Liwe kweli lina wanachama 100 kama katiba inavyoelekeza inamaana tunakuwa na wanachama 2000 hawa utawaeka ukumbi gani na mtaongea nini muelewane????


Lakini tukifanya kila tawi litoe mwenyekiti na Katibu kila tawi tutakuwa watu 400 tu nchi nzima hawa 400 nchi nzima ni watu ambao nao wamechaguana kwenye matawi yao kitu ambacho kitatufanya kabla ya mkutano wa uchaguzi wa klabu kunafanyika uchaguzi kwenye matawi kwanza tukimaliza huko tunaingia kwenye klabu ngazi ya huu zaidi




Mabadiliko tunayoyataka kwenye klabu yetu yameshafanyika ni nani wa kututoa hapa tulipo ili tuyafikie??? Jibu hakuna kwakua tunaochagua nini sisi na tunaosema hawafai nini
Natamani niendelee ila nitawachosha kusoma



Nitaendelea tena kesho tukijaliwa

By
Moody Kabwe Comredy
 
Ndo ujue magazet bila yanga hayauzki
 
Umeeleza vyema ila ktk mabadiliko sijaona nafasi ya mzeee mwenye akili kushinda wana yanga wote,gwiji Mzee Akilimali.Tambua kuwa kufanya mabadiliko yoyote ndani yanga pasipo kumshirikisha Akilimali ni kujisumbua labda atoe baraka zake.Swali kabla hatujarefusha mjadadala,je Mzee alishirikishwa ktk kuandaa mabadiliko hayo?
 
Back
Top Bottom