Watu wengi wako Smart Nyuma ya Keyboard na wengine Kinyume Chake!

Watu wengi wako Smart Nyuma ya Keyboard na wengine Kinyume Chake!

Ryzen

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2012
Posts
7,301
Reaction score
8,706
Majira Haya ya saa tatu kasoro usiku huu nikiwa nyuma ya keyboard ya computer yangu nikiwa natafakari mambo kadha wa kadha hili wazo limenijia kichwani. Nikachukulia kama jambo dogo ila naona akili yangu haitaki kuipa nafasi ya kulipotezea.

Kwa mfano hapa JamiiForums wapo watu wengi wapo smart sana nyuma ya keyboard (Wanaandika vitu sensitive na smart), pia wapo ambao ni kinyume cha hapo yaani wao wana uwezo wa kuponda na lugha za matusi.

Lakini pia nikawa najiuliza hawa watu pia wako smart katika maisha ya kawaida? sometime natamani kuonana nao japo nipate kuzungumza nao nigain kitu (Kati ya watu watatu naamini kuna mwalimu atayenifunza jambo ambalo silijui).

Lakini pia hawa wa upande wa pili natamani hata kukutana nao nijue tofauti na nyuma ya keyboard huwa wapo hivi? najua pia ningepata cha kujifunza kutoka kwao.

Hongereni Nyote ambao Mnaonesha usmart wenu Pamoja na kwamba Hatujuani!
 
dunia haiku sawa kimaisha wengine wanatafuta mlo mmoja wengine wanasaza
 
Lakini pia hawa wa upande wa pili natamani hata kukutana nao nijue tofauti na nyuma ya keyboard huwa wapo hivi? najua pia ningepata cha kujifunza kutoka kwao.
😀😀
Nje ya keyboard ni watu wastaarabu kweli yani huwezi amani kile wanachokiandika humu na matendo yao...
 
Ukiona comment MTU anajifanya hajui ujue imemgusa moja kwa moja
 
😀😀
Nje ya keyboard ni watu wastaarabu kweli yani huwezi amani kile wanachokiandika humu na matendo yao...
Nafikiri Hii tabia ya Nyuma ya keyboard ndio tabia Halisi ya Mtu, kwa maana si anakuwa huru na id fake!
 
Back
Top Bottom